Ramesh Patel Mgombea Ubunge Ukonga Dar, akamatwa na Takukuru akitoa Rushwa Check Point Pugu

Hii ni nchi ya watanzania and not foreigner

Tumekuwa wapuuzi kiasi gan watanzania kuruhu hawa waharibifu kututawala

UZALENDO UPO WAP?????
 
Hii ni nchi ya watanzania and not foreigner

Tumekuwa wapuuzi kiasi gan watanzania kuruhusu hawa waharibifu kututawala

UZALENDO UPO WAP?????
 

Attachments

  • 1438069797441.jpg
    1438069797441.jpg
    12 KB · Views: 271
Wanamwonea tu Mbona Dr.Mwakyembe anamwaga pesa Kyela na TAKUKURU wanaogopa kumkamata.Taarifa tumepeleka mara tano lakini hakuna kitu
 
Kelele za mwanzoni tu hizo na hakuna kitachofanyika, kwani wangapi wamekamatwa na kuhojiwa tu kisha wanaendelea na shughuli za chama kama kawaida. Takuruku wenyewe vibogoyo

Ni TAKUKURU sio Takuruku.
 
Sakata la Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ukonga Ramesh Patel pamoja na Wapambe wake wa karibu Prof. Felician Barongo , Msafiri Mohamed DK, Na wengine wamekamatwa na Takukuru jana usiku katika ukumbi wa check point Pugu wakigawa rushwa kwa wajumbe wa mashina ili kuwahamaisha kumshangilia leo kwenye mkutano wa kuomba kura katika kata ya Pugu na hatimaye kumpigia kura za maoni 1/8/2015.


Ramesh na wapambe wake waliingia na magari mawili aina ya Nissan Extrail moja likimilikiwa na Prof. Barongo na lingine na Msafiri DK Magari haya ndio yanayoongozana na Ramesh toka Jumamosi kwenye kata za mzinga,kitunda,kivule na ukonga.
attachment.php

Baada ya Takukuru kuvamia magari hayo, na kumweka chini ya ulinzi msafiri DK na dereva aliyefahamika kwa jina la Dotto kina Barongo na wenzake walimtoa Ramesh mlango wa nyuma na kupakiwa bodaboda kuondoka eneo la tukio bila dereva wa bodaboda kujua amebeba mjumbe wa NEC na mtuhumiwa wa rushwa!


Afisa usalama mmoja nae alidandia bodaboda na kuanza kumfukuza. Baada ya mwendesha bodaboda kujua anakimbizwa aliingia kwenye njia isiyotoka na hapo Ndio Ramesh alipotiwa nguvuni.
attachment.php

Mdau wetu alifika eneo la tukio na kuongea na mashuhuda kuthibitisha tukio hilo. Pamoja nimekuwekea picha za nyumba hiyo iliyopo pugu kigogo fresh karibu na Check Point Pub.Ambapo alikuwa na gari aina ya NissAN X-trail yenye namba T671 BQL,na magari mengine ya wapambe aina ya Carina yenye namba T 183 CJQ na Nissan X-Trail T888 DED ambayo kwa pamoja yalitimua mbio baada ya Maafisa wa TAKUKURU kuwawekea mtego ambapo Ramesh alitoroka na boda boda na kamera yetu ilipofika alipokimbilia ramesh ilikuta hayupo.
attachment.php
 

Attachments

  • XTRAIL 671 BQL.jpg
    XTRAIL 671 BQL.jpg
    21.3 KB · Views: 399
  • NYUMBA.jpg
    NYUMBA.jpg
    12.7 KB · Views: 384
  • YA WAPAMBE.jpg
    YA WAPAMBE.jpg
    19.6 KB · Views: 381
Huyu akikatwa ataenda UKAWA
Watampokea na kusema tatizo ni mfumo!!
kwani unataka kutuaminisha kuwa mfumo wetu wa kiserikali hauna matatizo au ndo pressure ya kujiandaa kuachia nchi inakuongoza kutoa post zako? usipanic brother mwaka huu tunaagana rasmi tukutane ikulu
 
baadhi ya wanaccm bado wana mbinu chafu za kuwania madaraka...

maana wakitumia njia halali, watakuwa hawana vigezo!!
 
Dar es Salaam, Taarifa zilizotufikia zinaeleza kwamba mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga, CCM Ramesh Patel amekamatwa na Takukuru wakati akitoa rushwa katika eneo la check point Pugu.

Chanzo Habari5.com
 

Attachments

  • 10444551_957901654273829_2112203084326384248_n-1.jpeg
    10444551_957901654273829_2112203084326384248_n-1.jpeg
    10.6 KB · Views: 866
Mbona sioni rushwa yoyote...
zaid ya kuonekana kama wanabonga
na kanjubahi anatoa "fegi" mfukoni.

attachment.php
 
Back
Top Bottom