Rais wafokee wakandarasi kwa kuchelewesha SGR kati ya Dar na Morogoro

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
13,405
19,069
Habarini wana jamvi. Juzi hapa tulimsikia rais akiwa-mind wakandarasi kwa kuchelewesha mradi wa stendi mpya ya kisasa pale mbezi jambo ambalo hakulitegemea tena mbele ya mgeni wake, Rais wa Malawi.

Sasa ni bora tumwambie kuhusu hili la SGR, maana tuliambiwa mwezi Novemba mwaka jana ingekuwa imeanza kazi kipande cha Dar-Moro, sasa ni karibia mwaka mzima umepita hatujasikia matangazo ya wapi tiketi zinakatwa. Haya mambo yanachelewesha maendeleo na kuleta ma-variation ambayo hayana mashiko.

Tafadhali sana Mh, najua kwa sasa mambo ya kampeni yamekubana sana, ukifanikiwa kurudi kazi yetu itakuwa ni kukumulikia tu maeneo ambayo watu wamelala usingizi wa pono.
 
CCM ndio harijojo kama unawadai wahi kuwafungulia kesi kabla chama hakijavunjika, la si hivyo deni lako litakua kwenye kumbukumbu tu.
 
tuliambiwa mwezi Novemba mwaka jana ingekuwa imeanza kazi kipande cha Dar-Moro, sasa ni karibia mwaka mzima umepita hatujasikia matangazo ya wapi tiketi zinakatwa. Haya mambo yanachelewesha maendeleo na kuleta ma-variation ambayo hayana mashiko.
Usiiamini CCM Mpya hata katika kupiga kura yako 28 October 2020, hivyo fanya maamuzi sahihi achana na kupiga kura kwa kutegemea ahadi hewa lukuki ikiwemo hii ya SGR Reli Mpya.
 
Tatizoo unazungumza na chama mfu ,aka mazombi ,CCM ndio harijojo kama unawadai wahi kuwafungulia kesi kabla chama hakijavunjika ,la si hivyo deni lako litakua kwenye kumbukumbu tu.
Usijali, bado mwezi mmoja tuu Lissu atakuwa ikulu pale ufipa atashughulikia hao wakandarasi akiwa na chama hai chadema. Achana na CCM mfu.
 
Tatizo Magufuli ni Rais mpole sana, ufisadi kila kona!

5430210.jpg
 
Injinia Faustine Kataraia mkurugenzi TRC azungumzia vipande vya reli ya SGR Mpya



Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge azungumzia sababu ya kuwaita viongozi wa dini kutembelea sehemu hiyo ya ujenzi wa reli.
 
Kuna tofauti kati ya mbwa anaebweka na mbwa mkali.Sasa mkuu kama Magufuli siyo Rais mpole sana ule ufisadi wa TZS 1.5 trillion ulitoka wapi?Kumbuka tokea uhuru hakuna Rais ambae aliwahi kufanya ufisadi wa TZS 1.5 trillion!Magufuli ni mbwa mbwekaji.
 
Sasa mkuu kama Magufuli siyo Rais mpole sana ule ufisadi wa TZS 1.5 trillion ulitoka wapi?Kumbuka tokea uhuru hakuna Rais ambae aliwahi kusimamia show ya ufisadi wa TZS 1.5 trillion!
Labda hizi ndo zimenunua ndege kwa cash, natamani pia tununue airbus A380-800 ili tuwafunge midomo manyang'au wa hapo jirani.
 
Mkuu kama ulipata tenda katika huo mradi na haujalipwa malipo yako yote dai mapema maana unaemwambia amebakiza wiki tatu tu za kukaalia hicho kiti.chagua Lisu 2810 tupate katiba Mpya yenye kumpa madaraka mwananchi kuliko Rais.
 
Chadema wakishinda hakika yake watang'oa reli na kuuza mataruma kama vyuma chakavu hawajui nini maana ya maendeleo wale jamaa,

Watachofanya sana sana ni kuanzisha kozi ya lazima ya kingereza kwa nchi nzima.
 
Labda hizi ndo zimenunua ndege kwa cash, natamani pia tununue airbus A380-800 ili tuwafunge midomo manyang'au wa hapo jirani.

Kwanini tukatengeneze ajira kwenye viwanda vya MABEBERU.

Kwanini matrilioni ya kununua ndege yasiwekezwe hapa nchini?
 
Back
Top Bottom