Raza arusha kombora zito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raza arusha kombora zito!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, Aug 30, 2011.

1. Felixonfellix

Felixonfellix JF-Expert Member

#1
Aug 30, 2011
Joined: Feb 16, 2010
Messages: 1,680
Likes Received: 4
Trophy Points: 135
Raza arusha kombora zito

By Mwinyi Sadallah

30th August 2011

Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza.
Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika hatari ya kupoteza wanachama wake kama kitaendelea kukumbatia viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa za ufisadi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Raza alisema wakati umefika kwa Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi mazito ya kuwafukuza viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa CCM kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
"Viongozi wanaoshindwa kuzingatia maadili watimuliwe, haiwezekani mamilioni ya fedha yanaibiwa wakati huduma za jamii zikiendelea kuanguka nchini," alisema Raza.

Hata hivyo, alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Kikwete za kupambana na ufisadi zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wenzake ili lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania lifikiwe.

"Uongozi wake Rais Kikwete hivi sasa anateremka kilima, lakini tunaweza kupoteza na kupunguza wanachama kama watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi hawatachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola," alisema Raza.

Alisema viongozi wengi wameshindwa kuheshimu misingi ya maadili ya uongozi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.

"Maadili waliyotuachia waasisi wa taifa hayapo tena Tanzania, kila mtu kawa mbabe sasa hatuna kiongozi katika nchi anayekemea maovu," alisema Raza.

Alieleza kuwa rasilimali nyingi za nchi zinachukuliwa na kupotea huku Taifa likikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na wanafunzi kuendelea kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.
Alisema ni jambo la kushangaza kwamba Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyokwapua mabilioni ya fedha, hadi sasa wahusika hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.

Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. milioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema wakati Watanzania Bara wakikabiliwa na tatizo sugu la mgawo wa umeme, Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua hadi sasa viongozi wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.

Alisema wahusika katika kashfa ya ununuzi ya rada na wizi wa fedha za EPA lazima wakamatwe ili kulinda misingi ya sheria na utawala bora nchini.
"Kiongozi ukipata tuhuma tu katika chama inatosha kujiuzulu, usisubiri hadi uingizwe hatiani na vyombo vya sheria," alisema Raza.
Alisema viongozi wa Afrika lazima wajifunze kwa kuangalia mfano wa yaliyotokea Misri baada ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Hosni Mubarak, alivyopelekwa mahakamani baada ya kuondolewa madarakani akiwa katika machela.

"Tumeona mfano Misri, aliyekuwa Rais kapelekwa mahakamani akiwa kabebwa katika machela … ndio maana nasema mafisadi wachukuliwe hatua kabla ya kulifikisha taifa pabaya," alisema.

Alisema iwapo rasilimali za nchi zingesimamiwa vizuri na serikali, leo watoto wasingesoma wakiwa chini wala wananchi kukosa dawa katika hospitali na vituo vya afya pamoja na kutembea masafa marefu kusaka maji safi.

"Leo tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, watoto wetu wanasoma wakiwa wamekaa chini, hospitali zetu zina uhaba wa dawa, yote haya ni kukosekana kwa maadili ya uongozi," alisema Raza.

Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema marekebisho ya katiba mpya yafanyike kwa umakini mkubwa ili kuendeleza umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.

Alisema ni vizuri wananchi wakapewa uhuru wa kutosha kujadili na kuamua muundo wa Muungano wanaoutaka.
Hata hivyo, alisema kwamba Tume ya Katiba Mpya hakuna sababu ya kupangiwa zaidi ya miaka miwili kwa vile suala hilo linaweza kukamilika ndani ya miezi sita iwapo nia njema itakuwepo katika mabadiliko ya katiba.

Alipendekeza kuwa wabunge na wawakilishi wapewe uhuru wa kutosha wa kuamua wananchi wanataka Muungano wa aina gani na wajiepushe na kauli ambazo zinaweza kuibua matatizo wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya.

Raza ambaye aliwahi kuwa Mshauri wa mambo ya Michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alisema Wazanzibari sio kunguru wala ndege ndani ya Muungano na kuwataka wabunge kuzingatia misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar badala ya kutoa kauli ambazo hazisaidii kujenga umoja wa kitaifa.

Kwa mujibu wa Raza, Wazanzibari wanaunga mkono Muungano, lakini uwe na maslahi ya kiuchumi kwa pande zote.  SOURCE: NIPASHE

2. Mwita25

Mwita25 JF-Expert Member

#2
Aug 30, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 3,840
Likes Received: 18
Trophy Points: 0
Tumewazoea mavuvuzela hao, watapiga kelele weee lakini JK yupo palepale.

3. Mimibaba

Mimibaba JF-Expert Member

#3
Aug 30, 2011
Joined: Jul 1, 2009
Messages: 4,566
Likes Received: 7
Trophy Points: 0
Nimekuzoea Tarumbeta langu, hata kama unanipia out of tune.

4. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#4
Aug 30, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,967
Trophy Points: 280
Ccm imekwisha.......
Ccm imeoza........
Ccm inanuka........,
haiwez kutufikisha.

5. C

Cognitivist JF-Expert Member

#5
Aug 30, 2011
Joined: Aug 7, 2011
Messages: 777
Likes Received: 983
Trophy Points: 180
Atamfukuza nani, amwache nani? Wote mafisadi, na wanafiki kibao. Wapi Msekwa na ngorongoro yetu.

6. Elli

Elli JF-Expert Member

#6
Aug 30, 2011
Joined: Mar 17, 2008
Messages: 26,828
Likes Received: 10,140
Trophy Points: 280
angeseam chadema wangeseam akwasababu ni wapinzani wa kila kitu kazi yao kupinga, haya sasa huyo ni mtoto wa familia hio hio, sijui watasema katumwa na jirani kumtukana baabake/kumweleza ukweli? mmh hata siju watsemaje mwayego

7. Mwendabure

Mwendabure JF-Expert Member

#7
Aug 30, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 2,056
Likes Received: 300
Trophy Points: 180
Katumwa na JK ili kujaribu kumtishia nyau EL. Kweli EL ni mwiba kooni mwa JK.

8. Vin Diesel

Vin Diesel JF Gold Member

#8
Aug 30, 2011
Joined: Mar 1, 2011
Messages: 8,402
Likes Received: 738
Trophy Points: 280
Ni wakati muafaka sasa kwa viongozi wa ngazi ya juu ndani ya CCM kufanya maamuzi magumu ya kuwatema moja kwa moja watuhumiwa wote wa ufisadi.
Wimbo wa kujivua gamba unaelekea kuchosha masikio na mantiki yake itatoweka muda mfupi ujao uamuzi utazidi chelewa.

9. Kalunguine

Kalunguine JF-Expert Member

#9
Aug 30, 2011
Joined: Jul 27, 2010
Messages: 2,544
Likes Received: 7
Trophy Points: 135

Sasa huyu Raza anatuambia nini? Hizo juhudi za kuungwa mkono ni zipi? Unafiki mtupu!

10. Crashwise

Crashwise JF-Expert Member

#10
Aug 30, 2011
Joined: Oct 23, 2007
Messages: 22,172
Likes Received: 862
Trophy Points: 280
hata gadafi alisema hivyo hivyo lakini leo inaishi shimoni kama mavi, endeleni kumpa moyo kikwete

11. Bishop Hiluka

Bishop Hiluka Verified User

#11
Aug 30, 2011
Joined: Aug 12, 2011
Messages: 4,101
Likes Received: 1,425
Trophy Points: 280
Ni kweli anafanya uungwana kutochukua hatua, maana kama ataamua kufukuza mafisadi
huenda chama kikafa maana sijui kina nani watabaki?...

12. Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu JF-Expert Member

#12
Aug 30, 2011
Joined: Oct 12, 2010
Messages: 4,986
Likes Received: 427
Trophy Points: 180
Wanapiga kelele JK yupo pale akiwalinda wezi na mafisadi, unafurahi siyo????????? Subiri ya Libya watu watadai uhuru wa nchi yao!!!!!!!!

13. U

Ulimakafu JF-Expert Member

#13
Aug 30, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 18,015
Likes Received: 743
Trophy Points: 280
Yeye ni msafi,maana wote huko wana mashaka makubwa.

14. T

Tata JF-Expert Member

#14
Aug 30, 2011
Joined: Dec 3, 2009
Messages: 4,738
Likes Received: 658
Trophy Points: 280
Hii CCM imekuwa kama bwawa la kambale (cat fish). Kambale wakiwa pamoja huwezi kujua nani baba, mama, dada au kaka kwa sababu wote wana ndevu. CCM kila mtu anaibuka na kutoa matamko yasiyokuwa na tija yoyote.

15. M

Mthuya JF-Expert Member

#15
Aug 30, 2011
Joined: Jun 9, 2011
Messages: 1,415
Likes Received: 65
Trophy Points: 145
Wacha wafu wazike wafuwao  Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza.

Mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo katika hatari ya kupoteza wanachama wake kama kitaendelea kukumbatia viongozi wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa za ufisadi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar, Raza alisema wakati umefika kwa Rais Jakaya Kikwete kufanya maamuzi mazito ya kuwafukuza viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi ili kurejesha imani kwa wananchi na wanachama wa CCM kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

“Viongozi wanaoshindwa kuzingatia maadili watimuliwe, haiwezekani mamilioni ya fedha yanaibiwa wakati huduma za jamii zikiendelea kuanguka nchini,” alisema Raza.

Hata hivyo, alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Kikwete za kupambana na ufisadi zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wenzake ili lengo la maisha bora kwa kila Mtanzania lifikiwe.

“Uongozi wake Rais Kikwete hivi sasa anateremka kilima, lakini tunaweza kupoteza na kupunguza wanachama kama watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi hawatachukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola,” alisema Raza.

Alisema viongozi wengi wameshindwa kuheshimu misingi ya maadili ya uongozi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.

“Maadili waliyotuachia waasisi wa taifa hayapo tena Tanzania, kila mtu kawa mbabe sasa hatuna kiongozi katika nchi anayekemea maovu,” alisema Raza.

Alieleza kuwa rasilimali nyingi za nchi zinachukuliwa na kupotea huku Taifa likikabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na wanafunzi kuendelea kukaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.

Alisema ni jambo la kushangaza kwamba Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyokwapua mabilioni ya fedha, hadi sasa wahusika hawajachukuliwa hatua zozote za kisheria.

Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. milioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema wakati Watanzania Bara wakikabiliwa na tatizo sugu la mgawo wa umeme, Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua hadi sasa viongozi wanaohusishwa na vitendo vya ufisadi.

Alisema wahusika katika kashfa ya ununuzi ya rada na wizi wa fedha za EPA lazima wakamatwe ili kulinda misingi ya sheria na utawala bora nchini.

“Kiongozi ukipata tuhuma tu katika chama inatosha kujiuzulu, usisubiri hadi uingizwe hatiani na vyombo vya sheria,” alisema Raza.

Alisema viongozi wa Afrika lazima wajifunze kwa kuangalia mfano wa yaliyotokea Misri baada ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Hosni Mubarak, alivyopelekwa mahakamani baada ya kuondolewa madarakani akiwa katika machela.

“Tumeona mfano Misri, aliyekuwa Rais kapelekwa mahakamani akiwa kabebwa katika machela … ndio maana nasema mafisadi wachukuliwe hatua kabla ya kulifikisha taifa pabaya,” alisema.

Alisema iwapo rasilimali za nchi zingesimamiwa vizuri na serikali, leo watoto wasingesoma wakiwa chini wala wananchi kukosa dawa katika hospitali na vituo vya afya pamoja na kutembea masafa marefu kusaka maji safi.

“Leo tunaadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, watoto wetu wanasoma wakiwa wamekaa chini, hospitali zetu zina uhaba wa dawa, yote haya ni kukosekana kwa maadili ya uongozi,” alisema Raza.

Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema marekebisho ya katiba mpya yafanyike kwa umakini mkubwa ili kuendeleza umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.

Alisema ni vizuri wananchi wakapewa uhuru wa kutosha kujadili na kuamua muundo wa Muungano wanaoutaka.

Hata hivyo, alisema kwamba Tume ya Katiba Mpya hakuna sababu ya kupangiwa zaidi ya miaka miwili kwa vile suala hilo linaweza kukamilika ndani ya miezi sita iwapo nia njema itakuwepo katika mabadiliko ya katiba.

Alipendekeza kuwa wabunge na wawakilishi wapewe uhuru wa kutosha wa kuamua wananchi wanataka Muungano wa aina gani na wajiepushe na kauli ambazo zinaweza kuibua matatizo wakati huu wa mchakato wa Katiba Mpya.

Raza ambaye aliwahi kuwa Mshauri wa mambo ya Michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alisema Wazanzibari sio kunguru wala ndege ndani ya Muungano na kuwataka wabunge kuzingatia misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar badala ya kutoa kauli ambazo hazisaidii kujenga umoja wa kitaifa.

Kwa mujibu wa Raza, Wazanzibari wanaunga mkono Muungano, lakini uwe na maslahi ya kiuchumi kwa pande zote.

SOURCE: NIPASHE[/QUOTE]

16. T

Taifa_Kwanza JF-Expert Member

#16
Aug 30, 2011
Joined: Sep 3, 2010
Messages: 443
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Yes, ni kweli kabisa, amesimama pale pale, haendi mbele, harudi nyuma, aruki, achutami, kama mzoga fulani hivi...

17. TOWNSEND

TOWNSEND JF-Expert Member

#17
Aug 30, 2011
Joined: May 8, 2011
Messages: 2,597
Likes Received: 48
Trophy Points: 145
jk aliwahi kusema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala masikini sijui lini atafurahia uraisi wake ..gadafi aliwaita watu wake rats wavuta unga leo sijui yuko wapi tunaoneshwa tu alikuwa anaishi hapa pale .....yote laana ya viapo ...mbaya sana

18. Bigirita

Bigirita JF-Expert Member

#18
Aug 30, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 13,976
Likes Received: 689
Trophy Points: 280
kumbe umeligundua hilo.....
Hata mm sikuelewa alikuwa ana maanisha nini.

19. Chakunyuma

Chakunyuma JF-Expert Member

#19
Aug 30, 2011
Joined: Apr 10, 2011
Messages: 811
Likes Received: 1
Trophy Points: 35

ni kweli uliyoyasema kikubwa ni kuwepo na utaratibu ambao hautaruhusu uwepo wa viongozi ambao c waadilifu kwa kufanya nomination mapema labda miezi 18 kabla ya uchaguzi ili kuzipa taasisi kuwachunguza wagombea wote na pia kuwapatz muda wa kuwafahamu na kuwafuatilia.

20. shegaboy

shegaboy JF-Expert Member

#20
Aug 30, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 214
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Tunakushukuru sana Raza ila unajua kuwa kama akisema amfukuze yeyote yule anayetuumiwa nayeye chali kaenda na maji.
1. Edwad Lowasa huyu anatuuma za Rachmond . Ok unaweza kuniambia kwanini hawakumpa muda wa kujieleza na pia walimzuia Rostam Azizi asiongee pale bungeni unaweza kutoa sababu Raza?
2. Andrew Chenge - Rada jamani raza unaweza kuniambia wakati chenge anaingia mikataba kikwete alikuwa wapi si waziri wa mambo ya nje jamaa anakwenda kununua rada yeye yuko ndio kila kitu kilikuwa kinashughulikiwa hukowizarani jamani. jk atoki hapo

tumuonee huruma jamani CCM imesha katika sijui watanzania wanataka nini kujua hili sitaki kusema Rais wetu kashindwa kuongoza ingawa hakuna mwenye uhakika na hilo ila.
1.Kweli mpaka leo hatuna wakuu wa mikoa je kuna mtu analijua hilo .
2.wakuu wa wilaya awajateuliwa mpaka leo nchi watu wanakaimu tu wanakula mishahara miwili miwili ila ngojeni tu nasema viongozi wengi wa ccm watakimbia hii nchi nawaambia mtashangaa.

Loading...