Ray atetea uamuzi wa kumvisha hereni mtoto wake ambaye ni wa kiume

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Dar es Salaam. Msanii wa filamu, Vincent Kigosi maarufu ‘Ray’ amesema kitendo cha kumvisha mtoto wake hereni ni kutokana na kuwa nyota kama yeye.

Ray amesema hayo alipozungumza na MCL Digital baada ya kuweka hadharani picha za mtoto huyo wa kiume aliyevishwa hereni hivyo kuzua gumzo. Maoni kadhaa yamekuwa yakitolewa kuhusu kitendo hicho pamoja na kunyolewa nywele staili ya kiduku.

Akizungumzia uamuzi wa kufanya hivyo kwa mtoto wake wa pekee aitwaye Jaden, msanii huyu aliyewahi kutamba na filamu za Oprah, Waves of Sorrow na Pretty amesema yeye ni nyota maarufu hivyo mtoto wake lazima afuate nyayo zake.

“Mbona mimi baba yake nimetoboa masikio watu hawasemi, si kwa kuwa wanajua mimi ni mtu maarufu, hivyo umaarufu huu nilionao hata mtoto lazima awe nao japo sijamtoboa sikio atakuja kufanya hivyo mwenyewe kama ataamua atakapokuwa mkubwa,” amesema.

Ray amesema, “Hao wanaosema waendelee tu kusema kwa kuwa kusema ni haki yao, na huyu ni mwanangu hakuna mtu wa kunipangia nini cha kumfanyia.”

mwananchi
 
Mbona wamasai wanavaa hereni na kutoboa masikio?
Wamakonde wamalaba walikuwa wanasifika kwa tattoo zao kama za watu wa Amazon.
Saa nyingine Westernization inawafanya muone baadhi ya tabia na mila za kiafrika kama tumeigiza kutoka ulaya, wakati wao ndiyo wameigiza kutoka kwetu.
Nyinyi mnaopiga kelele ndiyo mna matatizo ya kisaikolojia, kwanini mtoto mdogo kama yule muanze kumpangia future yake kisa amevaa hereni?
Wengine utotoni mmevaa magauni ila hamjijui tu, Enzi za zamani ilikuwa kawaida mtoto wa kiumwe kuvalishwa gauni. Mnabisha?
 
Mbona wamasai wanavaa hereni na kutoboa masikio?
Wamakonde wamalaba walikuwa wanasifika kwa tattoo zao kama za watu wa Amazon.
Saa nyingine Westernization inawafanya muone baadhi ya tabia na mila za kiafrika kama tumeigiza kutoka ulaya, wakati wao ndiyo wameigiza kutoka kwetu.
?

Kabisa. Wasukuma walikuwa wakisuka pia, hata wanaume haswa wacheza ngoma. Sasa hivi ukila msuko, ati unaonekana unaiga umagharibi!
 
Ukisema kwamba unaweza kujua uwezo wa kufikiri wa mtu kwa kuangalia jina lake tu, tena jina bandia la JF, unaidhihirishia dunia ufinyu wa uwezo wako wewe wa kufikiri.

Dude, kama unadhani unaweza kufanya kitu chochote kwenye mwili wa mtu mwingine sababu tu umemzaa, basi we upeo wako wa kufikiri ni finyu. By the way, haya majina bandia yanasaidia sana kumfahamu mtu yuko vipi kichwani.
 
Kabisa. Wasukuma walikuwa wakisuka pia, hata wanaume haswa wacheza ngoma. Sasa hivi ukila msuko, ati unaonekana unaiga umagharibi!
Kuna kundi la watu lipo Tanzania linajaribu sana kuingiza masuala ya dini kwenye maisha ya kila siku ya watanzania. Tusipokubali diversity na freedom of expression, tutakuja kuishia mahali pabaya sana kama jamii.
Hivi hamjiulizi kwanini madiwani wanavaa majoho na mawigi ya kijivu? What the hell is that? Hiyo asili yake ni Tanzania kweli?
Badala ya kuondokana na utumwa wa kimawazo ili kukuza uvumilivu, tunajielekeza kwenye utumwa huohuo na matokeo yake tutakuja kujuta huko mbele.
People are getting so intolerant and non-compromising. Its so stupid!
 
Dude, kama unadhani unaweza kufanya kitu chochote kwenye mwili wa mtu mwingine sababu tu umemzaa, basi we upeo wako wa kufikiri ni finyu. By the way, haya majina bandia yanasaidia sana kumfahamu mtu yuko vipi kichwani.
Kwa hiyo ukimtahiri mwanao ni kosa?
 
Dude, kama unadhani unaweza kufanya kitu chochote kwenye mwili wa mtu mwingine sababu tu umemzaa, basi we upeo wako wa kufikiri ni finyu. By the way, haya majina bandia yanasaidia sana kumfahamu mtu yuko vipi kichwani.

Jina langu la "Al-Watan" linakufanya uelewe nini kuhusu mimi?

Na utajuaje kwamba hata mtu anayejiita "Kichaa" hafanyi social experiment kuangalia jinsi akili yako ilivyo ndogo kwa kufikiri kwamba mtu anayejiita "Kichaa" ni kichaa kweli kwa sababu kajiita "Kichaa" JF ?

Zaidi, check your faulty logic.

Kumuwekea hereni mtoto si "kufanya kitu chochote".

Kwa sababu, "kufanya kitu chochote" kunajumuisha kumchoma kisu na kumuua. Na kumuwekea hereni si sawa na kumchoma kisu na kumuua.

Unajichanganya kwa kukosa kuweza kuandika kwa mantiki.

Mimi binafsi sipendi habari za kuvaa hereni wala kuweka tattoo, na nimezibukia Umarekani tangu mdogo, nipo Marekani miaka kibao, nchi ambayo watu wanaruhusu mpaka mtangazaji wa habari anayeheshimika kutoboa sikio na kuvaa hereni huku anatangaza habari kwenye TV.

Sijatoboa sikio wala kuvaa hereni. Hata tattoo ya ngama sina. Wakati huku mpaka ma profesa wa chuo kikuu wanatoboa masikio kuvaa hereni na kuweka tattoo.

Lakini, kutofagilia kwangu kuvaa hereni hakuzidi kutofagilia kwangu mzazi kuingiliwa katika malezi ya mwanawe kwa jinsi anavyoona yeye ni bora. Almuradi hajavunja sheria.

Pengine Ray anamuandaa mwanawe kuwa mcheza filamu, na katika jumuiya yao kutoboa sikio kuvaa hereni si issue. Na labda ndiyo kwanza itampandisha chati mwanawe, watu wamzungumzie kama unavyomzungumzia hapa. Kwa kanuniya "no publicity is bad publicity". Kama anaamini hivyo.

Sasa nyie watu baki mnamuingilia ili iweje?

Wabongo tunajali sana superficial appearance bila kuangalia deep issues.

Ndiyo maana wajanja wanatujulia wanakuja na wazungu wamevaa suti kali tunapigwa mikataba mpaka tunalia lia makinika.

Watu wanashupalia mtoto kavishwa hereni kama wameshiriki kumzaa.

Ukiwauliza mwanao ana college fund? Vichekesho vitupu.
 
Back
Top Bottom