Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 782
- 1,831
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametilia shaka tena uadilifu wa upinzani nchini humo, akikishutumu chama cha upinzani cha National Unity Party – NUP kwa kuhusika na vitendo vya udanganyifu kwenye uchaguzi. Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, alidai kwamba Jukwaa la NUP liliongeza idadi ya kura walizopata katika chaguzi zilizopita na kuwatuhumu viongozi wa upinzani kwa "kudanganya" badala ya kutoa njia halisi mbadala za kisiasa.
Pia alipuuza malalamiko ya uchaguzi wa upinzani akisema "hayana msingi". Kiongozi wa NUP Bobi Wine amepinga matokeo hayo, akidai kuwepo kwa ulaghai ulioenea, kufungwa kwa intaneti, na kutekwa nyara kwa mawakala wa vituo vya kupigia kura. Wine kwa sasa yuko mafichoni, kufuatia vitisho vya kumuua kutoka kwa Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Museveni na mkuu wa jeshi la nchi hiyo
Chanzo : DW SWAHILI