Yoyo Zhou
Member
- Jun 16, 2020
- 72
- 111
Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba kwenye mkutano maalumu wa kilele kuhusu mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupambana na COVID-19.
Ameahidi kuwa mara chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na China itakapokamilika na kuthibitishwa, nchi za Afrika zitakuwa kati ya nchi za mwanzo kufaidika.
Pia ameongeza kuwa Ili kupunguza athari za COVID-19, ni muhimu kuongeza ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa matokeo ya mkutano wa FOCAC wa Beijing.
Kipaumbele kikubwa kinatakiwa kutolewa kwa ushirikiano katika afya ya umma, kufungua tena uchumi, na maisha ya watu.