Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,350
- 26,166
Nawaandikia viongozi, watumishi wa umma, watu wote wa vyombo vya dola, wanasiasa,wanahabari, wasanii na wananchi wote wa kawaida. Tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2015, Rais Dr. John Pombe Magufuli amejipambanua kwa mambo mbalimbali kupitia matendo na maneno yake.
Amevionyesha wazi anavyofichukia (mfano rushwa, ufisadi na uongo) na anavyovipenda (mfano ukweli, uthubutu na kujituma). Hivyo amevionyesha waziwazi kwa kuteua, kutumbua, kukemea, kuelekeza na kuongoza. Tayari tumeshamjua Rais wetu ana vitu vyake.
Rais si mtu wa kujaribu wala kujaribiwa. Ni mkali kwa anavyovichukia na mcheshi na mwenye utani mwingi kwa vinavyomfurahisha. Anasema na kutenda anachokiamini na katika namna yake ya kipekee kwa awamu yake. Kujua hayo kwa miaka miwili na ushee sasa ni jambo kubwa.
Baada ya kumjua Rais wetu, sasa twende na midundo yake. Midundo aliyoianza kuipiga mwaka 2015, haitabadilika na wala hana hata dalili ya kuibadilisha. Kucheza tofauti na midundo ya Rais ni kutafuta vya kulalamikia kila uchao.
Heri ya mwaka mpya 2018!