Ray atetea uamuzi wa kumvisha hereni mtoto wake ambaye ni wa kiume

Mbona wamasai wanavaa hereni na kutoboa masikio?
Wamakonde wamalaba walikuwa wanasifika kwa tattoo zao kama za watu wa Amazon.
Saa nyingine Westernization inawafanya muone baadhi ya tabia na mila za kiafrika kama tumeigiza kutoka ulaya, wakati wao ndiyo wameigiza kutoka kwetu.
Nyinyi mnaopiga kelele ndiyo mna matatizo ya kisaikolojia, kwanini mtoto mdogo kama yule muanze kumpangia future yake kisa amevaa hereni?
Wengine utotoni mmevaa magauni ila hamjijui tu, Enzi za zamani ilikuwa kawaida mtoto wa kiumwe kuvalishwa gauni. Mnabisha?
YAN KWA LUGHA RAHIS
ZAMAN WATOTO WAKIUME WALIKUA
WANAVAA SAWA NA WA KIKE ?? KWAHIYO
NI SAWA??
 
Kama ni wa kwake amuue kama hajanyea debe
Unafananisha kumvisha hwreni ma kumuua?

You shouldn't compare apples with oranges out of context.

Nimeongelea kuua hapo juu. Soma thread.

Sasa wewe mtu baki anamvisha mwanawe hereni kinachomuuma kipi?
 
Hivi mtoto wa Will Smith, Jaden Smith anaendeleaje kwa sasa, last time nilimsoma kuwa anapenda kuvaa nguo za kike nikamuona kavaa sketi
 
Sasa kwa nini utoboe sikio uvae hereni uchore tattoo
Kwa sababu katiba, Univwrsal Declaration of human rights na Bob Marley, ukiachilia mbali wajuvi wa mahusiano ya kijamii, wote wanasema kila mtu aachiwe kuishi anavyotaka ili mradi hajavunja sheria na kumuingilia mwingine.

Ray angemtoboa sikio mwanao na kumvisha hereni wakati wewe hutaki angekuwa kakuingilia. Ungekuwa na haki ya kumsema kakosea.

Hajamtoboa mwanao. Kamtoboa wake.

Ukitaka kumpangia asimtoboe sikio mwanawe, akasema sawa, hatamtoboa kwa sharti na yeye akupangie amtoboe wako na kumvisha hereni, utakubali au utakataa?

Itakuwaje unataka kumpangia mtu mzima ambaye hajavunja sheria jinsi ya kumlea mwanawe?
 
Watu kwa kufwatilia vitu vyepesi bhana!!!!!!! ???

Ndio maana mapolisi wanakimbizana na wanyoa viduku kwasababu ya huu huu u-gorilla!!

Swala la Ray na mwanae limekuwa swala la umma mzima wa watanzania.

No wonder, mtu akiamua kufanya ushoga juu ya mwili wake mwenyewe inageuka kuwa mjadala na swala zito linalotikisa bara zima la Afrika!!

Teh......
 
Hapana. Habari za mtoto ni wa jamii zimeisha enzi za ujima.

Watoto wangekuwa wa jamii kusingekuwa na tofauti kati ya Feza Secondary na Mbavuzambwa Sekondari.
Matabaka ya kibeberu ndio yanayotutenganisha
 
Matabaka ya kibeberu ndio yanayotutenganisha
Na ndiyo yashatutenganisha sasa. Kwa nini tunakataa ukweli?

Ray anataka kuishi Kinyamwezi kama celebrity. Ndivyo alivyoamua.

Anataka kumlea mwanawe aje kuwa kama Jayden Smith wa bongo, na hatimaye mtoto awe mcheza filamu.

Mkulima asiyejua habari za celebrities kwa nini anataka kumlazimisha Ray aishi kama mkulima? Wakati Ray hajamlazimisha mkulima kuishi kama celebrity.
 
Huyu ana matatizo hata kama ni maarufu hivi hao wa ulaya wanafanyaga kama hayo. Halafu Ray ana kaushamba flani hivi huwa hakatoki na tabia nayo imekuwa ngumu kubadilika
 
YAN KWA LUGHA RAHIS
ZAMAN WATOTO WAKIUME WALIKUA
WANAVAA SAWA NA WA KIKE ?? KWAHIYO
NI SAWA??
Kwanini isiwe sawa? Watoto wa zamani si ndiyo hawa baba zetu wanaopanga hizi sheria? Au tunapangiwa na kina nani?
 
Ulimbukeni wa dizaini ya wakina Ray, ni hatari zaidi ya bomu la Hiroshima.
 
Jina langu la "Al-Watan" linakufanya uelewe nini kuhusu mimi?

Na utajuaje kwamba hata mtu anayejiita "Kichaa" hafanyi social experiment kuangalia jinsi akili yako ilivyo ndogo kwa kufikiri kwamba mtu anayejiita "Kichaa" ni kichaa kweli kwa sababu kajiita "Kichaa" JF ?

Zaidi, check your faulty logic.

Kumuwekea hereni mtoto si "kufanya kitu chochote".

Kwa sababu, "kufanya kitu chochote" kunajumuisha kumchoma kisu na kumuua. Na kumuwekea hereni si sawa na kumchoma kisu na kumuua.

Unajichanganya kwa kukosa kuweza kuandika kwa mantiki.

Mimi binafsi sipendi habari za kuvaa hereni wala kuweka tattoo, na nimezibukia Umarekani tangu mdogo, nipo Marekani miaka kibao, nchi ambayo watu wanaruhusu mpaka mtangazaji wa habari anayeheshimika kutoboa sikio na kuvaa hereni huku anatangaza habari kwenye TV.

Sijatoboa sikio wala kuvaa hereni. Hata tattoo ya ngama sina. Wakati huku mpaka ma profesa wa chuo kikuu wanatoboa masikio kuvaa hereni na kuweka tattoo.

Lakini, kutofagilia kwangu kuvaa hereni hakuzidi kutofagilia kwangu mzazi kuingiliwa katika malezi ya mwanawe kwa jinsi anavyoona yeye ni bora. Almuradi hajavunja sheria.

Pengine Ray anamuandaa mwanawe kuwa mcheza filamu, na katika jumuiya yao kutoboa sikio kuvaa hereni si issue. Na labda ndiyo kwanza itampandisha chati mwanawe, watu wamzungumzie kama unavyomzungumzia hapa. Kwa kanuniya "no publicity is bad publicity". Kama anaamini hivyo.

Sasa nyie watu baki mnamuingilia ili iweje?

Wabongo tunajali sana superficial appearance bila kuangalia deep issues.

Ndiyo maana wajanja wanatujulia wanakuja na wazungu wamevaa suti kali tunapigwa mikataba mpaka tunalia lia makinika.

Watu wanashupalia mtoto kavishwa hereni kama wameshiriki kumzaa.

Ukiwauliza mwanao ana college fund? Vichekesho vitupu.
Naomba mfano wa huyo mtangazaji please
 
Back
Top Bottom