Mheshimiwa rais kwanza nikupongeze kwa kuchaguliwa kuongoza kwa muhula mwingine. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akulinde, akupe hekima kama jinsi mfalme Selemani alivyoomba hekima, ili taifa hili liweze kusonga mbele. Miaka 5 umeiongoza kwa mafanikio makubwa hivyo ni matumaini yangu hii miaka 5 ijayo itakuwa yenye mafanikio zaidi.
Mheshimiwa rais, mimi ni msomi mwenye degree ya uhasibu, pia nina taaluma ya juu ya uhasibu yaani ni Certified Public Accountant (CPA). Ajira imekuwa ngumu sana, nimetafuta kazi kwa muda mrefu bila mafanikio. Umri unazidi kwenda na pia nina familia inayonitegemea.
Nimekuwa nikiendesha maisha yangu kwa tabu sana mpaka najihisi kukata tamaa. Mheshimiwa rais najua wasaidizi wako wanapitia hapa kama sio wewe mwenyewe, natumaini kupitia wao watakufikishia ombi langu, hivyo naomba unikumbuke mtanzania mwenzako. Wewe ni rais wa watanzania wote, maskini na matajiri.
Nakuomba unikumbuke mimi mnyonge ninayehangaika na maisha mheshimiwa Rais.
Natanguliza shukrani zangu za dhati na nakutakia utumishi mwema. Mungu akulinde.