Raisi akiulizwa swali lolote la kesi iliyoko mahakamani akatae kujibu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,907
Tanzania kuna mihimili mitatu inayojitegemea na isiyoingiliana ambayo ni bunge na serikali na mahakama

Raisi akiulizwa chochote kilicho mahakamani akatae kujibu kuwa siwezi jibu swala lililoko mikononi mwa mhimili wa mahakama. hana haja Hata ya ku comment chochote aseme tu no comment Hilo liko mahakamani
 
Unahakika haiingiliani🤔?vinginevyo Anza kwa ufafanuzi ni kwa jinsi Gani haiingiliani.
 
Ni ushauri mzuri,bila shaka washauri wake watamsihi.
 
Maswali kama hayo ndio kipimo cha kiti cha Rais, cheo cha Rais kinahitaji mtu mwenye brain proven brain , uelewa mpana wa mambo mengi hata nje ya fani yake. Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kuamua na kuamua ni matokeo ya kufikiri na kufikiri kunahuisha uhai wa akili.
 
Katiba ambayo haikatazi vyama vya siasa kufanya mikutano lakini rais anao uwezo wa kukataza na asiulizwe? Au katiba ipi?
Vyama vya siasa hufanya mikutano sasa hivi Chadema digital inafanya mikutano nchi nzima kusajili Wana chama na ripoti wanaleta kila wakati humu jamiiforums forums kuwa wako wapi
 
Na ndio Maana Zito Kabwe alimuuliza lile swali kupima uwezo wake kwa makusudi kabisa wakati Zitto anajua kesi iko mahakamani akamtegeshea Kwa makusudi na Raisi akaingia kichwa kichwa
Anyway washauri wa Raisi kazi wanayo
 
 
Hongera kwa comment bora mno. Akili kubwa hii. Naikopi kwa matumizi yangu japo nitaedit kidogo.
 
Asilimia 90 ya viongozi waliopo katika mhimili wa mahakama wameteuliwa na raisi sasa kwanini asiingilie? Hakuna mhimili unaojitegemea hapo

Katiba mpya
Jiwe alisemaga Kuna mhimili uliojichimbia chini zaidi kuliko mwingine eti kiss mhimili ambao yeye alikua ni mkuu ndio ulikua anatoa pesa kwa Ile mihimili mingine
 
Na ndio Maana Zito Kabwe alimuuliza lile swali kupima uwezo wake kwa makusudi kabisa wakati Zitto anajua kesi iko mahakamani akamtegeshea Kwa makusudi na Raisi akaingia kichwa kichwa
Anyway washauri wa Raisi kazi wanayo
Kuna kitu kimesemwa pia kuhusu Heshima, umesahau au umejisahaulisha Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…