Ratiba ya maandamano 2026

Ratiba ya maandamano 2026

Mshana wewe ni mtu mkubwa sana hichi ulichoandika sjui ulikuwa unajua effect zake upande wako maana humu tutakusifia tu na kukufanya uonekane shujaa but behind the scene kitachotokea hakuna mtu mwenye msaada humu zaidi ya pole za mdomo
Maadhimisho ya mwaka mmoja ya matukio na mauaji ya MO29 (Oktoba 29) yanatarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 29, 2026 nchini Tanzania.

Harakati na maandalizi haya yanatokana na kumbukumbu ya machafuko, maandamano makubwa, na vifo vilivyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.

Raia na wanaharakati mbalimbali, ikiwemo makundi ya vijana (GenZ) na vyama vya siasa, wamekuwa wakihamasishana kutumia siku hii kama alama ya kuwakumbuka na kuwaenzi wahanga waliopoteza maisha au kujeruhiwa katika matukio hayo.
 
Minaona ni Titi sio Ziwa...View attachment 3625040
142d8af1-3bc5-429b-8bcb-5c7121b7cc84.jpeg
 
Mshana wewe ni mtu mkubwa sana hichi ulichoandika sjui ulikuwa unajua effect zake upande wako maana humu tutakusifia tu na kukufanya uonekane shujaa but behind the scene kitachotokea hakuna mtu mwenye msaada humu zaidi ya pole za mdomo
Mmh sijaandika chochote kibaya lakini.. Haya ndio yanasemwa daily mitandaoni..
 
Mmh sijaandika chochote kibaya lakini.. Haya ndio yanasemwa daily mitandaoni..
Halafu maandamano siyo kosa la jinai! Vitisho ni vya nini tena!!

Mbona siku chache tu zilizopita Yanga na simba walifanya parade zao zilizoambatana na maandamano makubwa, na hatukuona yakipigwa marufuku? Haya mengine kwa nini yanazuiliwa kwa nguvu kubwa?
 
Mshana wewe ni mtu mkubwa sana hichi ulichoandika sjui ulikuwa unajua effect zake upande wako maana humu tutakusifia tu na kukufanya uonekane shujaa but behind the scene kitachotokea hakuna mtu mwenye msaada humu zaidi ya pole za mdomo
kwani ameandika nini cha kuogopesha. kwanini mko hivyo lakini!?
 
Halafu maandamano siyo kosa la jinai! Vitisho ni vya nini tena!!

Mbona siku chache tu zilizopita Yanga na simba walifanya parade zao zilizoambatana na maandamano makubwa, na hatukuona yakipigwa marufuku? Haya mengine kwa nini yanazuiliwa kwa nguvu kubwa?
The guilty are afraid..!
 
Sasa mbona Tanganyika sio nchi tena WaTanganyika wanatoka wapi
Ndio nchi yetu ya asili kama ilivyo Zanzibar... Tanzania ni jina la makaratasi lisilo na uhalisia wala mizizi ya asili
 
Ya sabasaba yamepita bila watu wengi kuandamana kutokana na nguvu kubwa ya ulinzi iliyotumika kudhibiti maandamano
Siku ya 7/7 ilitawaliwa na ukimya wa kutisha
Barabara zilikuwa tupu
Biashara asilimia 99 zilikuwa zimefungwa
Watanganyika kwa asilimia 90 hawakutoka majumbani, kitu ambacho si kawaida kwa siku kama hiyo

Serikali pengine itaona aibu kutoa tathmini ya hasara iliyopata kwa hiyo siku moja tuu
Kuanzia maenesho ya miaka 50 ya 7/7 kudoda na kudorora vibaya sana, gharama kubwa iliyomika kuvileta barabarani vyombo vya ulinzi na usalama, posho, mafuta, vifaa, silaha, nknk..

Biashara zote ambazo zilifungwa serikali pia ilikosa mapato
Ukimya ule wa jana haukuwa utulivu wa amani bali ulikuwa utulivu uliojaa fukuto la chini
Hilo fukuto la chini kwa chini linaendelea kufukuta chini kwa chini na hili na hili ndio linatengeneza ratiba endelevu ya maandamano kwa kila tukio kubwa la kitaifa kwa siku zijazo

1. Maadhimisho ya 8/8
2. Ufunguzi wa AFCON
3. Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa 14. Oct
4. Maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya October 29
5. Maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka X-mas na Mwaka mpya!

Kuna madai ya wananchi wa Tanganyika.. Hayafanyiwi kazi yanaendelea kupuuzwa.. Yakiendelea kupuuzwa tena na tena hizi ratiba za maandamano hazitakoma
ANDIKO BORA SANA KWA MWAKA HUU. NI BORA KSBB NDIO UHALISIA NA LINAHUSU MAISHA YETU YOTE KWA WAKATI TULIONAO NA WOTE UJAO
 
1. Maadhimisho ya 8/8
2. Ufunguzi wa AFCON
3. Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa taifa 14. Oct
4. Maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya October 29
5. Maadhimisho ya sikukuu za mwisho wa mwaka X-mas na Mwaka mpya!
Naunga Mkono hiyo ratiba yaani hakuna kupoa ,MWAMWI....Kila Jumatatu na Alhamis - Maria Space kujumuika kwa wingi ,ni kuwapiga tu kiuchumi mpaka waombe pooo!!
 
Haya madai ambayo unataka yafanyiwe kazi ni yapi au umeamua tu kuhamasisha vurugu mitandaoni.
 
Back
Top Bottom