Ruge amzungumzia Jaydee, Ruby, Rama Dee, Diamond, THT, Fiesta na Muziki wa Bongo Fleva ndani ya XXL


Jiraniyetu

Jiraniyetu

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Messages
351
Likes
332
Points
80
Age
23
Jiraniyetu

Jiraniyetu

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2016
351 332 80
Ruge Mutahaba ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group. Leo ameongea kwenye kipindi cha Radio Clouds cha XXL.

Tujuzane kinachoendelea hapo mjengoni. Sijui anataka kukamatia fursa ya nani mkali?

Karibuni..

=======
15135867_1255688217807927_2657390153682110326_n-jpg.439420


UNAUZUNGUMZIAJE MWELEKEO WA MUZIKI WA BONGO FLEVA?

Katika Africa kwa sasa [HASHTAG]#BongoFleva[/HASHTAG] inakwenda kulikamata soko la nje kutokana na vionjo tunavyovitengeneza. Tumetoka mbali sana na huu mziki lazima tuwasifie waanzilishi wa Bongo Fleva kama @sebamaganga, Kibacha, na Sugu.

KIBIASHARA JE?

Uzuri wa Bongo Fleva ni mchanganyiko wa vionjo vya mziki wa aina mbalimbali kiufupi mimi nasema kuwa hapa ni Ubunifu.

Kitu nilichofanya mimi ni kufanya mziki huu uwe biashara, hakuna jambo lisilokuwa na Manung'uniko mwanzoni. Chukulia mfano wa shamba anayewaza kulima shamba unakutana na Magugu lakini shamba lazima lilimwe.

Mimi ni msimamizi wa kituo lakini kwenye kituo kuna mifumo Mfano mimi huwa sihusiki na Fiesta lakini lawama zote ni kwangu. Siku zote naamini kwenye kipaji na uwezo aliokuwa nao mtu katika kazi, Diamond alipigwa chini THT lakini hakukata tamaa.

VIPI KUHUSU SUALA LA TEAM?

Ishu ya Timu kwenye muziki zilikuwepo kitambo tatizo linakuja pale kwenye athari za Uteam tuliokuwa nao. Nautaka Uteam utakaoleta athari kibiashara zenye kuleta faida, suala ni kwamba unasaidiaje kile unachokipenda.

Tulichofeli kujenga ni Team Tanzania linapokuja suala International tuangalie thamani yetu kama nchi tupo wapi. Ishu ya kuwa na Team mimi nasupport kabisa lakini ziwe kwenye tija kibiashara zaidi" - Ruge Mutahaba.

KASHFA YA UNYONYAJI WA WASANII?

Neno unyonyaji halipo tangu nchi yetu ilipopata uhuru. THT pale ni chuo cha muziki na Ruby alipita pale kama Mwanafunzi.

Tusichanganye professionalism na mambo binafsi, nafasi ya @iamrubyafrica kwenda [HASHTAG]#CokeStudioAfrica[/HASHTAG] tulimuombea sisi kama [HASHTAG]#THT[/HASHTAG].

Nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria kama una jambo lako kwanini usiende mahakamani kushtaki!?

Kwa mfano sisi hatupigi nyimbo za [HASHTAG]#RamaDee[/HASHTAG] napenda sana nyimbo zake ila ni kanuni za kazi zipo hivyo tusiishi kiunafiki.

Zaidi aliyoyasema Ruge ni....

"Bongo Fleva katika Afrika inaelekea mahali pa 'kutake over' ni muziki ambao unakuja kukamata kuwa ndio muziki wa Afrika, kama kipindi kile tulipokuwa tunasikiliza Mayenu, Bolingo kama tutaendeleza ile bidii yetu ya kuchukua vionjo mbalimbali kama tulivyoweza kuchukua ladha tofauti na kuchanganya na muziki wetu tutengeneze muziki wenye tija kwa Watanzania" RUGE MUTAHABA, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa louds Media Group

Kitu nilichofanya mimi ni kufanya mziki huu uwe biashara, hakuna jambo lisilokuwa na Manung'uniko mwanzoni. Chukulia mfano wa shamba anayewaza kulima shamba unakutana na Magugu lakini shamba lazima lilimwe. Mimi ni msimamizi wa kituo lakini kwenye kituo kuna mifumo Mfano mimi huwa sihusiki na Fiesta lakini lawama zote ni kwangu. Siku zote naamini kwenye kipaji na uwezo aliokuwa nao mtu katika kazi, Diamond alipigwa chini THT lakini hakukata tamaa.

Ishu ya Timu kwenye muziki zilikuwepo kitambo tatizo linakuja pale kwenye athari za Uteam tuliokuwa nao. Nautaka Uteam utakaoleta athari kibiashara zenye kuleta faida, suala ni kwamba unasaidiaje kile unachokipenda. Tulichofeli kujenga ni Team Tanzania linapokuja suala International tuangalie thamani yetu kama nchi tupo wapi. Ishu ya kuwa na Team mimi nasupport kabisa lakini ziwe kwenye tija kibiashara zaidi

"THT ni chuo haijawahi kuwa lebo, kwangu Ruby ni mtu ambaye amekuja kujifunza alikopita ameshinda Supa Nyota,amepata nafasi ya kuja pale kupata blasha kusaidiwa kurekodi, kama mlikuwa hamfahamu mimi ndiye niliandika mashairi ya wimbo wa Yule na Forever nikisaidiana na Barnaba, akijihisi yuko tayari kwamba yuko tayari haitaji dili zetu ndogondogo za hapa basi anaweza kuondoka, kuna watanzania wanapenda bifu, mtu akiwa na Uhuru wa kwenda mahali anaweza kwenda, sina tofauti yoyote na Ruby, alichokosea ni kuisemea maneno mabaya Taasis na Fiesta, lakini mimi binafsi niko tayari kufanya naye kazi" RUGE MUTAHABA

Diamond anaperfume yake ya Chibu Perfume hata akishuka kwenye muziki itamsaidia kuendesha maisha yake, mashabiki tushiwashabikie tu wasanii wetu kwenye mitandao tuwashauri wasiwe wanalewa lewa ovyo,wanatumia madawa mwisho wa siku wakianguka lawama zinakuja kwetu, kiukweli sina msanii ninayemmeneji kila msanii ni wangu anayekuwa kuniomba ushauri nampa, Diamond sio msanii wangu"
 
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
2,161
Likes
1,011
Points
280
MKATA KIU

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
2,161 1,011 280
ruge kaitengeneza bifu ili apige hela.....

haya sasa mashabik mjiandae kwa shindano kati ya team wcb vs team kiba na dimpoz
 
Raynavero

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Messages
34,627
Likes
43,101
Points
280
Raynavero

Raynavero

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2014
34,627 43,101 280
sielewi elewi hebu tuelezeeni ilivyo
 
warumi

warumi

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Messages
14,212
Likes
6,653
Points
280
warumi

warumi

JF-Expert Member
Joined May 6, 2013
14,212 6,653 280
Akizunguza kupitia kipindi cha XXL manager wa clouds fm ametamka wazi kuwa hana bifu na lady jaydee washamalizana mahakamani na yupo tayari kuonana naee akitaka, pia alizungimzia kuhusu kutopigwa nyimbo za lady jayee ambapo alisema alipewa amri na mwanamuzili hiyo kutopigiwa nyimbo zake wala jina lake kutajwa kwenye kituo hiko.
 
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Messages
13,162
Likes
6,663
Points
280
Age
29
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2011
13,162 6,663 280
dada wa watu anatia huruma sana
 
brave one

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
4,331
Likes
5,470
Points
280
brave one

brave one

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
4,331 5,470 280
Mkurugenzi wa clouds fm amesema hata tatizo na lady jaydee pamoja na kushinda kesi dhidi yake.
Amefafanua kuwa hawapigi nyimbo za jaydee kwasababu alitoa order ya nyimbo zake na jina lake visitajwe wala kupigwa kwenye kituo chao cha radio
Ameongeza pia hata wakikutana na jaydee hana tatizo nae na watapiga story na akitoa au kufuta order yake basi watapiga nyimbo zake hawana tatizo.
1480077646013-jpg.439413
 
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Messages
16,320
Likes
15,672
Points
280
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2014
16,320 15,672 280
Ruge

Kuna wasanii clouds imefungia nyimbo zao lakini mm binafsi nazipenda na nasiskiliza kila siku, napenda nyimbo za Rama Dee-Ruge xxl

-Ruge "Mim ndio nimeandika nyimbo za Rubby pia "Na Yule" niliandika na Barnaba "sijutii na forever" zote hizo

Boss Ruge ni jamaa kichwa sana

Amesema hana utofauti na Lady Jay Dee amesemaa anasubiri apewe ruhusa na Jide aanze kupiga nyimbo zake

Yupo tayari kukutana J Dee
 
B

babeney

Member
Joined
Oct 29, 2016
Messages
9
Likes
5
Points
5
Age
48
B

babeney

Member
Joined Oct 29, 2016
9 5 5
hongera sana kaka ruge kwaulicho kiamua wewe ni mfano wakuigwa pia hatamungu anapendahivyo kaka mungu andelekuku bariki nakukuongoza ktk imani hiyo amina
 
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
7,891
Likes
7,642
Points
280
Age
30
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
7,891 7,642 280
Ruge

Kuna wasanii clouds imefungia nyimbo zao lakini mm binafsi nazipenda na nasiskiliza kila siku, napenda nyimbo za Rama Dee-Ruge xxl

-Ruge "Mim ndio nimeandika nyimbo za Rubby pia "Na Yule" niliandika na Barnaba "sijutii na forever" zote hizo

Boss Ruge ni jamaa kichwa sana

Amesema hana utofauti na Lady Jay Dee amesemaa anasubiri apewe ruhusa na Jide aanze kupiga nyimbo zake

Yupo tayari kukutana J Dee
Jamaa anajua sana ukimsikiliza unaona kuwa yuko well informed na leo kawa so open.
 
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
7,891
Likes
7,642
Points
280
Age
30
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
7,891 7,642 280
yah ni mtu mmoja makini sana nimefatilia sana interview zake katika maneno kumi anayoongea lazima upate kitu
Sure man...
Inaelekea clouds fm wafanyakazi wake wanaenjoy kazi yao na wanapata opportunities nyingi.
 

Forum statistics

Threads 1,273,108
Members 490,297
Posts 30,471,653