Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

inasaidiaje nyufa kwa maeneo yenye ardhi ya kupasuka (ardhi inachanika chanika kipindi cha jua)
Hiyo sasa inafanywa chini kabisa kabla ya kulaza tofali za msingi, linamwagwa zege (blinding) kuzunguka msingi wote ambalo linakuwa na nondo zinazosukwa kama nondo za jamvi (slab) ili kuzuia hiyo mipasuko ya chini isiathiri msingi
 
Hakikisha socket zako utakazofunga nyumbani kwako ziwe ni za namna hii, usitumie zile socket ambazo unaweza ukaingiza chaja/chocote bila kupachua hiyo lock ya juu. Hii ni kwa usalama hata wa watoto, kwani wanaweza wakaingiza kitu kwenye socket ambacho kinapitisha umeme ikawa ni hatari zaidi kwao.
20240228_230034.jpg
 
Baada ya kufunga na kumwaga mkanda wa juu, pandisha kozi tatu badala ya mbili kama wengi wanavyofanya. Kumbuka ule mlalo wa bati (overhang) utaificha kozi moja (au na zaidi) na hivyo itabaki kozi moja inayoonekana ambapo nyumba itaonekana kama imemezwa na paa. Ukiweka kozi 3, nyumba itapendeza zaidi na pia itafanya hata taa za nje zikae vizuri bila shida
Asante kwa elimu,natamani ningekufahamu mapema ungenisaidia sana
 
Mkuu
Kuna apartments zinatakiwa kuezekwa
Sasa Kuna fundi kanishauri ili kuokoa gharama pamoja na ubora niezekee bati ya Alaf nyeupe halafu nipake PVA ya plascon au kiboko...kuliko kuezeka bati nyingine ya rangi

Ushauri wako wa kitalaamu tafadhali
Tena izo bati nyeupe za alaf tumia G28. Ziko vzr mnoo.
 
Hiyo sasa inafanywa chini kabisa kabla ya kulaza tofali za msingi, linamwagwa zege (blinding) kuzunguka msingi wote ambalo linakuwa na nondo zinazosukwa kama nondo za jamvi (slab) ili kuzuia hiyo mipasuko ya chini isiathiri msingi
ili liwe imara izo nondo zinatakiwa ziwe ngapi pale chini
 
ili liwe imara izo nondo zinatakiwa ziwe ngapi pale chini
Mininum nondo 4 kwa zile ndefu ambapo utaziweka katika spacing ya 15cm or less kutegemeeana na upana wa msingi uliochimba (kawaida upana ni futi moja na nusu sawa na 45cm)

Na zile nondo fupi ambazo zinakatiza ktk nondo ndefu weka spacing ya futi moja moja sawa na 30cm, wengine huwa wanaongezea na BRC mesh au wire mesh za kawaida hizi za vyumba vyumba (2x2) zinazotumika madishani ili kuongezea uimara zaidi
 
Kama mlango wako wa grill ni double door, jitahidi mlango mmoja uwe na lock ya kuzuia mlango mwingine usifunguke mpaka ifunguliwe milango yote. Hii itakusaidia endapo mhalifu amefanikiwa kuvunja kufuli la mlango wa kwanza kutoweza kuingia na hivyo kumpa kazi nyingine ya ziada ambapo anaweza akasitisha zoezi lake la kuiba ukawa umesalimika.

Kwa upande wa zoezi la kujiokoa na hatari itakayotokea ndani (mfano moto) pia zoezi litakuwa gumu kama ilivyo kwa mwizi kuweza kuingia ndani
 
Mzigo unaobebwa na mkanda huwa unatawanywa sawa sawa kutokea katikati na kuupeleka pembeni, yaani mfano kama mkanda una mita 4 basi uzito uliobebwa na nusu ya huo mkanda (mita 2) unapelekwa kushoto, na uzito wa nusu iliyobaki unapelekwa kulia.

Katika makutano yoyote ya kuta, kunakuwa na mkusanyiko wa uzito kutokea kati kati ya hizo kuta zinazounda hiyo kona kwa hivyo ni muhimu sana kuweka nguzo katika kona ili kuongeza uimara zaidi kwa sababu ndipo mahali ambapo mzigo mkubwa unapokelewa ili kuupeleka ardhini (japo wakati mwingine mkusanyiko huo wa uzito unaweza ukabebwa na tofali tu bila shida yoyote lakini ukiweka nguzo inakuwa imara zaidi)
Bro,
Nje ya mada, naweza kufahamu wewe halisi ulivyo? Yaani hua nakusomaga mpaka Facebook uko kwa username ya jina hili hili, unatema madini sana.

Naweza kukukadiria kua ukiacha Ufundi-kipaji pia una Ufundi-elimu. Na hua unajibu very technical na in details kiasi cha kwamba unaelewa unachojibu.

Wewe ni aina ya watu ambao ki uhalisia walipaswa kua Walimu sababu hufundisha na kuelezea zile key points ambazo unajua mtu akizielewa hizo basi anakua ameelewa swala husika.

Wewe unaelezea kitu na technicalities zake, kwamba hata anaekusoma au kufundishwa na wewe anakua anaelewa haraka zaidi. Kuna vitu viko hivyo vilivyo sababu ya vitu vingine, vyote hivi wewe huelezea.

Maua yako chukua Mkuu, uko vizur sana kwenye kuelewa, na kuelewesha pia.
 
Katika ujenzi wa kuta, kitaalam inatakiwa usizidishe kozi 6 kwa siku ili kuruhusu kozi za chini zianze kukomaa kabla kozi za juu hazijajengwa juu yake
Kozi 4 mwisho stop, wait till next day ready constructed courses will hv gained maxi strength to bear on next loaded courses. From this point hakikisha una cure hizo kozi vizuri siku Saba na zaidi guys
 
Kozi 4 mwisho stop, wait till next day ready constructed courses will hv gained maxi strength to bear on next loaded courses. From this point hakikisha una cure hizo kozi vizuri siku Saba na zaidi guys
Bado 4 ipo katika range ya 1 mpaka 6. Katika ujenzi muda ni mali sana, ndio maana hata kwenye ujenzi wa maghorofa huwezi ukakuta watu wanasubiri zege ikae siku 28 ndipo waendelee na ujenzi kwa hatua inayofata.

Kwanza hakuna fundi utakayemuuzia kazi halafu umuambie ajenge sijui kozi 4 au kozi 3 kwa siku, fundi atatumia siku nyingi kumaliza kazi na mwisho wa siku itakuja kumkata yeye mwenyewe. Tuchukulie mfano hizo kozi 4 kama ndio wamemaliza kujenga saa saba mchana, ina maana mafundi wasimamishe kazi warudi tena kesho kuendelea na kazi?

Ila kama hela ipo, mnaweza mkakubaliana kwa hayo masharti na kazi ikafanyika tu bila shida. Pamoja na uharaka wa mafundi wa kumaliza kazi, lakini wao wenyewe pia wanaelewa kwamba ikishafika hatua flani huwezi kuendelea tena juu, utaona tu wanaanza kupumzika mmoja mmoja hata kama ni saa kumi jioni
 
Bro,
Nje ya mada, naweza kufahamu wewe halisi ulivyo? Yaani hua nakusomaga mpaka Facebook uko kwa username ya jina hili hili, unatema madini sana.

Naweza kukukadiria kua ukiacha Ufundi-kipaji pia una Ufundi-elimu. Na hua unajibu very technical na in details kiasi cha kwamba unaelewa unachojibu.

Wewe ni aina ya watu ambao ki uhalisia walipaswa kua Walimu sababu hufundisha na kuelezea zile key points ambazo unajua mtu akizielewa hizo basi anakua ameelewa swala husika.

Wewe unaelezea kitu na technicalities zake, kwamba hata anaekusoma au kufundishwa na wewe anakua anaelewa haraka zaidi. Kuna vitu viko hivyo vilivyo sababu ya vitu vingine, vyote hivi wewe huelezea.

Maua yako chukua Mkuu, uko vizur sana kwenye kuelewa, na kuelewesha pia.
Nashukuru sana ndg, mimi hicho kipaji cha kufundisha mtu mpaka akaelewa ninacho tangu muda. Ilikuwa mfano kama nimekosa kipindi, basi aliyehudhuria kipindi anakuja kunifundisha mimi halafu baada ya hapo ananiomba discussion ya hicho alichonifundisha ili aelewe zaidi. Tupo pamoja mkuu
 
Yaan mimi nyufa zangu zinaanzia juu kushuka chini

Hii ni nini shida yani kila mwezi nyufa tuuuView attachment 2924280View attachment 2924279
Naanza na hiyo nyufa ambayo haijapigwa plaster

Hiyo nyufa bila shaka ilitokea wakati wa umwagaji wa zege, ambapo sehemu hiyo, zege iliyowekwa ilikuwa na maji mengi kwa hivyo hiyo sehemu ya chini ambayo ilikuwa na maji mengi ikashuka chini na hiyo sehemu ya zege ambayo ilikuwa ina ukavu kiasi ikawa imebaki juu (slump). Hizi kitaalam tunaziita shrinkage cracks.

Katika uchanganyaji wa zege, maji yanatakiwa yasizidi kipimo kinachotakiwa ambacho ni nusu ya uzito wa kiasi cha cement kilichotumika, maji yakizidi yanafanya kokoto zizame chini na kufanya sehemu ya juu isiwe na kokoto kabisa au iwe na kokoto chache kwa sababu kokoto zina density kubwa kuliko maji. Hii kitaalam tunaita Segregation

Hicho kipande cha juu cha tofali kilichovunjika, kuna uwezekano mkubwa wakati wa kukata tofali kikawa kimepata nyufa hivyo fundi akaona uvivu kukata kingine akaamua kukiweka hivyo hivyo. Nyufa imeendelea kukua ikiwa hapo hapo baada ya kufyonza maji mengi. Nimeassume hivi kwa sababu juu ya hicho kipande hakuna mzigo wowote juu yake kusema labda imeshindwa kuhimili huo uzito

Kingine fundi alikosea kuweka hilo tofali juu ya uwazi, ilitakiwa liwekwe katika namna ambayo uzito wake utakuwa umebebwa na tofali mbili za chini na sio hivyo alivyoweka (hii pia inaweza kuwa sababu ya hiyo sehemu kupata ufa kwa sababu upande wa kushoto wa tofali unakosa balance (kama ratio ya udongo ingekuwa ndogo, nyufa inngekatikia hapo hapo kwenye maungio ya tofali na mortar)
 
Katika kuta za nje ni vizuri ukatumia white skim wall putty badala ya gympsum powder kama wengi wanavyofanya. Wall putty unatumia maji tu kuchanganyia, lakini white cement unatumia rangi kuchanganyia
Mafundi wa mtaani siku hizi wanatuambia tutumie cement ku-skim.
 
Moja ya aspects za building design ni pamoja na usalama, hakutakiwi nje kuwe na access yoyote ya kuingia ndani bila kuingilia mlangoni. Wezi mara nyingi wanaposhindwa kuingilia mlangoni, huwa wanatoboa dari la kwenye kibaraza na kutambaa juu kwa juu (kwenye dari) na kuingia ndani hivyo inashauriwa kuta za juu zinazozunguka kibaraza ziende mpaka juu kabisa kugusana na bati ili ikitokea mwizi ametoboa dari nje ashindwe kuingia ndani mpaka avunje ukuta

Ni ngumu kumzuia mwizi lakini inabidi utengeneze mazingira yatakayomfanya mwizi atumie muda mwingi zaidi kuweza kufanya tukio, hii itamfanya asitishe zoezi lake la kuiba kwa kuhofia kukamatwa

Kwa mahitaji ya ramani za kitaalam zinazozingatia aspects zote za usanifu majengo tuwasiliane
Duh!! Hii nimeipenda. Sasa kwa sisi ambao tulishamaliza nyumba na tunaishi inawezekana kupandisha tofali tukajenge huo ukuta wa hapo kibarazani?
 
Duh!! Hii nimeipenda. Sasa kwa sisi ambao tulishamaliza nyumba na tunaishi inawezekana kupandisha tofali tukajenge huo ukuta wa hapo kibarazani?
Hapo labda ufumue dari kwanza, upandishe hizo kozi halafu ndio urudishie. Jirani yetu mmoja aliibiwa kupitia njia hii, watu wamechana dari ya kwenye kibaraza wakatambaa juu kwa juu wakaiba vitu. Ilikuwa ni fremu za kupangisha, wezi wamepitia frem zote huko huko ndani kwa ndani
 
Back
Top Bottom