Rasmi Mchezo wa Simba Vs USGN ni saa 4:00 Usiku Aprili 3, 2022

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limeamua mchezo wa mwisho wa Hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika katika ya wenyeji Simba dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale (US Gendarmerie) kuwa utachezwa saa nne usiku.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezo wa soka ngazi ya labu kuchezwa muda huo katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

“Ili kutoa nafasi kwa mashabiki wetu wa aina zote kupata muda mzuri wa kuja uwanjani kushangilia timu yao, mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN utakuwa ni saa 4:00 usiku,” Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally.

Ahmed Ally ameongeza kuwa kuhusu suala la usalama kila kitu kipo vizuri na Jeshi la Polisi limeahidi kuwa litaongeza askari wa usalama kwa ajili ya mchezo huo.

Maamuzi ya kuupeleka mchezo huo muda huo ni kwa kuwa wanataka michezo yote ya Kundi D chezwe muda mmoja.

Mchezo mwingine wa kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambapo timu zote nne zina nafasi ya kusonga hatua ya Robo Fainali.
 
“Ili kutoa nafasi kwa mashabiki wetu wa aina zote kupata muda mzuri wa kuja uwanjani kushangilia timu yao, mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN utakuwa ni saa 4:00 usiku,” Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally

Inaendelea....
Watanzania Kwa ukanjanja!! Mmeshindwa kueleza sababu ya Mechi kubadilishwa Muda mnatuletea huu uongo iliopakwa mafuta? Mashabiki wa Tanzania wanapenda kuangalia Mechi uwanjani Hadi Saa 6 usiku? Jumapili ni siku ya mapumziko kuelekea siku ya kazi Jumatatu, kama ni hiari ya Timu kupanga Muda Kwa nini muwalaze mashabiki wenu saa usiku halafu SAA 11 waamke kujiandaa na kazi?
Kwani kuna ubaya gani kusema ukweli?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Mbona sababu kasema kuwa shirikisho linataka mechi zote za kundi D zichezwe muda mmoja? Nafikiri kuepusha swala la upangaji wa matokeo maana ndo michezo ya mwisho.
 
Sijapenda kabisa. Wamekosa hela yangu ya kwenda uwanjani
Utaenda kibanda umiza siyo mbaya! Au kama vipi utasikiliza kwenye radio.

Uzuri kibanda umiza siku hiyo kutakuwa na

Barcelona vs Sevilla 22:00
Intermilan vs Juventus 21:45
Simba vs USG 22:00
 
Watanzania Kwa ukanjanja!! Mmeshindwa kueleza sababu ya Mechi kubadilishwa Muda mnatuletea huu uongo iliopakwa mafuta? Mashabiki wa Tanzania wanapenda kuangalia Mechi uwanjani Hadi Saa 6 usiku? Jumapili ni siku ya mapumziko kuelekea siku ya kazi Jumatatu, kama ni hiari ya Timu kupanga Muda Kwa nini muwalaze mashabiki wenu saa usiku halafu SAA 11 waamke kujiandaa na kazi?
Kwani kuna ubaya gani kusema ukweli?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Nafikiri pia hata berkane na ases watacheza muda huo huo na siku hiyo hiyo

Hivyo wameona zote zichezwe muda sawa ili kuweza kuondoa mchezo wowote mchafu kufanyika nyuma ya pazia.
 
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limeamua mchezo wa mwisho wa Hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika katika ya wenyeji Simba dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale (US Gendarmerie) kuwa utachezwa saa nne usiku.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezo wa soka ngazi ya labu kuchezwa muda huo katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

“Ili kutoa nafasi kwa mashabiki wetu wa aina zote kupata muda mzuri wa kuja uwanjani kushangilia timu yao, mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN utakuwa ni saa 4:00 usiku,” Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally.

Ahmed Ally ameongeza kuwa kuhusu suala la usalama kila kitu kipo vizuri na Jeshi la Polisi limeahidi kuwa litaongeza askari wa usalama kwa ajili ya mchezo huo.

Maamuzi ya kuupeleka mchezo huo muda huo ni kwa kuwa wanataka michezo yote ya Kundi D chezwe muda mmoja.

Mchezo mwingine wa kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambapo timu zote nne zina nafasi ya kusonga hatua ya Robo Fainali.
Simba watasinzia uwanjani
 
Watanzania Kwa ukanjanja!! Mmeshindwa kueleza sababu ya Mechi kubadilishwa Muda mnatuletea huu uongo iliopakwa mafuta? Mashabiki wa Tanzania wanapenda kuangalia Mechi uwanjani Hadi Saa 6 usiku? Jumapili ni siku ya mapumziko kuelekea siku ya kazi Jumatatu, kama ni hiari ya Timu kupanga Muda Kwa nini muwalaze mashabiki wenu saa usiku halafu SAA 11 waamke kujiandaa na kazi?
Kwani kuna ubaya gani kusema ukweli?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
Watu Wana angalia Uefa saa 5 usiku mechi inaisha saa 7 na kesho yake Wana amkia mzigoni vizuri tu. Sasa saa 4 hiyo???
 
Back
Top Bottom