Siku Rais Paul kagame alipokoswakoswa kupelekwa ICTR kujibu kesi ya Mauji ya Kimbali

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,892
22,649
WINGU la mashaka juu ya mustakabali wa utawala wa Kagame nchini Rwanda ,lilianza kutanda muda mfupi tu baada ya maadhimisho ya 12 ya mauaji hayo ya Kimbari ,pale Mwanasheria wa ICTR alipotangaza kwamba Kagame alitakiwa kudhihirishwa kwa matendo yake wakati wa mauaji ya Kimbari.

Mwanasheria huyo wa Marekani, Paul Erlinder ,alisema kwamba kuna ushahidi kutokana na kinachosemwa na mashahidi katika Mahakama hiyo ya mjini Arusha, Tanzania, kwamba Kagame alihusika kwa sehemu kubwa na muhimu katika matukio yaliyosababisha mauaji hayo.

Shitaka lingine lililomkabili ni kwamba alishindwa kuchukua hatua za kuzuia machafuko ; pia akaamuru kunyongwa raia katika maeneo yaliyokuwa yakishikiriwa na waasi wa RPF wakati huo, Meya wa Gikoro Paul Bisengimina ,alihukumiwa miaka 11 jela kwa kuua takribani watutsi 1,000 waliokimbilia hifadhi Kanisani. Hukumu hiyo ilitolewa Aprili 13 mwaka 2006.

Aprili mwaka 2006 Erlinder alionyesha ushahidi wa waasi wa RPF kuamrishwa na Rais kagame kupiga makombora mawili yaliyoangusha ndege iliyomchukua Habyarimana, Alipokufa tu ukawa ndio mwanzo wa mauaji ya kimbari.

Kuna madai kwamba kufuatia urafiki wa muda mrefu na Marekani Rais kagame alikuwa Shwari juu ya tuhuma hizi, lakini sasa adui zake wafaransa walitia chumvi katika kidonda kilichoanza kupona. Rais wa zamani wa Liberia ,Charles Taylor ,aliwahi kusema adui wako akiwa anapokuwa bosi wako umekwisha!

Kagame aliungana na Rais wa Uganda ,Yoweri Museveni katika vikosi vya National Resistance Army ( NRA) mwaka 1979 ; na akatumia miaka kadhaa kupigana msituni. Alifanywa mkuu wa mashushushu wa NRA mwaka 1986 ; na alitazamiwa kama rafiki wa karibu wa Museveni ,baadae kagame na rafiki zake ,Fred Rwigyema wakaanzisha RPF iliyokuwa na askari wa kinyarwanda waliokuwa wakipigana katika jeshi la Museveni la NRA Wakati Museveni akiwa katika harakati za kuipindua Serikali ya Uganda.

OKTOBA mwaka 1990 RPF waliishambulia Rwanda kwa mara ya kwanza ,wakitokea Uganda, yeye kagame alikuwa Marekani ambako alikuwa akichukua mafunzo ya kijeshi ,baada ya Fred Rwigyema kufa siku ya pili ya mapigano ,kagame akawa Kamanda wa RPF.

Julai mwaka 1994 kagame akawa makamu wa Rais na Mkuu wa majeshi ya ulinzi ; akamwachia Pasteur Bizimungu ( Mhutu)Urais.
Bizimungu alijiunga na RPF tangu akiwa Uganda, alijiondoa katika Serikali ya Juvenal Habyarimana . kagame hakutaka kukwea Kwenye kiti cha urais hadi Aprili mwaka 2000 ,Wakati Bizimungu alipojiuzulu ,kufuatia kuhitilafiana serikalini.

Bizimungu aliwalaumu rafiki zake hao ,baadaye akajikuta kufungwa jela kwa madai kwamba alishiriki shughuli za kisiasa kinyume na sheria, kwamba hali hiyo ilikuwa ikitishia usalama wa nchi. Kagame na rafiki yake Museveni waliivamia jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, julai 2002 waliondoka majeshi mashariki mwa Kongo.

Baada ya kukosana na Museveni majeshi yao yalipigana Kisangani mwaka 1999 na 2000. Hata hivyo bado walikuwa wakiwaunga mkono waasi wa Kongo, kagame ameoa ana watoto wanne anapendelea kucheza Tennis na pia kujisomea.

Sakata la kagame lilikuja baada ya Ufaransa kuingia katika vita vikali juu ya nani alimuua Rais wa Rwanda hayati Habyarimana Aprili 6 mwaka 1994. Ufaransa Ilidaiwa kuwa Paul kagame ,wakati huo akiwa kiongozi wa waasi wa kitutsi wa Rwandese Patriotic Front RPF aliamrisha ndege iliyomchukua Rais Habyarimana itunguliwe kwa Kombora.

Ndege hiyo pia ilikuwa imemchukua Rais wa Burundi ,Cyprien Ntaryamira, ilianguka katika kasri la Rais mjini Kigali : na huo ukawa ndio mwanzo wa mauaji makubwa yanayokadiriwa kuchukua roho za watu kati ya 800,000 na 900,000. Meja Paul kagame aliwatuhumu wafaransa waliokuwa na uhusiano na serikali ya Habyarimana, kuwa ndio chanzo cha mauaji hayo yaliyolenga kuwafyeka watutsi na wahutu wenye msimamo mkali wa wastani.

Inadaiwa kuwa Wafaransa pengine baada ya kumtumia Habyarimana na kuanza kumchoka, ndio waliotungua ndege hiyo, inadaiwa pia kuwa eneo ndege hiyo ilipoangukia, lilikuwa likidhibitiwa na vikosi vitiifu kwa Rais Juvenal Habyarimana, sasa swali likaja iweje watutsi wamuue?

Wapo wengine walidai wakoloni wa zamani wa nchi hiyo ,Ubelgiji, walihusika na mauaji hayo ya kwanza ya aina yake Afrika. Baadhi ya raia wa Rwanda walianza maandamano mwaka huo 2006 mjini Kigali, kupinga kauli ya mpelelezi wa mauaji hayo ,jaji wa kifaransa ,Jean Louis Bruguiere ,kwamba Rais Paul kagame na wenzake walihusika kutungua ndege hiyo, na ukawa ndio mwanzo wa mauaji ya kimbari.

Na kwamba alitakiwa kushtakiwa kama mhalifu wa kivita katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya mauaji ya Rwanda (ICTR) iliyoko mjini Arusha. Jaji Bruguiere, alisema hata wasaidizi wake tisa wa kagame ,wakiwemo majenerali wakuu wa Rwanda ,na Mkuu wa majeshi ,James kabarege , na Mnadhimu mkuu, Charles Kayonga ,walitakiwa kutiwa mbaroni ili kujibu mashtaka hayo ya mauaji ya kuangamiza anga lote la Afrika.

Jaji Bruguiere ,alitazamiwa kusaini hati ya kimataifa inayoruhusu wanajeshi hao tisa kukamatwa siku chache tu zilizofuatia ,lakini Rais kagame kwa kuwa anayokinga ya Mkuu wa nchi, hati hiyo haikuweza kutolewa kumkamata yeye, Kulingana na sheria za Ufaransa.

Kulingana na maofisa wa Mahakama ya Ufaransa ,waliosema bila kutaka majina yao yatajwe , walisema watu walioko karibu na kagame walisema aliamuru waasi wa RPF kuidungua ndege hiyo.

Rais kagame alikanusha vikali madai hayo ya Ufaransa . Novemba 22 mwaka 2006, wakati akiwahutubia wageni 300, wakiwemo wafadhili wa kigeni waliokuwa wakihudhuria mkutano wa mwaka wa maendeleo mjini Kigali, alisema; Majaji wa Ufaransa hawana mamlaka ya juu kuwazidi majaji wa Rwanda.

Kauli ya kulaani wafaransa Ilikuja siku moja tu baada ya kauli ya jaji Bruguiere ,kwamba kagame ndiye chanzo cha mauaji ya kimbari ya Rwanda, na kwamba anatakiwa kujibu mashtaka. Ndege hiyo ilipigwa na Kombora ilipokuwa inakwenda kutua mjini Kigali ,Ilikuwa baada ya mkutano jijini Dar es salaam na huo ndio ukawa mwanzo wa mauaji ya siku 100.

Kulingana na shirika la habari la Reuters na Shirika la Uingereza la BBC ,Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda ,Charles Muligande ,alisema kwamba; Ufaransa ilikuwa inajaribu kufukia kile ilichokifanya mwaka 1994, wakati watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani walipouliwa.

Kwamba sasa ufaransa ilikuwa inataka kumtoa kafara kagame na maofisa wake ,kuhusiana na mauaji hayo. Kagame alishawahi kusema " Majaji wengine wa Ufaransa ambao hata majina yao siwezi kuyatamka wana cha kusema kuhusu upelelezi dhidi ya Rais na maofisa wa Serikali ? Huu ni upuuzi " alisema Meja Paul kagame.

Kwa kuwa sheria za Ufaransa hazitoi upenyo wa kagame kushitakiwa kwa sababu ya kinga aliyonayo ya Mkuu wa nchi, Bruguiere alidaiwa kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ,Kofi Annan ,kuomba kagame ayakabili mashtaka ya uhalifu wa kivita katika Mahakama ya Arusha, ICTR.

Waendesha mashtaka wa Ufaransa walishapewa maelekezo ya kuanza mara moja Utaratibu wa kumfikisha kagame mahakamani kama mhalifu wa kivita kama alivyofanyiwa Saddam Hussein au Slobodan Milosevic
Mwisho wa siku Ufaransa walifeli kumshtaki kagame mpaka sasa wanamchungulia tu kwa mbali.
 
Good history review,sio kila saa Magufuli au Lissu au Samia au sijui....
 
Back
Top Bottom