Ray na wenzake wameukashifu ukatoliki

Ray na wenzake wameukashifu ukatoliki

Imani ipo rohoni. Mavazi si kitu. Akiukashifu ukatoliki dhambi zitabaki kuwa zake. Hatuna muda wa kuandamana sababu huo ni mtazamo wake. Huo muda wa kuandamana ni bora utumike kumuombea kwa mungu na kumwelimisha (kama kweli amekashifu) Hakuna aliye msafi 100% ila Mungu peke yake!
 
wangekuwa wamediss uislam kingenuka sasa hivi,lakin sisi tunapotezea hatuna muda wa kulipiza
 
kweli wakatoliki tuandamane?

Kisa mavazi?

Ili iweje?

Kwani wakiyavaa wanapunguza ukatoliki?????

Afterall wakatoliki wana mavazi????????????????
.
 
Huko dinioi ilipoanzia wanacheza movies wanamwigiza mpaka pope leo wewe unaleta udaku kina Ray wamevaa mavazi ya kikatoliki (padre n' sister) unatoa povu wamezalilsha ukatoliki...Ukatoliki upi unaouzungumzia wewe!
 
Wakatoliki ni watu wenye hekima kupindukia. Hawatoandamana kwa upuuzi huo wa Ray na hao changudoa wake. Yaani waache vikao vya kujenga mashule,hospital na miradi ya maendeleo waandamane!. You must be out of your mind! Labda wangekuwa kina nanihiu ndio wangeandamana
 
Sijaona kosa hapo!yani watu waandamane kisa movie ya ray!

Hakuna kashifa hapo hiyo ni kawaida, kwanza dini hazipo kwenye mavazi sema watu hawaelewi tuu!
 
Back
Top Bottom