Ndugu zangu Watanzania,
Rais wa Romania mh Klaus Werner lohannis anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi Nchini Tanzania kuanzia Tarehe 16 hadi 19 mwezi huu.ambapo masuala mbalimbali yanatarajiwa kuzungumzwa katika kuimarisha ushirikiano na mwenyeji wake Rais mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika,jasiri muongoza njia,simba wa nyika,nuru ya wanyonge,Sauti ya Afrika,mtetezi wa wanyonge na tumaini la watanzania.
Tanzania inaendelea kuwa kivutio cha wengi na kila mtu anatamani kufanya kazi na Tanzania, kushirikiana na Tanzania Na kuungana na Tanzania Katika masuala mbalimbali ya kiuchumi,kisiasa, kidiplomasia,n.k. hii inakuja ndani ya muda mfupi wa kuwa madarakani kwa Rais samia ambapo ameipaisha sana Tanzania na kuiweka katika kilele cha macho ya Dunia , ambapo sasa inatazamwa na kila Taifa kama Taifa la kuheshimika na kuigwa kabisa kutoka barani Afrika.
Ndio maana tunaona ndani ya muda mfupi tumeweza kama taifa kupokea viongozi mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali,ujumbe wa viongozi kutoka kila sehemu,.tuliona makamu wa Rais wa Taifa kubwa kabisa hapa Dunia yaani Marekani akiitembelea Tanzania,tumeona juzi juzi tu hapa tumetoka kumpokea Rais wa Ujerumani.
Tanzania imekuwa ni kama maji tu usipoyanywa utayaoga tu.ndio maana tunaona mafuriko ya watalii, wafanyabishara wakubwa, wawekezaji wakimiminikia na kufurika Tanzania.hii yote ni kazi ya Rais samia,ni mikono ya Rais samia,ni juhudi za Rais samia,ni maono ya Rais samia,ni ushawishi na nguvu za Rais samia,ni matunda za ziara ambazo amekuwa akifanya Rais samia nje ya nchi,ni mikakati na mipango ya Rais samia katika kuhakikisha tunakuwa wakwanza katika kuzoa fursa zote zinazopatikana katika uso wa Dunia na hii yote inatokana na kukubalika kwa kiwango cha juu kwa Rais samia na namna anavyoheshimika ,kupendwa na kukubalika ndani na nje ya Taifa letu.
Tuendelee kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa kituo cha Biashara,uwekezaji na utalii barani Afrika vitu vitakavyotupatia fursa nyingi za kiuchumi na kukuza uchumi wetu kwa kasi ya upepo.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.