VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,481
- 1,450
Rais Evariste Ndayishimiye amewanyoshea kidole raia wa Burundi wanaokwenda nje ya nchi kutafuta suluhu ya matatizo yao kana kwamba nchini kwao hakuna uongozi.Alisema: “Mrundi yeyote ambaye ana tatizo nchini na kwenda kutafuta suluhu nje ya nchi, Mrundi huyo hajui uhuru ni nini." Bila kusita, Rais Ndayishimiye aliwanyooshea vidole walioshindwa katika uchaguzi uliopita wa wabunge na wakuu wa wilaya kwa kugeukia Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kutafuta msaada. Mwishoni mwa juma lililopita, Wapinzani wa kisiasa walioikimbia Burundi waliungana pamoja wakisema kwamba wanaenda kupinga udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi uliopita.