Nakubaliana na wewe asilimia zote. Dr. Massau alikuwa mzalendo wa kweli. Aliacha kazi majuu (Texas) ili kuja kuhudumia nchi yake. Nakumbuka alikusanya vifaa vya hospitali vilivyokuwa havitumiki tena huko, huku kwetu vikiwa havijafika, akaja kuhudumia ndugu zake. Nilikuwapo aliponyanyaswa kwa kukataliwa msamaha wa kodi. alipigana hadi vikatoka, akaanza kutoa huduma kwa wanyonge ambao hawakuwa na uwezo wa kwenda India au Ujerumani. MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA HUKO ALIKOTANGULIA.