Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

Rais wangu Magufuli, uko kwa ajili ya masikini wapi?

Mungu mwema, atakayevumilia mpaka mwisho ndie atakayeokoka.
 
Baada ya kukamilisha ukusanyaji data wilayani Igunga baada ya Nzega na Sikonge mkoani Tabora juu ya hali ya elimu nchini na huduma za afya, nimejiuliza maswali mengi sana.

Hivi Rais wangu anasema atatembea na masikini, hivi masikini wapi??

Katika shule moja, unakuta walimu wanne wanafunzi mianane, shule zingine walimu watatu wanafunzi mia sita, hao watoto wanasomaje???

Tar 01/09/16 nilitembelea shule ya Msingi Mtungulu. Shule hii iko kilomita 22 kutoka Igunga mjini. Nilikuta walimu watano (05) huku wanne wakiwa kazini mwingine akiwa na matatizo.

Idadi ya wanafunzi shuleni hapo ni zaidi ya 600. Masomo ya yanayondishwa ni kama vile Historia, Uraia, Kiswahili, Kiingereza, Haiba na michezo, Hisabati, Jiografia, Tehama nk.

Madarasa ni kuanzia la kwanza mpaka la saba. Kwa masomo hayo hapo juu walimu watafundishaje???

Maana yake ni kwamba ni kwamba, vipindi vingi havifundishwi. Watoto wengi wanakwenda kuzurura shuleni.

Nilipofanya utafiti juu ya hali ya uwezo wa watoto, bado tatizo la kutokujua kusoma na kuandika ni kubwa sana. Sasa, kama tunashindwa kupeleka walimu kusaidia watoto hao wa masikini, hao masikini tutawasaidiaje????

Kuna msaada kwa masikini zaidi ya elimu na Afya???

Tuweke kando siasa za watumishi hewa, tusaidie Taifa hili. [HASHTAG]#Ajiri[/HASHTAG] walimu
Utakuwa umeshasikia usemi, "Rome wasn't built fin a day".

Rais hajamaliza hata mwaka tangu haingie madarakani. Unategemea awe ameshatatua tatizo la waalimu ambalo kulishughulikia linaweza kuchukua miaka hata 10!
 
Kuna janga LA watoto hawa waliomaliza Jana Kuoneshwa MITIHANI ndo kinaboa Sana mtoto anafika form Four hajui Kusoma..
 
Baba Mungu kwa nini wasimama mbali nyakati za shida za watanzania kama hizi
mkuu naona umeona ni bora uimbe pambio, usijali Mungu yupo kazini utamwonatu ndugu vuta subra.
 
Maendeleo hayaji kama mlipuko wa bomu..it is a step wise thing..kwani ww uliiahid familia yako nn kwamba ukipata kaz utawafanyia..mpaka leo umefanya vingap?

Issue ni VIPAUMBELE, VIPAUMBELE NA VIPAUMBELE ma men, huwezi kuanza kuezeka kabla ya kujenga msingi na kuta za nyumba, haya sasa Madawati mpaka yamepitiliza na mengi yako nje hakuna vyumba vya madarasa! Na walimu je?
 
Baba Mungu kwa nini wasimama mbali nyakati za shida za watanzania kama hizi
Mungu akamwambia Musa "kwa nini kunililia mimi? waambie wana wa Israel wasonge mbele"

Usimlilie Mungu, songa mbele
 
Yaani mm kinachoniuma ni kutufanya mazombie watoe tamko ili tujue hata kama Ajira mwakani tukae tukijua
 
"Sio kila mtu anasifa ya kuwa kiongozi au Raisi". Naomba ili liwe somo lenu hadi 2020.
 
Embu jitengeni na siasa tumsaidie huyu mkuu kuinua taifa letu sio lake peke yake.

Kwani wewe kwa miezi kumi ulitaka awe ameisha fanya nini???, nipe tu mfano.
tumsaidie kuajiri walimu au? maana sijui la kumsaidia coz he seems to know everything
 
Mkuu ni kweli tunatakiwa kumsaidia Rais..na tunamsaidia kwa kulipa kodi za PAYE, kodi kwenye mafuta na bidhaa zingine, na hata tulipowekea VAT kinyemela kwenye miamala ya fedha hatujaandamana. Ebu jiulize Kiongozi mwenye kujielewa angeanza kushugulikia matatizo ya elimu na walimu pamoja na afya, au angekurupuka na safari ya Dodoma ambayo imeteka akili/mawazo/resources za wizara zote kwa sasa. Tatizo ni kukosa vipaumbele na hata alipoweka kipaumbele cha serikali yake kuwa ni Tanzania ya viwanda.....akaibuka na safari ya Dom from nowhere.
Hivi kuhamia dodoma ni tsh ngapi??? Na ni miaka mingapi???

Kufufua viwanda/kuanzisha viwanda ni shilingi ngapi na ni miaka mingapi???

Na kuboresha elimu ni shilingi ngapi??? Na ni miaka mingapi???

Nilichogundua kumbe tulijiandaa kupinga na kubisha.
Mwisho mtataka uchumi uwe sawa na marekani kwa muda alioingia.
 
Kama una safari ya kwenda Mwanza ukapanda basi kuanza safari yako, kufika Mlandizi ukashuka ukapanda basi la kwenda Tunduma.....ni either hujui uendako au akili hazijakaa vizuri, haijalishi unatumia miaka mingapi kwenda Tunduma. Simpo logic
 
Changamoto ninayoona kwa kwa Namba moja ni kwamba, anapeleka mambo yeye kama yeye, zidumu fikra za Mwenyekiti..viongozi waandamizi hawafanyi kazi kwa utashi wao binafsi, hata mambo madogo lazima zipate baraka za namba moja...Uchumi yeye, afya yeye, elimu yeye, ubunge yeye nk. ushahidi ni kwamba hakuna kiongozi yeyote anayeng'ara kwa utendaji maana jamaa kashikilia nyota zote..nitarudi!
 
Kama una safari ya kwenda Mwanza ukapanda basi kuanza safari yako, kufika Mlandizi ukashuka ukapanda basi la kwenda Tunduma.....ni either hujui uendako au akili hazijakaa vizuri, haijalishi unatumia miaka mingapi kwenda Tunduma. Simpo logic
Kwani mkuu wewe unajua kwanini watu wameamua wahamie dodoma.
 
Kwani mkuu wewe unajua kwanini watu wameamua wahamie dodoma.

Iwe najua au sijui sio hoja hapa, hoja ni lack of vipaumbele. Kwani kwenda Dom ilikuwa kipaumbele kabla ya elimu/afya na Tz ya viwanda? Au kwenda Dodoma kuna accelerate kuanzishwa kwa viwanda? au kuna rahisisha maboresho ya elimu?
 
Wewe umejuaje kama haikuwa kipaumbele???au kwa vile hukutangaziwa.

harafu unapoambiwa serikali inahama dsm kuupisha mji huu wa kibiashara unaelewaje????

Harafu nikuulize serikali ina ratiba za kufanya mambo mangapi na ni kipi kinatakiwa kuanza kabla ya kingine?????

Elimu tumeanza na madawati, na ujenzi wa mabweni udsm na maabara kila shule ya sekondari kama mwanzo tu wa hayo maboresho. UNABISHA???.

usafiri wa anga,ndege mbili za kuanzia zimegizwa kufufua shirika.UNABISHA???

Miezi tisa unataka kuwe na viwanda viwe vinzalisha magari na computer na hospitali zote za kata ziwe tayari ni za rufaa[emoji1].kwanini nisikuite mchawi.
 
Mkuu ni kweli tunatakiwa kumsaidia Rais..na tunamsaidia kwa kulipa kodi za PAYE, kodi kwenye mafuta na bidhaa zingine, na hata tulipowekea VAT kinyemela kwenye miamala ya fedha hatujaandamana. Ebu jiulize Kiongozi mwenye kujielewa angeanza kushugulikia matatizo ya elimu na walimu pamoja na afya, au angekurupuka na safari ya Dodoma ambayo imeteka akili/mawazo/resources za wizara zote kwa sasa. Tatizo ni kukosa vipaumbele na hata alipoweka kipaumbele cha serikali yake kuwa ni Tanzania ya viwanda.....akaibuka na safari ya Dom from nowhere.

Tuacha ubinafsi. Kuhamia Dodoma ni mkakati wa kufikisha huduma kwa wengi. Je hampendi wengi tufaidi maendeleo? Hili la kuhamia Dodoma ni kipaumbele cha Taifa letu na kwa manufaa ya Taifa. Wa Dar ndio hawalitambui hili.
 
Hivi kuhamia dodoma ni tsh ngapi??? Na ni miaka mingapi???

Kufufua viwanda/kuanzisha viwanda ni shilingi ngapi na ni miaka mingapi???

Na kuboresha elimu ni shilingi ngapi??? Na ni miaka mingapi???

Nilichogundua kumbe tulijiandaa kupinga na kubisha.
Mwisho mtataka uchumi uwe sawa na marekani kwa muda alioingia.

Tuacheni ubishi. Tujenge Taifa Letu kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom