Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

Baada ya kukamilisha ukusanyaji data wilayani Igunga baada ya Nzega na Sikonge mkoani Tabora juu ya hali ya elimu nchini na huduma za afya, nimejiuliza maswali mengi sana.

Hivi Rais wangu anasema atatembea na masikini, hivi masikini wapi??

Katika shule moja, unakuta walimu wanne wanafunzi mianane, shule zingine walimu watatu wanafunzi mia sita, hao watoto wanasomaje???

Tar 01/09/16 nilitembelea shule ya Msingi Mtungulu. Shule hii iko kilomita 22 kutoka Igunga mjini. Nilikuta walimu watano (05) huku wanne wakiwa kazini mwingine akiwa na matatizo.

Idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni zaidi ya 600. Masomo ya yanayondishwa ni kama vile Historia, Uraia, Kiswahili, Kiingereza, Haiba na michezo, Hisabati, Jiografia, Tehama nk.

Madarasa ni kuanzia la kwanza mpaka la saba. Kwa masomo hayo hapo juu walimu watafundishaje???

Maana yake ni kwamba ni kwamba, vipindi vingi havifundishwi. Watoto wengi wanakwenda kuzurura shuleni.

Nilipofanya utafiti juu ya hali ya uwezo wa watoto, bado tatizo la kutokujua kusoma na kuandika ni kubwa sana. Sasa, kama tunashindwa kupeleka walimu kusaidia watoto hao wa masikini, hao masikini tutawasaidiaje????

Kuna msaada kwa masikini zaidi ya elimu na Afya???

Tuweke kando siasa za watumishi hewa, tusaidie Taifa hili. [HASHTAG]#Ajiri[/HASHTAG] walimu

Mwambie kwa sasa hatuhitaji UWANJA wa NDEGE wa KIMATAIFA wa CHATO.
 
Nadhani ishu ya madawati si kipaombele sana walimu,vitabu kwanza.umri hausubiri
 
Tatizo kubwa ni kwamba nina kundi kubwa nyuma yangu linaloniangalia hasa kwa wakati huu, bora nikae kimya kesi ya uchochezi inaweza kunihusu ktk hii mada,
 
Baada ya kukamilisha ukusanyaji data wilayani Igunga baada ya Nzega na Sikonge mkoani Tabora juu ya hali ya elimu nchini na huduma za afya, nimejiuliza maswali mengi sana.

Hivi Rais wangu anasema atatembea na masikini, hivi masikini wapi??

Katika shule moja, unakuta walimu wanne wanafunzi mianane, shule zingine walimu watatu wanafunzi mia sita, hao watoto wanasomaje???

Tar 01/09/16 nilitembelea shule ya Msingi Mtungulu. Shule hii iko kilomita 22 kutoka Igunga mjini. Nilikuta walimu watano (05) huku wanne wakiwa kazini mwingine akiwa na matatizo.

Idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni zaidi ya 600. Masomo ya yanayondishwa ni kama vile Historia, Uraia, Kiswahili, Kiingereza, Haiba na michezo, Hisabati, Jiografia, Tehama nk.

Madarasa ni kuanzia la kwanza mpaka la saba. Kwa masomo hayo hapo juu walimu watafundishaje???

Maana yake ni kwamba ni kwamba, vipindi vingi havifundishwi. Watoto wengi wanakwenda kuzurura shuleni.

Nilipofanya utafiti juu ya hali ya uwezo wa watoto, bado tatizo la kutokujua kusoma na kuandika ni kubwa sana. Sasa, kama tunashindwa kupeleka walimu kusaidia watoto hao wa masikini, hao masikini tutawasaidiaje????

Kuna msaada kwa masikini zaidi ya elimu na Afya???

Tuweke kando siasa za watumishi hewa, tusaidie Taifa hili. [HASHTAG]#Ajiri[/HASHTAG] walimu
Hao unaowaonea huruma wenyewe hawajali ndio kwanzaa kwenye Chaguzi wanaongoza kuvaa mafulana..yanayotamka Maneno ya kejeli
 
Yaani kuna watu huwa wana mipaka ya kufikiri . Nahisi yeye aliahidi kwenye familia yake kuwa akipata akazi atafanya vitu fulani fulani ila ameshindwa kutimiza so anafikiri wote watakuwa sawa na yeye.

Ki ukweli elimu ni waalimu hata kama wanafunz watakaa chini lakini waalimu wakiwepo wa kutosha na wanafunzi wakafundishwa vipindi husika kwa mpangalio mzuri sidahni kama kutakuwa na makelele ya kuhitaji hayo madawati.

Ila waalimu wakipewa stahiki zao zote na kuboreshewa mishahara yao na vitendea kazi vikawa sawa elimu yetu itakuwa juu maradufu hili suala la madawati mpaka sasa sijaona hela iliyotoka serikalini zaidi ya kuotoa hamasa kwa wananchi na wafanyabiashara kujtolea ili kufanikisha shule zote nchini ziwe na madawati. Lakini issue ya waalimu serikali inatakiwa ihusike 100% ili kuifanikisha.

TIME WILL TELL

Shida nchi yetu ni continuity. Mkwere hili alianza kulifanyia kazi lakini ndio hivyo tena hakufanikiwa kuliona miaka yote kaliona dakika za mwisho kabla haijaiva wengoine wameipua.
 
Ha ha haaaaa usinivunje mbavu aeti matisheti!
Ndio ukweli ndugu watu wa namna hiyo wanaabudu CCM kama mungu ndio maana mtukufu anaweza kudanganya anavyoweza na watu wakampigia Makofi
 
Issue ni VIPAUMBELE, VIPAUMBELE NA VIPAUMBELE ma men, huwezi kuanza kuezeka kabla ya kujenga msingi na kuta za nyumba, haya sasa Madawati mpaka yamepitiliza na mengi yako nje hakuna vyumba vya madarasa! Na walimu je?
Thats critisism...mtakosoa hadi lini au mnalipwa? Wewe kama mtz unanafasi ya kurekebisha hilo zaidi ya kukosoa kila jambo
 
Hata yeye anajua kuwa anachosema sio anachofanya

namba tunaisoma wote kwakwel. leo bibi yangu ananilalamikia maisha magumu namwambia bibi wewe si ndo ccm mbele kwa mbele bado anaitetea. yan wana fisiemu ni sheedah
 
Kuna shule ya msingi Ndechela huku Nanyumbu, Mtwara haijawahi kuwa na choo hata tundu moja. Watoto wote wanalikuwa wanajisaidia porini hadi mwaka jana. Mbunge wao aliahidi atawajengea. Sijaenda hivi karibuni nikashuhudie kama amewajengea. Naona hao masikini anaowasema anawajua yeye mwenyewe.
 
Thats critisism...mtakosoa hadi lini au mnalipwa? Wewe kama mtz unanafasi ya kurekebisha hilo zaidi ya kukosoa kila jambo
Mtz ana nafasi gani yakurekebisha ikiwa mtukufu anaamini huku Duniani mwenye akili isipokuwa yeye tu
 
Embu jitengeni na siasa tumsaidie huyu mkuu kuinua taifa letu sio lake peke yake.

Kwani wewe kwa miezi kumi ulitaka awe ameisha fanya nini???, nipe tu mfano.

Mkuu, rais keshasema mwacheni awaletee wananchi maendeleo na hataki mtu wa kumpotezea muda. Ukijitia kimbelembele kutoa ushauri si ndio utaswekwa ndani kwa uchochezi?
 
Mkuu, rais keshasema mwacheni awaletee wananchi maendeleo na hataki mtu wa kumpotezea muda. Ukijitia kimbelembele kutoa ushauri si ndio utaswekwa ndani kwa uchochezi?
Wananchi wanataka maendeleo.
 
Maendeleo hayaji kama mlipuko wa bomu..it is a step wise thing..kwani ww uliiahid familia yako nn kwamba ukipata kaz utawafanyia..mpaka leo umefanya vingap?
mkuu mbona mtoa mada ameelezea vizuri tu na wewe una panic? ni masuala ya kuelekezana na kujadili kwa muktadha wa jamii yetu.
 
Back
Top Bottom