Rasilimali zetu!

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,782
Points
1,250

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,782 1,250
Robin Szolkowy alizaliwa 17 Julai 1979 huko Greifswald,Mecklenburg-Vorgommem, ujerumani. Yeye na patna wake Aljona Savchenko, ndio wanashikilia medali ya shaba ya dunia na mabingwa wa ulaya katika mchezo wa figure skating(pair). Mama yake,nesi alikutana na baba yake, daktari kutoka TANZANIA wakati baba yake anasoma Greifswald. Ingawa ana picha za baba yake hawajawahi kukutana nae. Ni wangapi kama hawa tumewapoteza huku ulaya? Obama ambaye wakenya wanajivunia, baba yake alimuacha wakati ana miaka miwili. Ni juhudi zake tu ndiyo zilimpeleka mpaka Kenya. Huyu kijana, ingawa hajawahi kumuona baba yake bado anajivunia damu ya utanzania ama sivyo angeukana kabisa.Mimi nadhani kwa upande mmoja, kuna haja ya kuwavuta watu kama hawa kwenye asili yao, ambayo ni Tanzania. Hapo mbeleni wanaweza kutusaidia kama sehemu ya Tanzania diaspora. Ni rasilimali yetu.
 

Forum statistics

Threads 1,364,878
Members 521,053
Posts 33,331,509
Top