Rambirambi za waliokufa wa shule ya Lucky Vincent, Arusha zadaiwa kuchezewa rafu

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,858
5,101
Habari ndio hiyo, Yale kagera yanaelekea kujirudia



RAMBI RAMBI YA WAFIWA "LUCKY VICENT SCHOOL".

Familia za Wanafunzi, Waalimu/Dereva zilizopoteza wapendwa wao kwenye ajali ya gari la shule ya Lucky Vincent huko Arusha zimepatiwa kila moja kiasi cha shilingi Milioni 3.6, (Pesa Zingine zilizotolewa zimetumika kugharamia gharama Zingine. Millions 60, 400,000) zipi?

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Arusha,jumla ya shilingi milioni 190 zimetumika kwenye gharama zote.

Kimahesabu jumla ya shilingi Milioni 129,600,000 ndizo walizopewa wafiwa kama Rambirambi baada ya matumizi mengine.Kiasi cha shilingi milioni 60,400,000 ndizo zilizotumika kwa matumizi mengineyo.

Swali langu moja tuu,
"Serikali ilitangaza itagharamia Mambo yoote ya Msiba mpaka kuzika, sasa hii ya kusema tena kiasi flani cha fedha ya Rambi rambi kilichotolewa kimetumika kwa mambo mengine ni yapi hayo? Ili kuondoa utata vichwani mwa wengi, ingependeza endapo yangetajwa.
 
IMG-20170512-WA0011.jpg


Nimeikuta mahali
 
Waliozitoa ndo wana kiherere! Walishindwa nini kuwapatia wafiwa?

Kwa nini hatujifunzi? Watanzania we have huge trust deficit especially kwenye financial issues.

Haya mambo eti ya kuchangia maafa au Mpira au sherehe kupitia serikalini...I will never do it!
 
Ni kwamba huyo mkuu wa mkoa hajui kuandika na hesabu hajui ata kidogo.
215-190=25m,,sasa iyo 25m ukigawa kwa familia 36 utapata Kama laki sita na elfu tisini kwa kila familia.
Na Kama ni iyo 190m ndio imetumika kugawa (rambirambi) kila familia ingepata 5.2m.
 
Back
Top Bottom