Uchaguzi 2020 TAKUKURU: Ubwabwa wa Hashim Rungwe kwenye kampeni ni Rushwa

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,302
24,143
Sasa ni rasmi, ubwabwa kutolewa wakati wa kampeni ni rushwa kwa wapiga kura.

TAKUKURU imetamka rasmi kuwa kuwapa watu ubwabwa, wale wanaovutwa kuja kwenye kampeni za Hashim Rungwe, ni moja ya rushwa ili kupata kura.

Wengi tumeandika mitandaoni kuwa huyu Rungwe anatuchukuliaje Watanzania?

Are we so cheap?
Ubwabwa wa Rungwe wapigwa marufuku

====

Wakati mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, akitarajia kuzindua kampeni yake leo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemwonya kuhusu ahadi yake ya kuwapa ubwabwa wananchi watakaokwenda kwenye mkutano wake

Huku taasisi hiyo ikisema kugawa chakula hicho ni kosa kisheria na ni rushwa, mgombea huyo amesisitiza kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi na kwamba ubwabwa utakuwapo.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Christopher Myava, alitoa onyo hilo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam.

Myava alisema Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 inapiga marufuku kwa mgombea kutoa vitu kama chakula kushawishi wapigakura ili wamchague.

"Kwa mujibu wa sheria, kutoa chakula ni kosa kwa sababu huo ni ushawishi kwa kuwapa chakula ili wakupigie kura. Kwa nini afanye haya katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani kuna shughuli ngapi ambazo zinafanyika? Mikutano mingapi ambayo inafanyika watu hawaweki ‘bufee’?" Alihoji.

Myava alisema kipindi hiki kinachotakiwa kufanywa na mgombea ni kunadi sera zake ili kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua na si kushawishi kwa kutoa rushwa.

"Unapotoa chakula kipindi hiki cha kampeni kabla hata hujachaguliwa, huo ni ushawishi kwa mujibu wa sheria hizi. Anachotakiwa kukifanya mgombea ni kunadi sera na si kushawishi watu kutokana na chakula anachokitoa," alisisitiza Myava.

Rungwe akizungumza juzi na gazeti hili alisema leo atazindua kampeni zake eneo la Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 alasiri na kuwaomba wananchi wahudhurie kwa wingi kwa sababu kutakuwa na ubwabwa ambao watagawiwa bure.

Rungwe amekuwa akilisisitiza suala la kutoa ubwabwa kwenye mikutano yake ya kampeni kiasi cha kuwavutia wananchi ambao wamekuwa wakitoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kusubiri mikutano yake ianze.

MSIMAMO WA RUNGWE

Rungwe alipoulizwa msimamo wake baada ya tamko hilo la TAKUKURU, alisema ubwabwa utakuwapo kama kawaida na kudai kuwa kufanya hivyo si rushwa.

"Hiyo siyo rushwa nitatoa ubwabwa kama kawaida kwenye mkutano. TAKUKURU wajiandae kupelekana mahakamani," alisema Rungwe alipohojiwa na Nipashe.

Rungwe ambaye amekuwa mgombea anayetoa burudani kutokana na matamko yake, juzi alitoa mpya baada ya kueleza kuwa kama wananchi watampa ridhaa kuwa Rais, miongoni mwa mambo atakayofanya ni pamoja na kuuza ndege na magari yote yanayotumiwa na viongozi waandamizi wa serikali wakiwamo mawaziri na wakuu wa mikoa.
 
Sasa ni rasmi, ubwabwa kutolewa wakati wa kampeni ni rushwa kwa wapiga kura.

TAKUKURU imetamka rasmi kuwa kuwala watu ubwabwa, wake wanaovutwa kuja kwenye kampeni ni moja ya rushwa ili kulata kura.

Wengi tumeandika miandaoni kuwa huyu Rungwe anatuchukuliaje Watanzania?

Are we so cheap?
Yani hadi rungwe anawekewa kauzibe? Duh.
 
Vipi kuhusu kofia na ma tshirt ya ccm. Watanzania tambueni sheria zote zinazotungwa huwa ni kwa maslahi ya ccm hivi sasa tshirt na kofia ni ruksa ikitokea Chadema wakapata tshirt za ukweli na za kijanja na kuzigawa bure gafla tshirt zitatungiwa sheria na kuwa ni rushwa kutolewa. Mungu ingilia kati.
 
Hata hivyo mimi ningeshauri wamuache tu maana hana madhara kihivyo....tuweke nguvu nyingi kwa kina kyadema na actors, sorry act haswa kwa kule upande wa pili wa nji.
 
Sasa ni rasmi, ubwabwa kutolewa wakati wa kampeni ni rushwa kwa wapiga kura.

TAKUKURU imetamka rasmi kuwa kuwala watu ubwabwa, wake wanaovutwa kuja kwenye kampeni ni moja ya rushwa ili kulata kura.

Wengi tumeandika miandaoni kuwa huyu Rungwe anatuchukuliaje Watanzania?

Are we so cheap?
Ubwabwa wa Rungwe wapigwa marufuku
Kwani kuna tofauti gani kati ya ubwabwa wa CCM na vikundi vya muziki vinavyotumiwa na CCM kuvuta watu....!!?
 
Vipi waneokwenda kwenye kampeni kwajili ya wasanii??

Nayo ni rushwa kwa sababu kikawaida tamasha la mziki mtu huwa unalipia. Na ukitaka kujua kama ni rushwa basi jiulize jee siku za kawaida zisizo za uchaguzi, CCM wanaweka matamasha ya bure? In fact hata bendi yao wenyewe, TOT inatosha kiingilio.
 
Wanachotufanyia sicho CHAUMA tunahimiza kwa vitendo sera zetu tunataka taifa la watu wenye nguvu na si vinginevyo.. hao takukuru wanatuonea tu wanachauma hii si haki.. kwanini watunyime haki yetu ya kula..? Au wanataka hapo ofisini kwao tuwapelekee sufuria za wali ndo waelewe!.. ile sio rushwa ni uhimizaji wa sera zetu wana CHAUMA..
 
Wakati TAKUKURU wakipiga marufuku ubwabwa wa CHAUMA imebainika kuwa CCM nao waliwahi kuzindua kampeni kwa wali mchuzi kule Igunga.

1599283363432.png
 
Yaana Takukuru wamefikia upeo wa kufikili kiasi hiki? Hadi wanataka kutumika na maccm kututia kwenye msitali.
 
Back
Top Bottom