RAIS WA IRAN MWENDAWAZIMU.... LAKINI?..... CASTRO wa pili.

RAIS WA IRAN MWENDAWAZIMU.... LAKINI?..... CASTRO wa pili.

Mkandara said:
Mzee ES,
sasa umeona ukweli unavyozidi kujitokeza hapa?...
Kuna huyu anayejiita Mzee mwanakijiji ambaye anakuja na mapenzi yake bila hata kufikiri, jitu zima linasema ovyo! Yaani sikuelewa kama huyu jamaa mwenyewe ndio kundi la hao ambao kwamba!

Hakuna kitu kinachochekesha kama kujibu hoja kwa tusi! Mkandara, nitakusamehe kwa hilo kwani nilichosema ni historia rahisi ambayo mtu yeyote anayejua atakiri wazi. Nilichokisema si dini ni historia. Hata hivyo nitakujibu kwa hoja!!

Ebu nambieni jamani Mtume aliandika barua mwaka 628BK hiyo BK imesimama kama kifupi cha nini? Before Christ!.. hii mpya, na hata kama ikiwa baada ya Christ.
Je anafahamu kwamba Mtume hakujua kusoma wala kuandika

Kwa vile huijui historia ya Uislamu, nimeamua kujitolea kukusaidia na miye sina muda wa kashfa! Kama mtume hakujua kusoma wala kuandika, Kurani Imetufikiaje? Si yeye alikariri na baadaye alirudia kariri yake hiyo na ikaandikwa na manasaba wa Mtume (SAW)? Baada ya mkataba wa Hudaibiya Mtume aliwaita wafuasi wake wa karibu zaidi na kuwaagiza kwenda kwenye nchi na falme za karibu ili kutoa mwaliko kwa wakuu hao kusilimu. Nitakutajia baadhi yao:

- Dihyah ibn Khalifah al-Kalbi (ra) - Alitumwa kwa Heraklio Mfalme wa Himaya ya Roma ya Mashariki (Byzantine)
- Abdullah bin Hudhafah (ra) - Alitumwa kwa Kusras Parves Mfalme wa Uajemi
- Amr bin Umayyah (ra) - Alitumwa kwa Negus mfalme wa Uhabeshi (Abyssinia)
- Hatib' bin Abi Baitah (ra) - Alitumwa kwa Mukawis Mtawala wa Misri
- Shuja bin Wahab al-Asadi (ra) - Alitumwa kwa Harith Gassani Gavana wa Syria
- 'Ala bin Hadrami (ra) - Alitumwa kwa Al-Mundhir Bin Sawa, Mtawala wa Bahrain

zaidi ya hapo nchi gani za magaharibi ambazo anazungumzia zilikuwepo kiutalawa wakati ya mtume na waliweza kusoma Kiarabu. Huko Saudia kwenyewe wasomi walihesabika tena wanaojua kusoma na kuandika ndio elimu kubwa wakati huo nani aliweza kuandika lugha nyingine tofauti na kuzituma ktk mataifa..

Nilikosea niliposema Magharibi, ninamaanisha Himaya ya Roma ya Mashariki. Na watafsiri wa lugha hawakuanza leo!!!!

pia hizo barua zilikwenda kwa njia gani.. DHL?...
Kwa njia ya ngamia na punda na waendashaji wake!!

nani alimtambua Mtume kama kiongozi hali - waarabu wajulikanao kama Wasabi (Kureish) ndio walikuwa watawala. Yeye kama nani aandike barua hali maisha yake yote mwenyewe alikuwa akijificha kati ya Mecca na Madina.

Wengi hawakukubali wito huo, ndo Mtume na baadaye mahalifa wake walipoanza mapambano!!

Jamani acheni upuuzi wenu tunazungumzia mtu mmoja ambaye kaja na agenda yake. Siwezi kuutukana Ukristu kwa sababu ya agenda za Bush na kusema anafuata mafundisho yaa. Tuwe watu wazima, na ndio maana sikutaka kabisa kujiunga na hiyo site yake maana anaongea kama MLOKOLE!... Siasa na Dini vitu tofauti ndugu yangu unaonekana Mchawi tu. Mawazo yako yanaweza kuwa mazuri sana lakini kwa siasa za Bongo unaonekana sawa na huyo mwendawazimu Ahmadinejad.

Mkandara, kwa heshima kubwa na taadhima, sijawahi kuutukana Uislamu mahali popote wala kuukejeli!! Nimekulia na kusomea kati ya Waislamu! Hata hivyo miye siogopi kujadili kitu chochote!! Uislamu unajadilika na unaweza kuangaliwa katika mwanga wa ukosoaji. Itakuwa nafanya kosa la kiakili kupokea maneno ya watu bila ya kuyafanyia uchunguzi. Uniwie radhi kama hoja yangu umeichukukia kama matusi!!! Siyo kusudio langu.

Lengo langu ni kuonyesha kuwa Barua ya Rais wa Irani inafuata mfululizo wa barua kama hiyo ulioanzishwa na Mtume Muhammad. Tutajidanganya tukiliangalia suala la Irani kwa mwanga wa siasa tu. Kuna suala la dini na barua hiyo imeifichua. Soma hiyo barua utaelewa nasema nini au mnataka niende kuichambua barua nzima kwa kutumia mwanga wa historia?

Sehemu ya barua ya Muhammad ilisema hivi:

"Kwa jina la Allah, Mwingi wa Neema, Mwenye Kurehemu! Barua hii ni kutoka kwa Muhammad, Mtumwa wa Allah na Mtume wake, kwako Heraklio, Mtawala wa Bizentini. Amani iwe kwake yeye afuataye Njia Iliyonyoka. Zaidi ya yote, Nakualika kwenye Uislamu na Ukisilimu basi utaishi kwa amani na usalama, na Allah atakuongezea mara mbili. Kama ukikataa wito huu wa Uislamu utakuwa umetenda dhambi na unawapotosha wafuasi wako. Na ninakariri hapa kauli ya Allah..." Muhammad ananukuu Sura 3:64

Barua tatu zimesalimika hadi hii leo unaweza kufanya utafiti wapi utazipata.

Nilichosema na ninaendelea kusema ni kuwa Rais wa Iran ametoa mwaliko kwa barua hiyo na hiyo si tafsiri yangu bali yeye mwenyewe kasema hivyo Jakarta alipohojiwa na waandishi wa habari. Kama kitendo hiko ni sawa au la hilo ni swali kwenu. Tunaweza kuzungumza mambo ya dini kwa heshima kwa hoja na bila husuda. Kama watu wanaongozwa na vionjo na ni vigumu kwao kutumia mantiki na ushahidi wa kihistoria kuzungumzia hata yale tusiyotaka kuzungumzia basi watu hao wamefilisika. Siasa ni Imani na Dini ni Imani!!
 
Unajua ingia andika ya kwako na msimamo wako, hakuna anayeleta dini hapa wajumbe wanachangia kutokana na ujuaji wao wa issue, kuna anayeiona issue moja kutoka upande wa mtume na mwingine anaoina issue hiyo hiyo kutoka kwa yesu,

hii forum ninataka kuamini kuwa ni huru maana naona kuna wachangiaji fulani wanataka kuwa viranja waku-control wengine waandike nini na waandikeje, hakuna mtoto mdogo hapa wa kuambiwa namna ya kuandika wote ni watu wazima tunaozidi miaka 13 kama tulivyosaini wakati wa ku-register, halafu issue ya watoto inaweza kuwa muhimu kwako ikawa nonesense kwangu, it does not mean anything zaidi ya kwamba priority zangu na zako hazifanani, that is all!

Hapa tunamjadili a bully, naye ni rais wa Iran ambaye inaonekana haelewi anachokifanya, kwa sababu dunia nzima inaelewa nguvu za US yeye haelewi, na at this point and time US haijaichokoza Iran isipokuwa na huyu rais wa Iran ndiye the bully here, halafu ni lazima tuongee international politics na za nyumbani pia at the same level bila ya kutishiwa na baadhi yetu ambao wanaonekana kutojua siasa kabisaaaa!

Mheshimiwa rais Jakaya Kikwete, anaweza kufuta maktaba wowote ule ambao sio muhimu kwa wananchi wake, yaani sisi wabongo, isipokuwa hawezi kudai Israel iondolewe kwenye ramani ya dunia ama sivyo atatengeneza bomu la kuifuta, that is insane na US ina haki zote za kujibu kikamailifu ikiwa ni pamoja na kutuadhibu, kutokana na uwezo wa nguvu zao, period! Should that happen, wananchi wote duniani watakuwa na haki ya kujadili the issue bila ya kutishwa what is right or what is wrong! au nani ana nguvu kuliko mwingine na aliyejua mapema, NONESENSE!

US waliwasaidia makaburu, kama USSR walivyomsaidia Idd Amin na sisi at the same time wakati wa vita vyetu, ambapo mpaka leo bado tunalilipia lile deni. Na sisi tungeweza kusadidiwa na US kama Kenya, lakini tukaichagua Urusi, so what? Sasa leo mbona tunasaidiwa na US? Kwanini tusiseme kuwa US iliwasaidia makaburu zamani kwa hiyo hatuwataki? Balozi wa US Smith ametufanyia mangapi bongo? Leo rais wako yuko NY, keshokutwa atakuwa Boston kwenye shughuli ambazo ziliwekwa chini na Smith, sasa how do you explin that na siasa zako za kukumbuka zamani? Waarabu waliotufanya watumwa wanafanya nini hapa bongo kwa siasa kama zako? Salim aliwezaje kuwa PM, yaani ulikuwa wapi kupinga kutokana na tuliyofanyiwa zaman na watu kama Salim yaani waarabu? Wajerumani si ndio waliomuua Mkwawa tena bila sababu, je leo tunafanya nini nao hapa bongo?

Wachangiaji ni lazima waongee wanyofikiri, tena bila ya kufikiri mara mbili au kutihwa asiyetaka akae pembeni asubiri issue zinazomhusu, we are grown men hapa hakuna mtoto wa kukumbushwa cha kuandika au cha kusema, siasa zote ni siasa ziwe za nje au za ndani zote ni siasa for God's sake! I mean kumbe kina Mahita mko mpaka huku, yaani hii inanikumbusha yule mtu aliyekuwa anatumwa na Mahita kule BCS, PLEASE! Tuache utoto, na hakuna anyekimbia wala kuondoka na this I see getting very interesting, kwani hapa inaonekana kuna kazi ya kuwafundiusha wananchi wenzetu kuwa leo ni 2006, sio 1961.

Wachangiaji watoe michango yao hata kama itwaingiza kina Mtume na Yesu, it ok asiyetaka anajua mlango ulipo, full stop!
 
Mzee Bob Mkandara na Mzee Mwanakijiji,

This is exactly what we need, malumbano! Great contributions guys na keep it up, yaani wote na wengineo, in the process wenye akili watapata msimamo wa kinachoongelewa au authority!

And God bless you guys!
 
Mzee mwanakijiji,

Sina haja ya heshima yako kama mimi nitakuwa nimepotea mwelekeo na kutoelewa maana. Kiswahili ni lugha yetu sote.
Umeandika hivi:-
Sijui kwanini tunazunguka zunguka na hatutaki kukiita "kijiko kijiko"? Barua aliyoandika huyu Rais wa Iran inanikumbusha barua ambayo Mtume alizituma kwa nchi zisizokuwa za Kiislamu na kuwataka wawe tayari kusilimu ama sivyo watakiona cha mtema kuni

Kwa maana hiyo hapo juu niliyoipigia mstari siioni mahala popote ktk hiyo invitation yako kuwa mtume kasema AMA SIVYO MTAKIONA CHA MTEMA KUNI.
Mzee mwakijiji maneno uliyozungumza hapo juu hayana tofauti na hayo aliyosema huyo mwendawazimu huko Malaysia hivi majuzi ktk mkutano wao waarabu. Na kwa vile wewe umeyanukuu na kulinganisha na maneno ya Mtume wetu nadhani sioni tofauti kabisa kati yenu.
Kwa taarifa yako naifahamu dini yangu na hiyo barua unayongumzia haikuwa kama unavyodai ila ni AYA za Kuran ambazo zilitumika kwa mwaliko huo. Kama wanavyokuja hao walokole Bongo hawana bunduki wala hawamshiki mtu koo ila neno la Mungu na wanasema Usipomkubali Yesu basi utaangamia, hapa hawana maana hao walokole watamwita Bush kutuangamiza.... wanachozungumzia ni life after!
Anyway, sura zilizotumika ni hizi hapa na utangulizi wa huo mwaliko ulikuwa Surah al araf 7:158, isemayo O' mankind! Certainly I have come to you all as the Messenger of God.
* We have sent you as a bearer of glad tidings and a warner to the entire mankind but most people do not know - Sura saba 34:28.
* The Qur'an is nothing but a reminder from God to mankind -Suah al Qalam 68:28.
* No religion other than Islam will be accepted from anyone. Whoever follows a religion other than Islam will be loser in the Hereafter. (Surah Ale Imran 3:85).
*The Qur'an has been revealed to warn to those who are living and the words of Allah may be fulfilled against the unbelievers. (Surah Yasin 36:70).
* It is Allah Who has sent His Messenger with guidance and a true religion that will prevail over all other religions though the polytheists may be averse. (Surah Tawbah 9: 33).
Na kati ya watawala wote walioalikwa nusu yao hawakufuata Uislaam na hapakutokea vita ktk nchi zao hadi leo. Pengine nisema Mfalme wa Abesinia yeye alikuwa Mkristu hadi siku yake ya kufa na alikuwa rafiki mkubwa wa Mtume pia aliwasaidia sana waislaam ambao walikuwa wakipigana na Makoreish! Wakati hali adui wa waislaam walikuwa waarabu. Huo Ulikuwa mwaliko na huyu mjomba hatoi mwaliko kwa Marekani ila kuonyesha yeye ngangari! - Hatikisiki.

Mzee ES,
Narudi kwako tuachane na habari hii ya dini, kifupi nitarudi nyuma kidogo baada ya huyu mshirika kuleta zake za kuleta. Kuna statement moja umekosea...Pale uliposema:- Kuichukia US ni one thing na kuuliza uhalali wa nchi nyingine kuwepo duniani ni another story of itself, now should we go back kufuatilia mipaka ya nchi zetu kabla ya wakoloni kuja, then tutakua na a big problem hasa Africa!

Umesahau kwamba Rhodesia ilikuwa nchi na waafrika tulihakikisha imeondoka ktk ramani!... India wamehakikisha Bombay imeondoka ktk ramani na Wachina wameondoa kasumba za Muingereza ktk mji wao wa Beijin ambo zamani ulikuwa ukijulikana kama Peking. Pia Ivory Coast kuwa kasumba ya Kifaransa badala ya Muingereza. zaire na Mobutu n.k
Hii ndio maana kamili ya kuondoa uhalali wa nchi na sio kama unavyofikiria wewe. nadhani hata sisi TZ tunatakiwa kuondoa kabisa kasumba za kiarabu na kuuita mji wetu Dar- Bongo ama Mwambao. Jina ambalo linatafsirika ktk lugha yetu na kutafsiri utajiri wetu kwa lugha yetu.
Mwisho mshikaji naona umekamatwa ktk lindi la siasa za magharibi. Huyu Iran hakuwa namatatizo kabisa na USA hadi pale alipotangaza kuwa EURO ndiyo itakayotumika kununua mafuta yake. hiyo Nuklia kama kujengwa imeanza lini? na nani walokuwa wakijenga kama sio nchi hizo hizo za magharibi. je, sikuya kwanza kukubali mkataba wa ujenzi watu hawa hawakufahamu kwamba hawa jamaa ni waislaam tena wenye siasa kali chini ya hao Ma - Ayatollah. Think braza think! wewe kweli kama sii wazimu wa hao wazungu wenyewe ni kitu gani kuanzisha mradi wa nuklia Iran hali mkijua kwamba hawa sii watu wa kuaminika, tena kukubali kuweka saini...Sasa huyu jamaa anachokumbatia ni mkataba wa kuweza kutengeneza nuklia kwa matumizi ya nyumbani na hakuna sheria yeyote inayomkataza kwani hatua za mwanzo za mkataba wa nuklia hajazivunja bado.
 
Mzee Bob,

US walienda Iraq, kwa sababu siku moja yule mwendawazimu mwingine aliropoka kuwa ana bomu, na nitalitumia wakati wowote over Israel tena ninaikumbuka vizuri sana siku aliposema nilikuwa bado US ninasoma bro! Toka siku ile US hawakulala mpaka walipomvamia,

Leo mwenda wazimu mwingine tena anasema kuwa antengeneza bomu na yuko karibu kuwa nalo, na ikibidi atalitumia kuifuta Israel kwenye ramani, US tayari imeshaanza kukosa usingizi,

Now India na Pakistani wana hilo hilo bomu na US haijawafanya kitu au kuwatisha, WHY? ni kwa sababu hawajamtishia mtu au nchi yoyote duniani kuwa wataifuta kwenye ramani kwa kutumia bomu hilo,

Je rais wa Iran alimaanisha kuwa ataibadili jina Israeli kama Rodhesia, Congo Kinshasa, au Ivory Coast, kwa kutumia bomu? Sidhani kama tungekuwa na hii debate au amerika ingekuwa inahangaika nao,

I refuse kumuweka huyu mu-Iran katika itikadi zozote za siasa duniani kwani he does not fit in anywhere, US siku zote wana agenda zao za kisiri siri ndio maana walipopigwa bomu tu Sept/11 baada ya siku tatu tu Congress ikaja na sheria za Patriotic Act za kurasa 300! I mean it is simple and clear kuwa walikuwa nazo hizo page 300 somewhere ila walikuwa wanasubiri tu siku itokee!,

Sasa whether we like it or not, US wana beef na Iran toka Shah alipotolewa na kina Khomein, sasa leo anatokea mwenda wazimu wa kusema ataitoa Israel kwenye ramani, hivi hufikiri kuwa US siku hiyo walifanya party!, kule White House kuwa finally, wana probable cause ya kuishambulia Iran, it is only a matter of time sasa hivi,

I mean two wrongs do not make it right, na regardless of the politics za unafiki za West na the rest, hapa kuna ma-bully wawili mmoja mdogo Iran na mwingine mkubwa US, at the end atakayepigwa ni bully mdogo kwa sababu ours ni dunia ya the fittest! Halafu bully mkubwa atamkamata huyu mu-Iran na kumpeleka the Hague kwenye tribunal ambayo yeye sio mwanachama,

In the perfect world, it wrong lakini in the World we live now ni possible kutokea Iran itengeneze bomu bila kelele, at this point ninaamini kuwa hawana hilo bomu kwani Israel wangeshalichukua siku nyingi na ninaamini kuwa US wanajua kuwa hana hilo bomu, lakini kwa sababu ameingia mwenyewe kwenye agenda yao hawatamuacha, that is my thinking kutokana na the experience ya Us na Panama, Grenada, Iraq, Vietnam, na Afaghanstan, I could be wrong sio a perfect world!
 
Mzee ES,

Mshikaji hapa unaongea maneno ya maana sana lakini kidogo unachanganya vitu. Iraq au niseme Saadam hakuwahi kusema anatengeneza Bomu la nuklia kuiondoa Israel. Bali uzushi wa Bush mwenyewe baada ya Iraq pia kutangaza kuwa itanunua mafuta yake kwa euro na kikubwa zaidi kuwa Saadam alimkosakosa baba yake Mzee Bush baada ya vita ya kwanza. Vita ya kwanza ilitokea baada ya saadam kuivamia Kuwait... hapa hakuna Bomu wala mjomba wake bomu. Kumbuka zile missile zote alizokuwa nazo Saadam waliziteketeza Marekani kwa kupitia UN...baada ya kuwekea vikwazo vilivyoshindikana kuondoa nia yake ya kutumia Euro. Unakumbuka Marekani walidai Iraq inajeshi kubwa la watu millioni 3 na sijui mabomu ya ajabuajabu ndege sijui 300. Jamani ziko wapi hizo silaha na majeshi mbona tunaona silaha za kirusi tena za miaka ileee ya ukombozi 1960s. Na mbona miaka imepita hatujaona hata ndege ya maana ach kifaru maanake vile tulivyoona wakati wa Kuwait kidogo vilitupa hope kwamba anaweza kuwa navyo.
Leo hii Iraq ipo miaka hamsini nyuma hata Zimbabwe wana afadhali.
Huyu mwendawazimu wa Iran kusema kweli ni mbabaishaji tu, yeye kama Korea ya kaskazini kasema ikiwa Marekani wataishambulia Iran basi mtu wa kwanza kuumia ni Israel. Korea walidai kuiangamiza tena kwa maneno yake kuididimiza Japan na sijasikia mtu akitukana na kutangaza vita zaidi ya makubaliano wala kusema hiyo ni imani ya Ki -Budhaa!.
Mjomba waarabu wote na nitarudia kusema waarabu wote wanaamini kabisa kuondoka kwa Israel kama taifa. Labda pitia upya historia ya Israel hii tunayoizungumzia kama nchi. Acha kuweka watu wake ktk mkondo huohuo. Yes ni kweli kabisa tuliondoa Rhodesia kwa sababu ilikuwa serikali ya Mkoloni muingereza ambayo iliwakandamiza weusi, lakini haina maana tuliuwa wazungu wote na vibaraka wake. Leo hii kama kutakuwepo na serikali Israel ambayo inawakubali wananchi wa nchi hiyo bila tofauti za kabila na dini sidhani kama hili swala la Palestina linaweza kuwa na sauti. Matatizo tunayopata sisi kutokana na vita ya Kongo, tunatakliwa kwa kila hali kumlaani M7 na hata kusema tutahakikisha utawala wa Kabila unatokomea kama tulivyomuondoa Idd Amin.
Nachoamini mimi hakuna nchi yeyote inayoweza kuondoa utawala wa Israel leo hii. Sii wayahudi wenyewe wala Marekani kwa sababu nyingi na za kimsingi. Ebu nambie leo hii mafuta yamepanda bei dunia nzima tunalia na waarabu. Waarabu wenyewe hawana kitu kwani mafuta yanachimbwa na mashirika ya magharibi sio waarabu. bei zinapandishwa na mashirika hayo kutokana na risk kuongezeka, insurance imepanda, bei za zana za uchimbaji zimepanda na hata nauli zameli kusafirisha mafuta hayo zimepanda yote kutokana na hali mbaya ya kisiasa nchi za mashariki ya kati. Nani kaingiza mkono kuleta hiyo risk - Marekani na sio Wayahudi au Israel. Why? waarabu wanataka kumtupa nje baada ya nchi kibao kusaini mikataba na China, Urusi na Ujerumani badala Marekani na Uingereza. Watu kibao hawaelewi Blair anaingia vipi ktk deal hili zaidi ya kufikiri ati terrorists!
Mwarabu anakatiwa kidogo sawa na sisi nchi za kiafrika ktk madini hana sauti isipokuwa Wachumi wakuu wa nchi za magharibi kwa kutumia media wanahakikisha lawama zote zinamfuata mnyonge. leo hii bei ya dhahabu ni kubwa kuliko wakati wowote ule hali kuna ongezeko kubwa sana la uzalishaji. WHY? ikiwa kweli supply imeongezeka kwa nini bei pia ipande? na ajabu kubwa kuliko yote dhahabu ya Tanzania inaonyesha kuwa na risk kubwa sana kisiasa hivyo insurance yake ni kubwa kishenzi. kweli kuna ukweli hapa?.. Jamani tusiwe tunabebwa kama gari bovu. hawa Wamarekani hawana elimu na wanakubali kila linalosemwa ktk CNN.
Kuitetea Marekani na siasa zake na kuhalalisha hatua wanazotishia ni kukubali mashirika makubwa kuendelea ukoloni mamboleo. Na baya kuliko yote ni kwamba hata kichaa anayaona mabaya ya siasa ya Marekani hali wenye akili timamu tunakumbatia, sasa sijui kati yetu nani hasa mwendawazimu. Samahani huu msemo tu msije fikiri natukana.
 
Mzee Bob,

Mwenye nguvu hupishwa apite, kumkumbatia na kutomkumbatia haibadili kitu chochote, tutasema maneno mengi lakini mwisho tutasubiri IMF na World bank za US zitusaidie,

Bei ya mafuta ni uizi tu wa US si juzi nimesikia CEO wa kampuni moja ya US ya mafuta ame-retire na kiinua mgongo cha $ 365,000,000! mpaka Congress wamepiga kelele,

Tuache siasa zilizopitwa na wakati za kufukuza mwenda wazimu tukiwa uchi, tunawahitaji US at the end of the day hatuna ubavu!
 
Mkandara,

Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kutuma ujumbe wake wa kuwaalika viongozi hao kuiingia na kuupokea Uislamu, nini kiliwapata wale waliokataa? Sina haja ya mjadala wa dini hapa, kwani siyo lengo langu. Nilichokisema ni kuwa barua ya rais wa Iran (ukichaa au siyo ukichaa) ilikuwa inafuata nyayo za mwaliko huo wa kuingia uislamu. Nataka ukanushe haya:

a. Muislamu yuko huru zaidi kutimiza matakwa ya dini yake hasa akiishi katika nchi ya Kiislamu.

b. Mahali ambapo Waislamu siyo wengi na hivyo hawawezi kujenga Taifa la Kiislamu basi hawana budi kuishi na watu wa dini nyingine na kufuata sheria za nchi husika.

c. Pale Waislamu wanapokuwa wengi na wenye uwezo wa kuunda Taifa la Kiislamu, ni bora kufanya hivyo ili waweze kutekeleza (a) hapo juu.

d. Endapo, Uislamu unapingwa au unazuiwa kuenea basi ni jukumu la Waislamu wote kuitetea dini ya Mwenyezi Mungu, hata ikibidi kwa vita.

e. Dini ya kweli na ya Mwisho ni ya Uislamu, na Muhammad ndiye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na watu wote wanaitwa kuwa Waislamu kwani dini nyingine/vitabu vingine vimeharibiwa!
 
Mzee mwanakijiji,
Maneno yako dhahiri yanazidi kukuacha Uchi kama MLOKOLE na sina muda wa kuzungumza dini na matokeo ya mitume. Mimi namwabudu Mungu peke yake, huyo Muhammad labda anawaumiza roho wengine hao akina Ayatollah kwani ni binadamu kama alivyokuwa Ibraham, Moses, Yesu na wengineo. Biblia Kuran na vitabu vingine vyote ni ELIMU kwangu, sio maisha na matukio ya Muhammad wala Yesu.
Yesu alijitoa mhanga kutuambia yale ambayo hakutakiwa kutuambia! INJILI -Ufalme wa Mungu na sio alijitoa mhanga kufa msalabani. Hii ni imani yangu mimi na sii lazima waislaam waamini hivyo wala wakristu. Imani hii imenifundisha mimi kwamba kama kuna neno la haki na litamwokoa mtu mwingine kwa gharama ya maisha yangu basi nipo radhi kuyasema maneno hayo! Sacrifice of Jesus is the Word of God reaching us not dying on the cross! kama wewe unaamini tofauti basi hilo juu yako na Mungu wako. Sintakunywa damu wala kula mkate wa kigiriki kwa mfano wa Yesu, ila nitafuata mafundisho yaliyosababisha hukumu yake.
Hao wote mitume ni binadamu walikunya na kuchekea chooni kama sisi.
Kifupi wakati wa mtume Muhammad hakuna vita iliyopiganwa nje ya Saudi Arabia na vita vyote vilikuwa kati ya Waislaam yaani waumini na wale wasioamini - Koo za kifalme za waarabu ambao kati yao kulikuwepo waliokuwa na imani ya Kiyahudi.. Judaism. hakuna hata vita moja iliyopiganwa kati ya waislaam na wakristu ama nje ktk nchi nyinginezo. Kushambuliwa na kujihami ni tofauti kabisa na kushambulia wasioamini.
Mzee ES,
Hapa sasa unazungumza - mwenye nguvu mpishe! hiyo ni statement inayofunga kazi na kuna wakati huwa nafikiri hata sisi hapa tunapoteza muda wetu ikiwa malengo ya mijadala kama hii sio kuelimishana. hakuna kati yetu anayeweza kuibadilisha CCM wala kuitetemesha mwisho wa yote ni SEGEREA!...kama wanavyojazana hao machizi wa kiarabu huko Guantamo bay. lakini kama kweli sisi sote waumini kwa njia moja ama nyingine hatima ya hawa wote ipo. Hakuna taifa ama utawala ulitikisha dunia nzima kama wa Roman Empire, Marekani msenge tu na uliondoka!..Je, tuache kusema na kuwafahamisha wengine mabaya ya huyu Marekani?.. kwa sababu ana nguvu.. nadhani hapa inategemea na malengo ya Mjadala huu.
Na hata wakija shindwa Marekanni hawa wanyonge wote watabaki wanyonge na mwenye nguvu mwingine ataibuka na amini maneno yangu sii muda mrefu na pengine generation hii tunaweza kuwepo duniani bado - CHINA is the next super power! ....Pretty soon.
 
Mkandara said:
...Sacrifice of Jesus is the Word of God reaching us not dying on the cross! kama wewe unaamini tofauti basi hilo juu yako na Mungu wako. Sintakunywa damu wala kula mkate wa kigiriki kwa mfano wa Yesu, ila nitafuata mafundisho yaliyosababisha hukumu yake.
Hao wote mitume ni binadamu walikunya na kuchekea chooni kama sisi.
Kifupi wakati wa mtume Muhammad hakuna vita iliyopiganwa nje ya Saudi Arabia na vita vyote vilikuwa kati ya Waislaam yaani waumini na wale wasioamini - Koo za kifalme za waarabu ambao kati yao kulikuwepo waliokuwa na imani ya Kiyahudi.. Judaism. hakuna hata vita moja iliyopiganwa kati ya waislaam na wakristu ama nje ktk nchi nyinginezo. Kushambuliwa na kujihami ni tofauti kabisa na kushambulia wasioamini.

Mkandara... unaweza kuchagua kuamini kuwa dawa ya sumu ya panya ni maziwa!!! Hiyo ni hiari yako. Wewe kuamini kwa nguvu zako zote hilo halisababisha maziwa kugeuka sumu!! Unaweza kuamini kuwa Yesu hakufa msalabani kwa ajili ya dhambi za watu au hakuwa mwana wa Mungu, sawa!! lakini hilo haliondoi ukweli. Kama Yesu alikuwa mwana wa Mungu na alikufa msalabani wewe kuamini vingine kunaathiri vipi ukweli huo.?

Haitoshi kuamini tu, bali pia inabidi uamini kilichokweli, siyo ukweli according to Mkandara!! for the truth is one!!! Siyo lengo kuzungumzia masuala ya imani (of which I'm very competent) lakini hapa tulikuwa tunazungumzia siasa!! Tukubaliane tu kuwa huyo Rais wa Irani ni Mchizi!!! Zaidi ya hapo tuanzishe mjadala mwingine wa kidini!!! usio na jazba au matusi!!
 
Mzee ES,
Unajua mshikaji mimi nimeandika yote yale ktk hoja yangu ya nyuma kwa madhumuni maalum. Jamaa yangu kaupanda mkenge, na vigumu kama mtu hukutumia busara kuelewa nilichoandika. Itabidi nimrudishe darasani.
Mzee mwanakijiji,
Hapo nyuma sikusema Yesu hakufa msalabani?.. soma tena vizurri na utaona hapa tunapishana kuelewa tafsiri ya neno kujitoa Mhanga.

Nachosema mimi Mhanga wa Yesu, sio hukumu aliyopata Yesu - kufa msalabani, ila mhanga wake Yesu ni kosa kama utataka kuliita kosa - alichofanya Yesu na kusababisha hukumu hiyo...
KOSA la YESU ama kwa lugha yangu kujitoa mhanga kwa YESU, ni kutuletea INJILI -neno la Mungu yaani ELIMU ambayo ni pingamizi na mafundisho ya utawala wa dunia ndiko kulikosababisha Yesu akamatwe. Kama asingefundisha Injili - neno la Mungu basi Yesu alikuwa salama na angepeta mitaani kama watu wengine hali elimu ile ingekuwa imepotea na binadamu wote tumepotea. Lakini hakutaka kutuacha watupu na kuendelea kubeba mzigo wa madhambi. Kwa hiyo basi alimua kujitoa muhanga kutufundisha IJNILI hali akijua kwamba hukumu yake ni kifo (kwa electric chair ya wakati huo)... Huu ndio Mhanga wa Yesu na sote leo TUTAOKOKA kama tutafuata mafundisho hayo......siamini kabisa kuwa nikila mkate wa kigiriki na kunywa wine ati mfano wa damu (damn) basi mimi poa kabisa Yesu kisha beba madhambi yote!.. Then why tunafundisha na kusisitiza dini ama kuamini kufanya yaliyo mema na kuepuka mabaya hali Yesu kesha chukua madhambi yetu....
Nooo way naamini Yesu kachukua risk ili mimi kuelewa na kutenganisha kati ya mabaya na mazuri. Elimu ambayo nikiisoma na kuyafuata basi pepo yangu.
Sasa kama wewe dini yako ama imani yako ni kuamini kwamba mhanga wa Yesu ni pale alipokufa msalabani na kuacha sababu iliyomhukumu hilo lako.
Narudi ktk mjadala wetu. Mimi huyu mshirika wa Iran sina haja ya kufahamu kama ni mtu mzuri, shetani ama mwendawazimu ila nimeangalia mafundisho yake. Huyu mshenzi anajitoa mhanga kwa njia yake, kutupa ukweli wa Marekani na mabaya yake na yupo tayari kufa lakini sote tunaelewa nini kibaya. For that, only that namsifia mtu huyu na nitajaribu kuyaangalia mafundisho yake ktk maisha yangu. Tofauti na mtu mwingiine ambaye anaamini, na kumfuata Yesu au Ahmadinejad maisha na hatima yao kuwa mkondo wa imani zao badala ya message waliyotupa hawa watu..
Ukizielewa tofauti hizi za mtazamo kati yetu (mimi na wewe ama wengine)basi utakuwa umenipunguzia kazi kubwa!
 
Mkandara said:
Mzee ES,
Unajua mshikaji mimi nimeandika yote yale ktk hoja yangu ya nyuma kwa madhumuni maalum. Jamaa yangu kaupanda mkenge, na vigumu kama mtu hukutumia busara kuelewa nilichoandika. Itabidi nimrudishe darasani.

Mkandara, kama ulilonipa hapa chini ni darasa, basi miye elimu siitaki! Kama nilivyosema, unaweza kuweka label yako yoyote kwenye chupa lakina haitabadili kilichomo ndani ya chupa.

Mzee mwanakijiji,
Hapo nyuma sikusema Yesu hakufa msalabani?.. soma tena vizurri na utaona hapa tunapishana kuelewa tafsiri ya neno kujitoa Mhanga.

Nachosema mimi Mhanga wa Yesu, sio hukumu aliyopata Yesu - kufa msalabani, ila mhanga wake Yesu ni kosa kama utataka kuliita kosa - alichofanya Yesu na kusababisha hukumu hiyo...
KOSA la YESU ama kwa lugha yangu kujitoa mhanga kwa YESU, ni kutuletea INJILI -neno la Mungu yaani ELIMU ambayo ni pingamizi na mafundisho ya utawala wa dunia ndiko kulikosababisha Yesu akamatwe. Kama asingefundisha Injili - neno la Mungu basi Yesu alikuwa salama na angepeta mitaani kama watu wengine hali elimu ile ingekuwa imepotea na binadamu wote tumepotea.

Mkandara, kwa maelezo yako hapo inaonyesha ni jinsi gani hufahamu au hujapata maarifa ya kina juu ya elimu juu ya Kristo (Christology). Unachokisema wewe hakina msingi wa maandiko wala ushahidi wa kihistoria. Kwa sababu hiyo basi nitakusaidia kidogo kujibu swali "Kwanini Yesu Alikatamatwa na kuhukumiwa kifo"?

Jibu la swali hilo liko pande mbili (two fold) nalo ni maelezo ya kusulubiwa kama tukio la kihistoria na pili maelezo ya kusulubiwa kama sehemu ya mpango wa wokovu (tukio la Kimungu)

Kusulubiwa kama sehemu ya Historia.
Ukisoma maandiko utaona sababu zilizomfanya Yesu akamatwe na hatimaye ahukumiwe kifo kwa kuning'inizwa mtini. Kwa mujibu wa maandiko Yesu alishatikiwa kwa makosa yafuatayo.

a. Kudai yeye ni mwana wa Mungu (kosa kwa warumi na kwa wayahudi)
b. Kudai atalibomoa Hekalu na kulijenga kwa siku tatu (kosa kwa wayahudi)
c. Alikuwa anachochea uasi kwa mafundisho yake (kosa kwa warumi)
d. Alijidai yeye ni mfalme na hivyo anapingana na Kaisari (kosa kubwa kabisa - High Treason)

Hayo ndiyo mashtaka dhidi ya Yesu.

2. Kusulubiwa kama Sehemu ya Mpango wa wokovu.
Kama ukibahatika kujifunza elimu ya wokovu (soteriology) utaona kwamba Yesu hakujitoa mhanga ili tu kutetea mafundisho yake. Kifo chake hakikuwa mhanga, bali kilikuwa kafara yaani sadaka. Yesu alikufa ili kulipa deni la dhambi na ukisoma mafundisho ya Biblia utaliona hilo wazi. Yesu hakufa kwa bahati mbaya!!! Wakati Ibrahim alipokubali kumtoa mtoto wake Isaka kuwa sadaka, na alikuwa tayari kakiinua kisu kumchinja, Malaika wa Bwana akamtokea na kumwambia "Ibrahim weka chini kisu chako usimdhuru mtoto" Na akaelekezwa pembeni ambako Kondoo alikuwa amenaswa kwenye kichaka na akamchukua kondoo huyo kumtoa sadaka. Kwa kufanya hivyo Ibrahim aliingia deni na Mungu.

Ndipo Ibrahim akauita mlima ule "Yehova Yire" yaani "Bwana Atapata!". Ni katika Yesu ndo tunakuta Mungu akilipa deni, deni ambalo mwanadamu hakuwa na uwezo wa kulilipa. Yohana mbatizaji alipomuona Yesu ng'ambo ya mto Yordani alisema "Tazameni mwana kondoo wa Mungu aiondoaye dhambi ya dunia" Yeyote aliyesikia maneno hayo alielewa kondoo kama kafara! Na Yesu mwenyewe akizungumzia kifo chake alisema "Kama vile Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa bali kutumikia, na kutoa uhai wake kuwa fidia ya wengi" Matthayo 20:28

Lakini hakutaka kutuacha watupu na kuendelea kubeba mzigo wa madhambi. Kwa hiyo basi alimua kujitoa muhanga kutufundisha IJNILI hali akijua kwamba hukumu yake ni kifo (kwa electric chair ya wakati huo)... Huu ndio Mhanga wa Yesu na sote leo TUTAOKOKA kama tutafuata mafundisho hayo......siamini kabisa kuwa nikila mkate wa kigiriki na kunywa wine ati mfano wa damu (damn) basi mimi poa kabisa Yesu kisha beba madhambi yote!.. Then why tunafundisha na kusisitiza dini ama kuamini kufanya yaliyo mema na kuepuka mabaya hali Yesu kesha chukua madhambi yetu....

Yesu hakufa kujitoa mhanga (it was not a suicide mission)! Alikufa kutekeleza mpango wa wokovu uliohitaji malipo ya damu isiyo na doa, damu ya Mwana Kondoo wa Mungu!!!!

Nooo way naamini Yesu kachukua risk ili mimi kuelewa na kutenganisha kati ya mabaya na mazuri. Elimu ambayo nikiisoma na kuyafuata basi pepo yangu.
Sasa kama wewe dini yako ama imani yako ni kuamini kwamba mhanga wa Yesu ni pale alipokufa msalabani na kuacha sababu iliyomhukumu hilo lako.

Huwezi kuamini pasipo msingi, unaweza kuamini Yesu alikuwa Mchina!! Lakini ukweli ni kuwa ushahidi wote uliopo unasema alikuwa Myahudi!! Unaweza kuamini hiyo nadharia yako ya Mhanga. Kwa taarifa yako, nadharia hiyo haina msingi wa kiteolojia, kihistoria au kiukweli. Ni nadharia uliyojitungia ili kukuridhisha akili yako. Kwa hilo unayo haki. Hata hivyo, ni bora nadharia hiyo ubakie nayo wewe mwenyewe kwani ukiitoa hadharani watu watacheka.!!!


For that, only that namsifia mtu huyu na nitajaribu kuyaangalia mafundisho yake ktk maisha yangu. Tofauti na mtu mwingiine ambaye anaamini, na kumfuata Yesu au Ahmadinejad maisha na hatima yao kuwa mkondo wa imani zao badala ya message waliyotupa hawa watu..
Ukizielewa tofauti hizi za mtazamo kati yetu (mimi na wewe ama wengine)basi utakuwa umenipunguzia kazi kubwa!

Kama unamlinganisha Yesu na Ahmedinajad unafanya kosa kubwa. Kama nilivyosema Yesu hakujitoa Mhanga!! Usichague ni mafundisho gani ya Yesu ya kufuata!! Kama kweli Yesu amekupa fundisho la aina fulani basi angalia mafundisho yake yote. Ni yeye aliyesema, "Huu ni Mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu, kuleni kwa ukumbusho wangu, Hiki ni kikombe cha damu yangu itakayomwagika kwa ajili ya wengi kwa MAONDOLEO YA DHAMBI fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi" Usichague cha kuamini!! au usijitengenezee cha kuamini chochote kisicho na msingi wa maandiko, historia au mantiki!! Vinginevyo ni bora uwe mfuasi wa Bahaiullah!! (or something!)
 
Mzee mwakijiji,
ndugu yangu itakuwa kazi kubwa kunivuta mimi ktk imani yako. Nakuelewa na ndio maana nikatoa Mada ya Shujaa!... Kila mtu ana mtazamo wake ktk tafsiri ya neno.
Napenda sana Ukristu lakini sii kwa imani yako! napenda sana Uislaam lakini sii kwa tafsiri ya baadhi ya waislaaam. Mimi sii mwana zuoni aliyebobea ktk dini lakini nafuata Logic kwa sababu naamini Mungu alituumba na akili. Sote hata yule ambaye hajasikia neno la Mungu anafahamu baya na zuri kama ndama anavyofahamu chuchu za ziwa la mamake. Isipokuwa kutokana na vishawishi vya kidunia binadamu tomepotoka na ndipo mitume wameingia!...Naamini dini zimevumbuliwa (discovered)sio kwamba zimeumbwa (created). The principles are created by God and discovered by man.
Kwa hiyo hii ni Elimu kama vile hesabu, science n.k. tunavumbua tu yale yaliyokwisha kuwepo. na wazee wetu walijua kuua ni dhambi kabla hawajawasikia ama kusikia mafundisho ya Yesu wala Muhammad.

Maelezo yako yote hapo juu hayana nguvu ya hoja yangu kwako ila upotoshi wa maana yangu.
Kwa nini nasema hivi, ebu soma tena sentesi yangu ya mwisho hapo juu!
Inasema hivi:- Narudi ktk mjadala wetu. Mimi huyu mshirika wa Iran sina haja ya kufahamu kama ni mtu mzuri, shetani ama mwendawazimu ila nimeangalia mafundisho yake. Huyu mshenzi anajitoa mhanga kwa njia yake, kutupa ukweli wa Marekani na mabaya yake na yupo tayari kufa lakini sote tunaelewa nini kibaya. For that, only that namsifia mtu huyu na nitajaribu kuyaangalia mafundisho yake ktk maisha yangu. Tofauti na mtu mwingiine ambaye anaamini, na kumfuata Yesu au Ahmadinejad maisha na hatima yao kuwa mkondo wa imani zao badala ya message waliyotupa hawa watu.. Ukizielewa tofauti hizi za mtazamo kati yetu (mimi na wewe ama wengine)basi utakuwa umenipunguzia kazi kubwa!
labda niifanye rahisi kwako, Kuna makundi matatu hapa yenye tafsiri tatu tofauti za imani ya dini.
1. Mimi:- naamini kuwa message za mitume ndio important - not their life story!... Hii ni elimu kama navyoamini watunzi ama wavumbuzi wa hesabu na sayansi bila kujali maisha ya wasomi waandishi.
2. Wewe:- Unaamini maisha ya mtu kuwa ndio kielelezo cha elimu na principal.. Kama Yesu angekuwa mlevi ama hakusulubiwa basi usingeamini kabisa message yake..
3. Kundi la tatu ni sawa na lako, isipokuwa hawa wako upande wa pili. Hawa pia wanafuata maisha ya Ossama, Ahmadnejad, Bush na wengineo kwa sababu message zao zimevutia mapenzi yao ya imani. wapo radhi kufanya lolote kwa sababu ya imani namapenzi hayo.
kwa hiyo basi tofauti kati yangu na makundi haya mawili ni kwamba siamini wala kumfuata mtu kuwa na Uuungu fulani ama ukaribu fulani na Mungu, hawa wote ni binadamu wanaokula na kunya...na wote wanamwomba Mungu kwa usawa na mimi, isipokuwa wamejaliwa kupata ELIMU fulani ambayo mimi sina. Na ikiwa Elimu hiyo ndio ukaribu na Mungu hapo nakubaliana na wewe lakini sio washikaji wa Mungu -HAWAJAMUONA.

Shukran na endelea kuamini unavyoamini. Umenichekesha sana uliposema Yesu alisema - Yehova Yire - bob mbona hii lugha Yesu hakuwa akiizungumza? au unafikiri ndio umeandika mojawapo Ki-Hebrew/Kitaliani?
Je, unafahamu kwamba jina la Yesu kwa Ki-hebrew cha zamani linatamkwa kama Yisa na sio Yesu wala Jesus?...
soma ndugu yangu soma dini ngumu sana!
 
Mkandara said:
Mzee mwakijiji,
ndugu yangu itakuwa kazi kubwa kunivuta mimi ktk imani yako. Nakuelewa na ndio maana nikatoa Mada ya Shujaa!... Kila mtu ana mtazamo wake ktk tafsiri ya neno.

Mkandara, siyo lengo langu kukuvuta kwenye imani yangu. Ila najaribu kukuweka sawa kuwa kuna imani moja tu katika Ukristu nayo ni ile ya mitume. Kutaka kuelewa ukristu unaamini nini hatuna budi kwenda mwanzoni toka kwa wale waliopokea mafundisho ya mitume.

labda niifanye rahisi kwako, Kuna makundi matatu hapa yenye tafsiri tatu tofauti za imani ya dini.

Hakuna urahisi wowote uliofanya hapa zaidi ya kujivingirisha wewe mwenyewe kwenye nyavu uliyoitandika mwenyewe.


1. Mimi:- naamini kuwa message za mitume ndio important - not their life story!... Hii ni elimu kama navyoamini watunzi ama wavumbuzi wa hesabu na sayansi bila kujali maisha ya wasomi waandishi.

Makosa mawili unayafanya hapa. Kwanza, huwezi kutenganisha mitume na maisha yao. Suala la mitume wa Mungu ni suala linalohusu maisha ya milele. Wao wanadai kuwa wamepewa ujumbe na Mwenyezi Mungu kuwafikia wanadamu. Hata hivyo ujumbe huo unaenda sambamba kabisa na maisha yao. Kosa la pili ni kulinganisha masuala ya imani na masomo ya elimu ya dunia. Ni kweli kama mtu anajua hesabu anaweza kuifundisha hata kama yeye ni muuaji, mbakaji au mlevi!! kwani 2 + 2 ni 4 hata kama anayefundisha ni jambazi!!! Kwenye masuala ya dini hata hivyo kuna tofauti kubwa. Mjumbe wa mwenyezi Mungu akija na kutuambia "Msiue" halafu yeye mwenyewe akaendelea kuua hatuwezi kumuamini!! Ndiposa, utaona kuwa huwezi hata chembe (hata kama utake vipi) kutengenisha maisha ya Yesu na Ujumbe wake! Kuzaliwa kwake, mafundisho yake, kifo chake na hatimaye kufufuka kwake ni sehemu nzima (part and parcel) ya ujumbe wake! Of course, unaweza kujaribu kufanya hivyo kwa "wajumbe" wengine, lakini kwa Yesu huwezi. Yeye hakuja kuleta tu neno la Mungu bali yeye mwenyewe alikuwa ndiye Neno! (yoh 1:1-12)


2. Wewe:- Unaamini maisha ya mtu kuwa ndio kielelezo cha elimu na principal.. Kama Yesu angekuwa mlevi ama hakusulubiwa basi usingeamini kabisa message yake..

Of couse nisingemuamini!! kama alisema kuwa atatoa uhai wake kwa ajili ya fidia ya dhambi halafu akakimbia asife nisingemuamini. Kama angesema kuwa "nitasulubiwa na kufa siku ya tatu nitafufuka" halafu akasulubiwa lakini baada ya siku tatu asingefufuka, nisingemuamini. Ujumbe wa Yesu siyo tu maneno yake tu bali pia maisha yake!!!

3. Kundi la tatu ni sawa na lako, isipokuwa hawa wako upande wa pili. Hawa pia wanafuata maisha ya Ossama, Ahmadnejad, Bush na wengineo kwa sababu message zao zimevutia mapenzi yao ya imani. wapo radhi kufanya lolote kwa sababu ya imani namapenzi hayo.

Wala siko kwenye kundi hilo. Mimi najaribu kumfuata Yesu siyo kama Kipofu bali nimeangalia maisha na ujumbe wake, hivyo viwili ni vivutio tosha. Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa kuna watu ambao wanaamini tu bila ya kuangalia ukweli wa kile wanachokiamini na kulinganisha na maisha ya yule wanayemuamini!!


kwa hiyo basi tofauti kati yangu na makundi haya mawili ni kwamba siamini wala kumfuata mtu kuwa na Uuungu fulani ama ukaribu fulani na Mungu, hawa wote ni binadamu wanaokula na kunya...na wote wanamwomba Mungu kwa usawa na mimi, isipokuwa wamejaliwa kupata ELIMU fulani ambayo mimi sina. Na ikiwa Elimu hiyo ndio ukaribu na Mungu hapo nakubaliana na wewe lakini sio washikaji wa Mungu -HAWAJAMUONA.

Unaona, unachokisema ni imani uliyojitengenezea wewe mwenyewe ili ikufae! Siyo imani ya Kikristu na wala haina msingi wa imani ya Kikristu. Unayo haki ya kuamini chochote unachotaka kuamini, lakini kwa kufanya hivyo usikiite kile unachokiamini ni imani katika Kristu. Kwani imani uliyotaja juu ya Kristu haina msingi wowote wa Kibiblia, Kihistoria au Kiteolojia. Ni imani uliyojichongea mwenye ili kukupa faraja na kutuliza akili yako!!


Shukran na endelea kuamini unavyoamini. Umenichekesha sana uliposema Yesu alisema - Yehova Yire - bob mbona hii lugha Yesu hakuwa akiizungumza? au unafikiri ndio umeandika mojawapo Ki-Hebrew/Kitaliani?

Sikusema Yesu alisema hivyo, nilisema Ibrahim alipaita pale kwa lugha hiyo ya kiebrania! Yesu alikuwa akizungumza kiaramaiki!

Je, unafahamu kwamba jina la Yesu kwa Ki-hebrew cha zamani linatamkwa kama Yisa na sio Yesu wala Jesus?...
soma ndugu yangu soma dini ngumu sana!

Not even close! Jina la Yesu kwa kiebrania ni Yeshua! ambacho ni kiini cha jina Yoshua! ambalo lina maanisha "Mungu anaokoa". Jina Issa halijawahi kutumika mahali popote hata waarabu wakristu wa Mashariki ya Kati hawajawahi kumuita Yesu Isa... !! Issa ni invention ya baadaye!! Ndo maana Yesu wa Biblia siye Issa wa Kurani!!!
 
Mwanakijiji na Mkandara,
Kubishana kuhusu dini ni suala ambalo litaleta chuki na hamtalimaliza! Always ni KUKU na YAI nani alianza! Jioneni kwanza ni Watanzania, halafu ni Waafrika, halafu ni wanadunia! Hata mashehe na mapadiri hawazozani. Hata mie ninavyoona mnavyotaka kutoona macho hapo juu nacheka tu!! Huu ndiyo utumwa tuliorithi! Sasa kama mkiona ile Da Vinci sijui hapo mtasema nini!!
Siku moja wewe jaribu kuingia Kanisa ambalo limejaa wazungu watupu, au msikiti ulijaa waarabu watupu; unajisikiaje??
Naamini mungu lakini sina muda wa kuhoji Yesu au Mohamad ndiyo perfect!
 
IO, hakuna kitu hatari kama kukubali hoja za mtu bila kuzijadili kwa kuogopa watu watakasirika. Huu ni moja ya udhaifu wetu kama waafrika na hasa kama Watanzania. Sijui kwa upande wa Kiislamu, lakini kwa Wakristu, Ukristu unazungumzika na wala hakuna kutoana ngeu. Majadiliano kati ya watu wenye imani na wasio na imani ni mojawapo ya uzuri wa mjadala wa kitaaluma na kisomi. Tazizo letu Tanzania kinachofanyika zaidi ni kashfa na siyo mijadala. Pia tunaogopa kuichunguza imani yetu kwa kina kwani tunaogopa kugundua mapungufu na hivyo kuweka imani yetu hatihati.

Mimi nilianza kama hivyo tangu nikiwa na miaka 17 kule Tanga na kwenye mijadala ya Mnazi mmoja mpaka ilipopigwa marufuku. Niliacha mijadala hiyo kwa sababu wakati huo sikujua jinsi ya kujadiliana kwa heshima, kujenga hoja, kuvunja hoja, na kukubali ukweli wa hoja fulani. Kwa kufanya hivyo tunajifunza kutetea siyo tu imani bali hoja nyingine. Mjadala unaoendelea hapa si wa matusi au kashfa. Kama nilivyosema hapo juu, sijawahi na wala sitawahi kuutukana Uislamu au dini nyingine kwani yote haya ni imani. Ninachojaribu kuonyesha ni kuwa sisi kama viumbe wenye akili na uwezo wa kufikiri (intelligent and rational beings) tunauwezo wa kuangalia hizi dini na mantiki iliyopo. Ukristu siyo dini ya weupe au weusi peke yake!! Ninapoingia katika kanisa lenye watu weupe wala sijisikii vibaya au wasiwasi kwani Ukristu ulifika Afrika kwanza kabla ya Ulaya!!!! Afrika ilitoa watetezi wengi wa imani kabla Europe haijatoa hata mmoja. Hivyo, hii ni dini yangu iliyoota, kukua na kukomaa tangu enzi na enzi katiba bara la Afrika. Ukristu ulikuwepo Afrika kabla ya Wazungu kuja!!!

Mimi binafsi sina hofu ya mtu yeyeote kusoma, kuujadilia au kujaribu kuonyesha mapungufu ya Ukristu kwani kwa kufanya hivyo wananifanya nijiulize kuhusu imani yangu, kama ninachoamini kina msingi au nimepotoka.

Hata hivyo kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine mazungumzo haya yanawaletea kikwazo ninatanguliza samahani zangu lakini nawashauri wafuatilia tu, na kama wanaswali (siyo kejeli) waulize, tukiwa na jibu tutajibu kama hatuna tutakiri!!!
 
Mimi niliposoma tu haya majibazano. Ninahisi kuna dini hapa!

Lakini mshikaji mmoja akaja na zake kuwa eti hakuna dini na nisitishe watu!!!!!!!!!!

Baada ya muda topic ikawa wazi! niliamua kukaa kimya!!
 
Mzee Bob na Mwanakijiji,

Great topic kwani sisi pagans tunafarijika na elimu hii ya dini ambayo no question kuwa ni high level, haya wanangu tuwekeeni vitu vya mbinguni tuamke na sisi,

It is ok guys, unajua vikikushinda vya dunia kuna wakati kuna haja ya kujua ambavyo hatujaviona, na wazee hawa wawili wanatuamsha wengine smahani kwa wale wanaodhani kuna vita, hapana hapa kuna maneno matamu ya kusafisha mioyo yetu, I mean sometimes we have to talk about God na tuwaachie wanaofahamu wasme kuliko kuwakatisha tamaa, ninaamini kuwa tuko wengi hapa tunaojifunza dini kwenye hii topic,

Mzee Bob na Mwanakijiji BRAVO! Hii ndio Demokrasia yenyewe at work!
 
Back
Top Bottom