Mwanamke Jela miaka 29 kwa kumbaka mtoto mdogo wa kiume mwenye miaka 8

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Mahakama ya Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Lumuli wilayani Iringa, Desderia Mbwelwa (57) (katikati) miaka 29 jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingoni (grave sexual harassment) mtoto wa kiume mwenye miaka nane wakati kijana huyo akiwa anachunga ng’ombe ndipo mama huyo akamlazimisha kufanya naye mapenzi.

Picha na Friday Simbaya
---

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 29 jela mwanamke wa Kijiji cha Lumuli, Desderia Mbwelwa (57) kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na kumsababishia magonjwa ya zinaa. Iringa.

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 29 jela mwanamke wa Kijiji cha Lumuli, Desderia Mbwelwa (57) kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na kumsababishia magonjwa ya zinaa.

Siku ya tukio mwanamke huyo alimkuta mtoto ambaye ni mwathirika wa tukio hilo akiwa anachunga ng'ombe kisha akamuuliza wenzake wako wapi na alipojibiwa kuwa wenzake hawapo ndipo akambaka akiwa chini ya mti.

Kesi hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Said Mkasiwa na ilikuwa na mashahidi watano akiwemo daktari aliyempima mtoto na kuthibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa na michubuko na aliambukizwa magonjwa ya zinaa kutokana na kutokwa uchafu eneo la haja ndogo.

Mahakama ilimpa nafasi ya kujitetea, Desderia amesema yeye ni mtu mzima na kuwa ana watoto na wajukuu wanaomtegemea, ndipo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka 29 jela kwa kosa la ukatili wa kingono kwa mtoto wa miaka 8 pamoja na kumsababishia magonjwa ya zinaa.

Hata hivyo Wakili wake, Frank Mwela amesema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kuwa mteja wake hakupimwa ili kubaini kama kweli ana magonjwa hayo ya zinaa.

"Mteja wangu hakupimwa kuonekana na magonjwa hayo ambayo mteja wangu na shahidi wake wamethibitisha kuwa wao magonjwa hayo hawana kwa sababu shahidi mmoja wapo ni mume wake," amesema.

Desderia ambaye ana miaka 57 ameanza kutumikia kifungo hicho cha miaka 29, huku wakili wake akiendelea kushughulikia taratibu za kukata rufaa.
 
Back
Top Bottom