Kuwajengea Ushirikiano na Diaspora ya Tanzania

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,775
6,588
Robin Szolkowy alizaliwa 17 Julai 1979 huko Greifswald, Mecklenburg-Vorpommern, Ujerumani. Yeye na patna wake Aljona Savchenko, ndio wanashikilia medali ya shaba ya dunia na mabingwa wa ulaya katika mchezo wa figure skating (pair).

Mama yake, Nesi, alikutana na baba yake, daktari kutoka Tanzania, wakati baba yake anasoma Greifswald. Ingawa ana picha za baba yake, hawajawahi kukutana nae. Ni wangapi kama hawa tumewapoteza huku Ulaya? Obama, ambaye Wakenya wanajivunia, baba yake alimuacha wakati ana miaka miwili. Ni juhudi zake tu ndiyo zilimpeleka mpaka Kenya.

Huyu kijana, ingawa hajawahi kumuona baba yake, bado anajivunia damu ya Utanzania, ama sivyo angeukana kabisa. Mimi nadhani kwa upande mmoja, kuna haja ya kuwavuta watu kama hawa kwenye asili yao, ambayo ni Tanzania. Hapo mbeleni wanaweza kutusaidia kama sehemu ya Tanzania diaspora. Ni rasilimali yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom