Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

gibishi

Senior Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
182
Reaction score
268
Baada ya kukamilisha ukusanyaji data wilayani Igunga baada ya Nzega na Sikonge mkoani Tabora juu ya hali ya elimu nchini na huduma za afya, nimejiuliza maswali mengi sana.

Hivi Rais wangu anasema atatembea na masikini, hivi masikini wapi??

Katika shule moja, unakuta walimu wanne wanafunzi mianane, shule zingine walimu watatu wanafunzi mia sita, hao watoto wanasomaje???

Tar 01/09/16 nilitembelea shule ya Msingi Mtungulu. Shule hii iko kilomita 22 kutoka Igunga mjini. Nilikuta walimu watano (05) huku wanne wakiwa kazini mwingine akiwa na matatizo.

Idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni zaidi ya 600. Masomo ya yanayondishwa ni kama vile Historia, Uraia, Kiswahili, Kiingereza, Haiba na michezo, Hisabati, Jiografia, Tehama nk.

Madarasa ni kuanzia la kwanza mpaka la saba. Kwa masomo hayo hapo juu walimu watafundishaje???

Maana yake ni kwamba ni kwamba, vipindi vingi havifundishwi. Watoto wengi wanakwenda kuzurura shuleni.

Nilipofanya utafiti juu ya hali ya uwezo wa watoto, bado tatizo la kutokujua kusoma na kuandika ni kubwa sana. Sasa, kama tunashindwa kupeleka walimu kusaidia watoto hao wa masikini, hao masikini tutawasaidiaje????

Kuna msaada kwa masikini zaidi ya elimu na Afya???

Tuweke kando siasa za watumishi hewa, tusaidie Taifa hili. [HASHTAG]#Ajiri[/HASHTAG] walimu
 
Vipi kwene suala la madawati? kuna ambao bado wanakaa chini?
 
hata kama kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati lake inasaidia nini kama hafundishwi? walimu kwanza.

Labda awamu ya pili ni kuboresha hayo mapungufu baada ya kuhakikisha kwanza wote wamekaa kwene madawati ili la walimu litafuata nafikiri si muda.
 
Elimu na afya ndo zawadi kubwa anayiweza wapa waTanzania.Tukipata hivyo mengine tutacheza nayo wenyewe
 
Jaman anaijitahd imechukua zaid ya miaka 52 kushindwa kukomesha tatizo hili kwanza hana mwaka lakin kajitahd kwa kiasi chake wafanyakzi hewa wanafunzi hew vita dhid ya ufsad
 
labda awamu ya pili ni kuboresha hayo mapungufu baada ya kuhakikisha kwanza wote wamekaa kwene madawati ili la walimu litafuata nafikiri si mda

Ni kweli mkuu lakini huko vijijini kuna shule ambazo hazikuwa na upungufu wa madawati bali upungufu wa wanafunzi kwa sababu kutokana na uhaba wa walimu wazazi hawahamasiki kupeleka watoto shule. Kama shule nzima ina waalimu wawili unatarajia nini hapo?
 
Inashikitisha sana. Kinachotia hasira ni majigambo ya wanasiasa hasa wabunge, wakati hali ya watu wao ni ya ufukara wa kihalaiki. MUNGU ATAWAONA TU.
 
Kuna shule iko Katoro Geita, ina wanafunzi 10,000.ukiwakuta nje mfano wakati wa mapumziko utadhani michezo ya umitashumta unafanyika hapo.
Ila sijui idadi ya walimu na mahitaji mengine.siku nikirudi tena huko nitaulizia
 
Embu jitengeni na siasa tumsaidie huyu mkuu kuinua taifa letu sio lake peke yake.

Kwani wewe kwa miezi kumi ulitaka awe ameisha fanya nini???, nipe tu mfano.
 
Kuna shule iko Katoro Geita, ina wanafunzi 10,000.ukiwakuta nje mfano wakati wa mapumziko utadhani michezo ya umitashumta unafanyika hapo.
Ila sijui idadi ya walimu na mahitaji mengine.siku nikirudi tena huko nitaulizia

Hao wengi mno wanaelewa chochote kweli.
 
Yaani kuna watu huwa wana mipaka ya kufikiri . Nahisi yeye aliahidi kwenye familia yake kuwa akipata akazi atafanya vitu fulani fulani ila ameshindwa kutimiza so anafikiri wote watakuwa sawa na yeye.

Ki ukweli elimu ni waalimu hata kama wanafunz watakaa chini lakini waalimu wakiwepo wa kutosha na wanafunzi wakafundishwa vipindi husika kwa mpangalio mzuri sidahni kama kutakuwa na makelele ya kuhitaji hayo madawati.

Ila waalimu wakipewa stahiki zao zote na kuboreshewa mishahara yao na vitendea kazi vikawa sawa elimu yetu itakuwa juu maradufu hili suala la madawati mpaka sasa sijaona hela iliyotoka serikalini zaidi ya kuotoa hamasa kwa wananchi na wafanyabiashara kujtolea ili kufanikisha shule zote nchini ziwe na madawati. Lakini issue ya waalimu serikali inatakiwa ihusike 100% ili kuifanikisha.

TIME WILL TELL
 
Back
Top Bottom