Rais wa FIFA awapa makavu wazungu dhidi ya Afrika

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,174
2,278
RAIS WA FIFA GIAN INFANTINO.

Rais wa FIFA Gian Infantino ameibuka leo na kutoa kauli yenye utata ikiwa imebaki siku moja kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Qatar.

Infantino ambaye ni raia wa Switzerland mwenye asili ya Italia amesema kuwa kwa mambo ambayo wazungu wamewafanyia waafrika kwa miaka 300 iliyopita hawatakiwi kuwafundisha chochote na badala yake wanatakiwa kuwaomba msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.

Katika hotuba yake ambayo imekosolewa vibaya na vyombo vya Habari vya mataifa ya Ulaya Infantino amesema akiwa Qatar ameonesha kuguswa na wakimbizi, watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja lakini pia anajiona mwafrika wakati huohuo anajiona mwarabu.

Infantino amesema raia wa Ulaya wanatakiwa kuwaomba msamaha waafrika na dunia kwa ujumla kwa miaka 300 ijayo
Infantino ameyasema hayo ikiwa ni katika jitihada zake za kutetea ufanyikaji wa Kombe la Dunia nchini Qatar jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikosolewa na wadau mbalimbali wa soka hasa wanaotoka mataifa ya Ulaya ambao wanaamini kuwa ilikuwa ni makosa kupeleka mashindano hayo nchini humo.

“Najua ni kivipi inamaanisha kunyanyasika na kutengwa, Mimi ni raia wa Ulaya na sit u kwamba najivunia kuwa raia wa Ulaya lakini hakika mimi ni raia wa Ulaya, Nadhani kwa kipindi cha miaka 300 mambo tuliyofanya Afrika na duniani kote kwa ujumla tunatakiwa tuombe msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.” amesema Infantino.

# Hawa ndio wazungu wanaojielewa sasa. Wote wangekuwa km huyu Africa tusingekuwa tunaomba misaada ulaya.
 
RAIS WA FIFA GIAN INFANTINO.

RAIS wa FIFA Gian Infantino ameibuka leo na kutoa kauli yenye utata ikiwa imebaki siku moja kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Qatar.

Infantino ambaye ni raia wa Switzerland mwenye asili ya Italia amesema kuwa kwa mambo ambayo wazungu wamewafanyia waafrika kwa miaka 300 iliyopita hawatakiwi kuwafundisha chochote na badala yake wanatakiwa kuwaomba msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.

Katika hotuba yake ambayo imekosolewa vibaya na vyombo vya Habari vya mataifa ya Ulaya Infantino amesema akiwa Qatar ameonesha kuguswa na wakimbizi, watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja lakini pia anajiona mwafrika wakati huohuo anajiona mwarabu.

Infantino amesema raia wa Ulaya wanatakiwa kuwaomba msamaha waafrika na dunia kwa ujumla kwa miaka 300 ijayo
Infantiono ameyasema hayo ikiwa ni katika jitihada zake za kutetea ufanyikaji wa Kombe la Dunia nchini Qatar jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikosolewa na wadau mbalimbali wa soka hasa wanaotoka mataifa ya Ulaya ambao wanaamini kuwa ilikuwa ni makosa kupeleka mashindano hayo nchini humo.

“Najua ni kivipi inamaanisha kunyanyasika na kutengwa, Mimi ni raia wa Ulaya na sit u kwamba najivunia kuwa raia wa Ulaya lakini hakika mimi ni raia wa Ulaya, Nadhani kwa kipindi cha miaka 300 mambo tuliyofanya Afrika na duniani kote kwa ujumla tunatakiwa tuombe msamaha kwa miaka mingine 300 ijayo.” amesema Infantino.

# Hawa ndio wazungu wanaojielewa sasa. Wote wangekuwa km huyu Africa tusingekuwa tunaomba misaada ulaya.
Don't get deceived.

#MaendeleoHayanaChama
 
Masharti yaliyowekwa na qatar kwenye haya mashindano ni kama watu wako kwny bumbuwazi jamaa kaongea hiv kama kuleta hamasa mashindano yakipita wanarudi kulekule
 
Likitoka Qatar kombe la dunia lijalo linaenda dubai likitoka hapo linaenda saudi arabia hapo tutakuwa tumenguza mashoga kidogo na walevi maana wale wengine hii vita wameshaishindwa tayari wapo dilema ngoja waarabu watusaidia kuondoa nuksi.
 
Waafrika hovyo tu na tunasingizia wazungu kwa u hovyo wetu. Mwafrika ni mbinafsi na anajali tumbo lake tu. Ufisadi mnafanya wenyewe kwa ubinafsi na faida ya matumbo ya kikundi cha watu halafu umasikini wa wananchi mnasingizia wazungu.
Kuna matendo ya ubinafsi makubwa kushinda yale ya kumfanya binadamu mwenzako Mtumwa? Au kuzidi ya Ukoloni?

Kuna mzungu yeyote anayekuja Afrika kufanya fair business!? Mikataba ya madini hamuioni!? Utakatifu wao uko wapi?

Mmepewa matusi ya kujitukana mjidharau na kujiona si kitu mbele za wazungu, nanyi mmeyakariri pasi kuruka hata neno na kuyahubiri kila mtaa.

Mnatuangusha!
 
Hakuna aliesema ukoloni ulikuwa mzuri. Ufisadi unaofanywa sasa unatokana na ukoloni wa miaka 61 nyuma? Mzungu anaweza kuingia nchi ya kiafrika na kufanya business isiyo fair bila kushirikiana na waafrika?
Kwani Mikataba ya hovyo wazungu wanasahinishana na nani kama sio baadhi ya waafrika?
 
Sasa issue ya Ukoloni wa Africa na kombe kufanyika kwa Waarabu kunahusiana nini?

Kwanini asingewaomba msamaha Waarabu kwa uharibifu walioufanya katika hizo Nchi bila kuihusisha Africa?

alichoongea ni indirect, wenyewe wazungu wamefahamu vizuri na ndio mana wanamwaga povu.

Kinachowatesa wazungu kombe la Dunia kufanyika Qatar ni wivu wa kibaguzi.
 
Hakuna aliesema ukoloni ulikuwa mzuri. Ufisadi unaofanywa sasa unatokana na ukoloni wa miaka 61 nyuma? Mzungu anaweza kuingia nchi ya kiafrika na kufanya business isiyo fair bila kushirikiana na waafrika?
Kwani Mikataba ya hovyo wazungu wanasahinishana na nani kama sio baadhi ya waafrika?
Unaposema Waafrika ni hovyo, labda inamaanisha kuna jamii isiyokuwa hivyo. Ndio maana nikahoji ni IPI?

Kama kuna inayotuzidi Ubinafsi kwanini tujilaani kwa maneno makali pasipo kujipa matumaini?

Je, tumeshawahi kutafakari athari za mtu kujidharau kila siku?

Hakuna mwenye akili timamu atakayesain mkataba wa kuua ndugu zake willingly, hayup popote duniani.
Hivyo wanaosainishwa mikataba ya hovyo ni hamnazo kichwani au amelazimishwa. Na kinachowatoa akili viongozi wetu ni Kasumba kama hii yako inayopandikizwa na wazungu kwa makusudi, kwamba sisi ni hovyo. Wapandikizaji ni hao tunaowaona kuwa smart na kutokuwa wabinafsi.

Chunga mtazamo wako, maana waweza kuwa unapalilia uovu unaouchukia. Hatuna sababu ya kujinenea kwa dharau kwanini haitusaidii zaidi ya kutudidimiza zaidi.

Kila la heri Mkuu!
 
Back
Top Bottom