Rais wa Senegal asema nchi hiyo hairuhusu ushoga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
RAIS wa Senegal Macky Sall ametetea hatua ya taifa lake kupiga marufuku mapenzi baina ya watu wa jinsia moja, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.


Mataifa 28 kati ya 49 yaliyoko Kusini mwa janga la Sahara yameweka sheria zinazopiga marufuku shughuli kama vile ushoga na usagaji.


Nchini Senegal watu wanaopatikana na hatia ya kushiriki vitendo kama hivyo hupewa adhabu ya kifungo cha miaka mitano gerezani.


Rais Sall alisema sheria za nchi hiyo zinaoana na mila na tamaduni za watu wake zinazochukulia mapenzi baina ya watu wa jinsia moja kama mwiko.


“Taifa la Senegal haliruhusu mapenzi ya jinsia moja. Sheria zetu sawa na tamaduni za watu wetu hazikubali tabia kama hizi,” Rais Sall akaambia wanahabari jijini Dakar.


Kiongozi huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya Waziri Mkuu Trudeau ambaye alikuwa ziarani Senegal baada ya kuzuru Ethiopia, kudai kuwa aliibua suala katika majadiliano kati yao.


“Huwa naibua masuala ya haki za kibinadamu popote ninapoenda. Kila wakati ninapokutana na kiongozi yeyote mimi huzungumzia maadili ya Canada,” Trudeau akawaambia wanahabari.
 
HATA SISI HATURUHUSU USHOGA.

UKIITWA 'SHOGA' KAMA NI MWANAUME BASI PIGANA MPAKA UTETEE HESHIMA YAKO.

NENO LENYEWE TU "SHOGA" KWA MWANAUME WA KIAFRIKA KUITWA HIVYO INA MAANA AMETUKANWA TUSI ZITO, LENYE KUDHALILISHA NA ANAWEZA KUKUPELEKA MAHAKAMANI IKIWA HATA KUNASA MAKOFI. YES

UKIAMBIWA BABAAKO NI SHOGA INA MAANA UMETUKANIWA MZAZI! HAPO SASA HATA SILAHA YA MAWE INAWEZA IKATUMIKA KUTETEA HESHIMA YA MZAZI YES.

LAKINI KWA MATAIFA HAYO YENYE MAIBILISI MWANAUME UKIITWA SHOGA, NI KAMA VILE MTU AKUITE DIRECTOR!! HAHAHAHA

MAKONDA HATAKIWI KWENDA KWAO KWA SABABU HATAKI USHOGA, SASA SI BORA ASIKANYAGE HUKO? KWANI ASIPOENDA ATAKOSA PUMZI?

HAKI ZA BINADAMU:

TETEENI KWANZA HAKI ZA WANAUME WASIINGIE KTK KUINGILIWA NA WANAUME WENGINE. HIYO NDIO HAKI YA BINADAMU.


HAKI ZA BINADAMU:.

TETEENI HAKI ZA TAMADUNI ZA KIAFRIKA. MUME AOE AZALISHE, SIO AINGILIWE NA KUTOA HARUFU KALI NA AKAWA LEGELEGE TUTAKOSA HATA NGUVU KAZI.
 
Back
Top Bottom