Rais umekosea kuwakilishwa na Balozi kwenye mkutano wa EAC kuhusu Congo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Rais hapa kakosea na tumekuwa wazembe sana na wavivu kama nchi. Congo DRC ni sehemu muhimu sana lakini tumekuwa wazembe sana na tunawaachia nchi za nje wanatumia mbinu za kuwagombanisha ili tu wachukue madini. Tanzania kama nchi kubwa tulikuwa na uwezo mkubwa sana kuanzia enzi za kabila kuifanya Congo kuwa sehemu yenye usalama na kusaidia nchi yetu.

Kwenye mkutano wa Kenya, Tanzania imewakilishwa na balozi yaani hata Makamu wa Rais au waziri wa ulinzi ameshidwa kwenda. Ni aibu na ni Rais gani ataongea vitu vya siri kwa balozi? Tusishangae balozi wetu kuwekwa nje wakati wakiongea mambo muhimu.

Ni bora hata Rais Samia angetumia mtandao na sio hivi. Lakini kibaya tunaonekana dhaifu sana kwa Rais wa Congo kwasababu tu tunaogopa kumkasirisha Kagame kwa kupingana naye kwenye hili. Kikwete ndiye aliweza kumsema wazi wazi na Samia hapa kakosea na kuonyesha udhaifu mkubwa kwa majirani zetu.

Maslahi yenu siyo maslahi ya Tanzania, wacha maneno 'kamundu'.

Tanzania imeshiriki kwenye mambo makubwa zaidi ya kutafuta maslahi kama haya mnayoyatafuta sasa hivi.

Tulipokuwa tunavuja damu katika ukombozi, nyinyi mlikuwa mkinywa chai na wakoloni. Sasa ndio mmekumbuka umuhimu wa amani, wakati wachokozi ni hao hao rafiki zenu?

Achana na Tanzania bhwanah. Nilishakwambia, kama uliamua kuja hapa, basi jivue kabisa uhuni wa huko ulikotokea, lakini naona huelewi kitu chochote.

Najua utalalamika, lakini utajielewa mwenyewe ninachokwambia.
 
Na ni heri hakwenda huko congo,,,hilo linchi limejaza makatili wengi tu, tutampoteza mama yetu. Nchi zenye amani kama oman, emirates na kwa mzee puttin hata akienda no problem.
 
Tatizo la Congo DR ni la siku nyingi, nchi hii imekosa kiongozi wa kuiunganisha nchi hii kubwa ya DR Congo.

Historia inaonesha ina matatizo toka ipate uhuru, marais wanajifungia Kinshasa na wakijitahidi sana wanajiimarisha tawala zao ktk majimbo ya vijiji vya mababu zao tu majimbo mengine hawayachukulii kwa uzito kama yapo ndani ya taifa la DR Congo.

Mbaya zaidi kuna wadau wa kikanda na kimataifa wanaochochea hali hii ya DR Congo isitawalike kama nchi moja ili waendelee kuchimba na kupora rasilimali kubwa za madini katika taifa kubwa kieneo la Afrika.

Tanzania imeshatuma batallani za TPDF kulinda amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa / UN - monusco mara nyingi kwa miaka lakini juhudi hizo zinagonga mwamba kutokana na wadau-wenye tamaa za kupora mali za madini yenye thamani kubwa Congo.

https://monusco.unmissions.org › ba...
Background | MONUSCO - UN missions

Although significant progress has been achieved in the DRC since the establishment of UN peacekeeping operation there and the situation in ....Since 1999, about US$8.74 billion has been spent to fund the UN peacekeeping effort in DRC. As of October 2017, the total strength of UN peacekeeping

W5 + 1H
 
Mikutano ya kikanda kuhusu Drc imekuwepo miaka nenda rudi lakini hakuna tija yoyote iliyopatikana.
Sijakuelewa!
Screenshot_2022-06-21-00-07-57-12.jpg
 
Raisi hapa kakosea na tumekuwa wazembe sana na wavivu kama nchi. Congo DRC ni sehemu muhimu sana lakini tumekuwa wazembe sana na tunawaachia nch za nje wanatumia mbinu za kuwagombanisha ili tu wachukuwe madini . Tanzania kama nchi kubwa tulikuwa na uwezo mkubwa sana kuanzia enzi za kabila kuifanya Congo kuwa sehemu yenye usalama na kusaidia nchi yetu.

Kwenye mkutano wa Kenya Tanzania imewakilishwa na balozi yaani hata Makamu wa Raisi au waziri wa ulinzi ameshidwa kwenda. Ni aibu na ni Raisi gani ataongea vitu vya siri kwa balozi? tusishangae balozi wetu kuwekwa nje wakati wakiongea mambo muhimu. Ni bora hata Raisi Samia angetumia mtandao na sio hivi. Lakini kibaya tunaonekana dhaifu sana kwa Raisi wa Congo kwasababu tu tunaogopa kumkasirisha Kagame kwa kupingana naye kwenye hili. Kikwete ndiye aliweza kumsema wazi wazi na Samia hapa kakosea na kuonyesha udhaifu mkubwa kwa majirani zetu.

Tayari Tanzania tuna majeshi ya kulinda amani DRC na huu mkutano ulikuwa unajadili kupeleka ASKARI huko DRC. Rais Samia hakuona umuhimu wa kwenda kwenye kikao hicho sababu hiyo.
 
Rais yupo sahihi.Migogoro ya DRC inasababishwa na Kagame na Museven hao ndiyo wanaofadhili vikundi vya waasi kwa lengo la kuiba rasilimali za DRC.Uganda na Rwanda wote Wana majeshi ndani ya DRC.Wanaingiza majeshi yao kwa kudai yanaenda kupambana na waasi wa nchi zao wakati huohuo kusapot vikundi vya waasi wa DRC na kuiba madini ya DRC.
Tanzania kuwakilishwa na balozi ni sawa na kutuma ujumbe wa kidiplomasia kuwa acheni ujinga.Hao ndiyo wanaosababisha mgogoro halafu wanakutana bila kuambiana ukweli.
 
Mimi binafsi nimesikitishwa na mama kutohudhuria kikao hicho ambacho kidiplomasia nadhani ilikua ni muhimu ahudhurie. Tuache ushabiki wa kiitikadi, suala la balozi kutuwakilisha katika kikao hicho nyeti ni kuwavunja moyo mataifa wanachama.Haiwezekani katika kikao kama hicho, Rais asiende, makamu wa rais asiende au waziri Mkuu. na mpaka sasa serikali ipo kimya kwamba wakati wito wa kikao hicho unatolewa, huenda viongozi hao wote wako ughaibuni.
Lakini kama nchi tumekosea sana.Zipo ziara nyingi tu viongozi wakubwa wamesafiri kwenda tena kwa garama kubwa na ambazo sio hata muhimu ukilinganisha na kikao cha jana na chenye gharama nafuu. TUMECHEMKA
Tuache ushabiki wa kivyama na tusimame kama Taifa
 
Raisi hapa kakosea na tumekuwa wazembe sana na wavivu kama nchi. Congo DRC ni sehemu muhimu sana lakini tumekuwa wazembe sana na tunawaachia nch za nje wanatumia mbinu za kuwagombanisha ili tu wachukuwe madini . Tanzania kama nchi kubwa tulikuwa na uwezo mkubwa sana kuanzia enzi za kabila kuifanya Congo kuwa sehemu yenye usalama na kusaidia nchi yetu.

Kwenye mkutano wa Kenya Tanzania imewakilishwa na balozi yaani hata Makamu wa Raisi au waziri wa ulinzi ameshidwa kwenda. Ni aibu na ni Raisi gani ataongea vitu vya siri kwa balozi? tusishangae balozi wetu kuwekwa nje wakati wakiongea mambo muhimu. Ni bora hata Raisi Samia angetumia mtandao na sio hivi. Lakini kibaya tunaonekana dhaifu sana kwa Raisi wa Congo kwasababu tu tunaogopa kumkasirisha Kagame kwa kupingana naye kwenye hili. Kikwete ndiye aliweza kumsema wazi wazi na Samia hapa kakosea na kuonyesha udhaifu mkubwa kwa majirani zetu.

Kwa hiyo wewe ndio unajua Sana kuliko Rais,Mwanasheria mkuu na Wizara ya mambo ya nje?

Tayari jeshi letu liko DRC so huo mkutano kwetu sio muhimu Sana ni kupiga kura tuu ya watakachokubaliana.
 
Itisha mkutano wa kusuluhisha Urusi na Yukreni halafu ufanyike Urusi uone kama mama hataenda kama ataalikwa
 
Kama Samia hakuhudhuria labda Ina maana ameshakubaliana na jambo litakalojadikiwa,yaani, kupeleka stabilization force kule.
 
Rais hapa kakosea na tumekuwa wazembe sana na wavivu kama nchi. Congo DRC ni sehemu muhimu sana lakini tumekuwa wazembe sana na tunawaachia nchi za nje wanatumia mbinu za kuwagombanisha ili tu wachukue madini. Tanzania kama nchi kubwa tulikuwa na uwezo mkubwa sana kuanzia enzi za kabila kuifanya Congo kuwa sehemu yenye usalama na kusaidia nchi yetu.

Kwenye mkutano wa Kenya, Tanzania imewakilishwa na balozi yaani hata Makamu wa Rais au waziri wa ulinzi ameshidwa kwenda. Ni aibu na ni Rais gani ataongea vitu vya siri kwa balozi? Tusishangae balozi wetu kuwekwa nje wakati wakiongea mambo muhimu. Ni bora hata Rais Samia angetumia mtandao na sio hivi. Lakini kibaya tunaonekana dhaifu sana kwa Rais wa Congo kwasababu tu tunaogopa kumkasirisha Kagame kwa kupingana naye kwenye hili. Kikwete ndiye aliweza kumsema wazi wazi na Samia hapa kakosea na kuonyesha udhaifu mkubwa kwa majirani zetu.

We nyang'au umeandika upuuzi ndo maana uzi wako umepuuzwa. Nafikiri huu ndo muda wa JF kuangalia uwezekano wa kusajiri watu kulingana elimu zao. Maana sasa hivi jukwaa hili limejaza mambumbumbu na mazezeta.
 
Acha wafu wazikane.

Maza anaenda overseas tu hapo jirani tunaweza tuma hata balozi wa nyumba 10.
 
Hija ni muhimu kuliko vikao kama hivyo, tens kimefanyika nchi jirani. Angemtuma makamu, waziri mkuu au hata rais mstaafu
 
Back
Top Bottom