Rapper 50 cents akiri kurogwa

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,067
26,997
Ni kupitia wimbo wake "Many Men" ambapo rapper 50 cents anasema.

" In nightmare niggas keep pulling tecs on me .

Psychic says some bitch dumb PUT A HEX on me"

Akimaanisha " katika ndoto zangu za usiku nawaona watu bado wananishambulia Kwa risasi, Mganga akaniambia Kuna mpumbavu ameniroga"

To put a hex= kumroga MTU.

( To put a curse on a person. It can be any kind of a curse, eg a death curse,. Curse on their finances etc )

Hilo tukio obviously lilitokea baada ya 50 kutoka hospitali alikoenda kutibiwa baada ya kushambuliwa Kwa risasi na akiwa bado ana pambana ku recover akawa anaota ndoto za kutisha watu bado wanamuwinda wakammalize ( Na Ni Kweli jamaa walikuwa bado wanamuwinda)

Then 50 akaamua kwenda Kwa mtaalamu WA mambo ya kiroho/ mganga/ ( A Psychic) ili kujua what is going on in his life ndipo mganga AKAMWAMBIA Kuna mtu ame kuroga .. au Kwa maana nyingine Kuna mtu ameingia katika agano la kishetani kwenye Madhabahu ya kishetani ili wewe ufe..

Ni hivi alicho kisema 50 cents ni Kweli kabisa.

Nilipokuwa jambazi, anasema Calvin kijana ambae Kwa Sasa ameokoka huko nchini Nigeria, tulikuwa tukipewa Kazi ya kuua mtu ilikuwa lazima Kwanza tupitie Kwa mganga wa kienyeji.

Kazi ya mganga WA kienyeji ilikuwa ni;

1. Kumlaani muhanga kwa kutumia majina yote ya miungu wake

2. Kutazama nyota ya muhanga.

Calvin anaendelea kusema kwamba laana inayo fanyika kwa mganga ni kumtamkia mauti muhanga. Huwa haliwi Jambo la kitoto. Hufanyika ibada maalumu ya KICHAWI Kwa ajili ya kumtamkia mauti mhusika ibada ambayo huendana na sadaka ya damu Kwa miungu. Ibada hii mara nyingi hufanyikia makaburini Na Wanyama wanao tolewa sadaka huwa ni Wanyama wenye Rangi nyeusi( MANENO YANGU: NI KWELI KABISA KATIKA HABARI YA MAKAFARA, WANYAMA.WENYE RANGI NYEUSI HUTOLEWA KWA MAJINI/ MAPEPO WAOVU ILHALI SADAKA YA WANYAMA WENYE RANGI NYEUPE HUTOLEWA KWA MAJINI/ ROHO WEMA.. )

Ama Kwa habari ya kutazama nyota ya muhanga mganga hutaka kujua mambo yafuatayo.

1. Ni siku Gani nzuri kinyota katika kutekeleza shambulio husika Kwa muhanga mtarajiwa. Kwamba ili lengo la shambulio lifanikiwe ( Yani muhanga kuuwawa) tukio lifanywe siku Gani Na SAA ngapi?

So baada ya kusoma nyota ya muhanga mtarajiwa mganga atawaambia wahusika kwamba ili tukio lenu lifanikiwe ni lazima tukio lifanyike siku labda ya jumanne Kati ya SAA nane Na dakika Saba mchana na SAA nane Na dakika Kumi Na Saba mchana..

Mganga huwaambia Kwa kutazama nyota ya muhanga endapo mtaenda katika Muda ambao mganga hajawaelekeza basi kuweni Na uhakika kwamba kusudio lenu halitakamilika...

Pia mganga hutazama kinga ya mhusika . Mganga akiona mhusika ana kinga kubwa basi anaipiga Kwanza kinga ili kuiharibu. Kinga ya victim ikiwa kubwa victim anaweza kuoteshwa usiku kuhusu Jambo litakalo tokea na victim anaweza kuchukua hatua kama vile kwenda Kwa mganga wake ambae anaweza kuwamaliza KICHAWI wahusika kabla hamjatimiza lengo lenu.

Vile vile kama victim ana nyota kubwa Sana basi nyota yake lazima ishushwe Kwanza ndipo hufuata zoezi la kumtamkia maneno ya kumlaani kumtamkia mauti..

Calvin anaendelea kusema kwamba mganga hutazama pia ni siku Gani nzuri kinyota Kwa Sisi kufanya tukio bila kupata matatizo Na vyombo vya usalama so mganga anapo kuwa anatazama nyota ya victim hutueleza pia siku nzuri ya kufanya tukio ambayo tutafanya tukio Na kuondoka Salama na hatutokamatwa.


Ama Kwa habari ya uvamizi kwenye mabenki, mganga pia hutazama na kutuambia siku na SAA sahihi kinyota ya kwenda kufanya tukio Kwa mafanikio Na kuondoka bila kupata matatizo na vyombo vya dola.

Anamaliza Kwa kusema , ujambazi ni Madhabahu nzito Na Hatari sawa Na uchawi ndio maana watu wengi wakiingia kwenye ujambazi ni ngumu kutoka..

My take: Alie mroga 50 hakumroga ili 50 afe Kwa uchawi ila alimroga /alimlaani kumtamkia mauti Kisha akatuma watu waende kummaliza Kwa risasi..
 
Back
Top Bottom