Rama dee (kinega) amaliza beef na Ruge

Hako nako kajinga tuu Clouds hawajamfanyia ubaya wowote ule ...kupewa hela unayo ona ndogo isiwe sababu ya kwenda kuwatukana watu wakati unayo nafasi ya kuikataa au kuikubali au kuongea nao wakuongeze...
Ungeangalia pande zote mbili maana Ruby alihojiwa kama ungesikia alichozungumza ndio ungejua kama hawa jamaa KILAULI mabwege sana wanataka kila msanii awatetemekee wao that's stupid at all and really unacceptable in the media.
 
Ule msemo wa Wahenga kuwa ‘wagombanao ndio wapatanao’ umedhihirika tena leo baada ya mkali wa RnB, Rama Dee kumalizana rasmi na kituo cha redio cha Clouds Fm ikiwa ni miaka kadhaa tangu ashiriki harakati za Anti-Virus dhidi ya kituo hicho.


Rama Dee ambaye alikuwa kwenye XXL ya Clouds Fm kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya ‘Nibebe’ alieleza kuwa alishiriki kwenye kanda mseto za Anti-Virus kwa sababu na ameamua kurudi nyuma na kupatana na kituo hicho kwa sababu bora zaidi.

“Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wanaonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa pamoja. Kwahiyo, kwa chochote ambacho kiliwahi kutokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana sio sahihi, naweza kusema ‘I’m sorry’ kwa Clouds Fm wenyewe,” alifunguka.

“Na kama [Clouds Fm] wanaona kuna sehemu walinikosea tayari tumeshazungumza nao na tumeshamaliza,” ameongeza.
 
hivi kweli kushindana na Clouds haiwezekani?

maana yake hawa jamaa wote wanarudi kuomba msamaha.
ndio tatizo la kifanya vitu kwa kufuata mkumbo kama una njaa bora usiwe mwanaharakati halaf mwenzao sugu aliwachukua yeye akenda bungeni baadaye kazunguka akapatana na Ruge naona kila mtu anarud mdogo mdogo sasa
 
Rama dee atajuta kujishusha akumbuke mapacha walichofanyiwa nyimbo ilipigwa mara moja ikapigwa chini

Sent from my GT-S7562 using JamiiForums mobile app
Swala hapa sio kutopiwa nyimbo au kupigiwa nyimbo nincho amini hapa kikubwa ni kutafuta amani na watu kwakuwa hakuna anayejua kesho yake na hiki alichokifanya ndicho tunatakiwa kufanya kwenye maisha yetu maana hakuna kitu kizuri kama kuwa na amni na kujua kuwa huna shida na watu na una amani yani hata ukipumzika kesho unakuwa huna deni.

Nampongeza sana.....
 
Rama D amesema yy nimfanya biashara kwaio lazma aguse pande zote za media kuserch for market which z truu.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Sugu dhambi ya usaliti haitomuacha salama....Aliwatia wenzake kwenye ugomvi kwa maslahi yake binafsi
 
Sugu dhambi ya usaliti haitomuacha salama....Aliwatia wenzake kwenye ugomvi kwa maslahi yake binafsi


Ukishakuwa mtu mzima, tena mwanaume ukikubali kushikwa masikio basi we lofa. Huwezi kumlaumu SUGU, kwasababu bifu lake na Clouds FM ni la kitambo sana kabla ya Vinega. Hawa wote walidandia gari kwa mbele wenyewe tu hakuwalazimisha
 
Dozen ni kama alikua anamlazimisha jamaa aombe msamaha on air..

Sent from my itel_it1503 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom