Rama dee (kinega) amaliza beef na Ruge

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,970
2,184
Baada ya beef na mvutano wa muda mrefu baina ya Ruge (clouds media) na msanii Rama dee sasa wameamua kuzika tofauti zao

Itakumbukwa Rama dee ni miomgoni mwa wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya ant virus kuidiss clouds na kujiita vinega yaani wanaharakati, lakini mpaka sasa
yamekwisha, wamesahau yote na muda huu kinega yupo live XXL na b12, mchomvu na wengineo wanareview mziki wa album wake na story zote zilizowahi tokea kipindi iko


Hongera Ruge kwa kukubali kusamehe na kuendelea kusonga mbele licha ya matusi na mabango mengi waliyokumwagia vinega!
Hongera pia kwako Rama dee, umethubutu.


Hii itakua somo kwa wasanii kama akina Ruby, muziki si bifu!
 
Unapokua unanyonywa na mnyonyaji hataki kuacha kufanya hivo,je unatakiwa ufanyaje?

Sent from my HTC One using JamiiForums mobile app
 
Ati?
Ila Clouds Media kwa kutengeneza watu mbadala hawajambo...
Alivyoondoka Gardener Habash bado nikawa naisikia sauti ya jamaa kwenye matangazo yao hasa ya kuinadi FM ACADEMIA (Ile sauti sijui ya jamaa gani...alitembea mulemule)
Baada ya Ray C kukabwa na unga kooni,Recho na 'Upepo' wake uka-cover nafasi ya mtoto wa Chalamila..
Ruby nae akasusia pilau,kisa halina kachumbari,kutahamaki, kigoli Nandi akalila pilau lote.....
Sijasikia tu mbadala wa Komando Jide...
Shubaaamit!
 
Unapokua unanyonywa na mnyonyaji hataki kuacha kufanya hivo,je unatakiwa ufanyaje?

Sent from my HTC One using JamiiForums mobile app
Ndio ivyo mkuu, jamaa kashaomba msamaha kabisa
 
hao wote waliingizwa mkenge na sugu, mwenzao akamalizana na clouds wakabaki wenyewe hawaelewi pa kuanzia, gud for him
 
Safi sana kwa hili nampongeza sana Rama dee maana hakuna kitu kizuri kama kutafuta amani na watu huwapo duniani..
Lazima tujifunze kusamehe na kusameheana maana hatutoishi milele...
Rama dee ameonesha ukomakuvu na huu ndio utu uzima na hapa si swala la biashara bali ni swala lakuwa na amani na watu wote..
Nategemea ipo siku Lady Jaydee atahamua kusamehe kama wenzie
Mara nyingine utoto husababisha watu kugombana hata kwa sababu za kijinga.....
Lazima tukubali kila media ina umuhimu wake ni vyema wasanii wakajaribu kutafuta amani

Hongera Rama dee na Ruge
 
Back
Top Bottom