Kauli zinazotolewa na Rais Magufuli na zile za Spika Ndugai kuhusu viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA), zinashabiana sana

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Kwanza nieleze kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi kuna mihimili 3 katika nchi, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama, ambayo inatakiwa kufanya shughuli zake bila kuingiliana, katika kile tunachokiita kwa Kiingereza kama "check and balances"

Hali ni tofauti sana katika nchi hii, kwa kuwa Rais ndiyo kawa kama Spika wa Bunge ambaye anatoa maagizo ya nini kifanyike humo Bungeni.

Nitatoa mifano michache ya ninachoongelea, siku za nyuma Rais Magufuli aliwahi msifu hadharani kuwa kitendo anachofanya Spika Ndugai, kule Bungeni cha kuwatimua viongozi wa Chadema kuwa anafanya vizuri sana na akamuahidi Spika kuwa aendelee na Uzi huo huo na akamuahidi kuwa baada ya kuwatoa kule Bungeni wakija huku "uraiani" amwachie yeye Rais ambaye atajua namna atakavyowashughulikia.

Rais alitamka pia hadharani pale Chato wakati akimwapisha waziri Mwigulu mbele ya waandishi wa habari kuwa amemuagiza Spika Ndugai, asiwalipe posho zao wabunge wote wa Chadema waliosusia vikao vya Bunge.

Hivi unadhani vitendo vinavyofanywa na Spika Ndugai vinafanyika "by coincidence"?

La hasha, bali ni "conspiracy" ya hao watu wawili na huo mkakati wao wa utekelezaji wa kukiangamiza chama hicho kikuu cha upinzani nchini cha Chadema

Hebu tuchukulie hatua aliyochukua Spika Ndugai, kuhusu wale wabunge 4 ambao Chama chao cha Chadema wametoa taarifa kuwa wamevuliwa uanachama wao.

Inafahamika wazi kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhiri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 71(1)(e) inatamka wazi kuwa mbunge ambaye chama chake kilichomdhamini na kuupata ubunge huo kinapomvua uanachama, automatically ubunge wake pia unakuwa umekoma.

Sasa kiburi hiki anakipata wapi Spika wa Bunge cha kuwaambia wabunge hao waendekee na shughuli zao za ubunge wakati yeye Spika anaelewa fika Katiba ya nchi inavyosema kuhusu kuendelea na ubunge?

Ifahamike pia kuwa Chama cha Chadema ndiyo nimekuwa "main target" tokea Mheshimiwa huyu aingie madarakani mwaka 2015.

Refer kauli mbalimbali zilizotolewa huko nyuma na makada mbalimbali wa CCM kuwa chama cha Chadema kitakufa kabla ya mwaka 2020.

Hivi kuna tofauti gani ya hizo "wishes" za hao makada wa CCM na kauli aliyotoa Spika Ndugai majuzi wakati akiwakingia kifua wabunge hao wa Chadema na kauli yake kuwa anamuomba msajili wa vyama aangalie tena kama chama cha Chadema, kinastahili kuwepo nchini?

Niwatie Moyo viongozi wakuu wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema kuwa tumaini pekee la wananchi wa nchi hii lipo kwenu kwa hiyo pamoja na mateso makubwa mnayopitia katika kipindi hiki cha utawala huu wa awamu ya , wakati mnatekeleza kihalali majukumu yenu, zingatieni ile kauli mbiu inayosema NO RETREAT NO SURRENDER.
 
Kitu kinachowapa "frustrations" hao viongozi wa CCM ni kutokana na ahadi yao kwa wananchi kuwa watakiangamiza chama cha Chadema, kabla ya mwaka 2020!

Wanachoshangaa hao makada ni kukiona chama hicho bado "kina-survive"

Walichosahau hao makada wa CCM ni kuwa Chadema ni mpango wa Mungu
 
JIWE yupo ndani ya ubongo waNdugai, MATAGA wapo kwenyee soli za JIWE wanazilamba, , MUSIBA, GWAJIMA, LUSINDE na BASHITE , MUFTI MKUU na waganga wa kujifukiza ndio washauri wakuu, unategemea nini
 
Kitu kinachowapa "frustrations" hao viongozi wa CCM ni kutokana na ahadi yao kwa wananchi kuwa watakiangamiza chama cha Chadema, kabla ya mwaka 2020!

Wanachoshangaa hao makada ni kukiona chama hicho bado "kina-survive"

Walichosahau hao makada wa CCM ni kuwa Chadema ni mpango wa Mungu
Mtu yeyote anayetamani upinzani ufutike ana matatizo ya kifikiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Job Ndugai, atakuwa spika wa kwanza barani Afrika kufikishwa mahakamani baada ya kustaafu na kufungwa kwa matumiza mabaya ya ofisi na kuvunja katiba ya nchi.
Neno hilo nalitoa Leo tarehe 14.05.2020 nikiwa na akili timamu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom