Rais Samia ziarani mkoani Arusha, kuwatunuku Kamisheni Maofisa wa JWTZ (TMA)

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,703
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani atafanya Ziara ya kikazi Arusha kuanzia kesho Novemba 21, 2021.

Akiwa Arusha atawatunuku Kamisheni Maofisa Wanafunzi wa JWTZ Kwenye Chuo Cha Uongozi wa Kijeshi Monduli (TMA).

Mama Samia pia atahusika kwenye uzinduzi wa Hotel ya Nyota 5 iliyopo Jijini Arusha.

KaziIendelee.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hongera mama SSH. Arusha tulizoea maafisa wa Jeshi la wananchi wakipewa Kamisheni yao hukuhuku Arusha.

Hapa kati ghafla tulianza kushuhudia Kamisheni ikitolewa katika 'nchi ya ugenini' Magogoni DSM. Nini kilisababisha hali ile? Ilikuwa Kwa maslahi ya nani?

Hongera kurudisha utaratibu unaokubalika Jeshini. Tusiichezee Jeshi la nchi hata kidogo.
 
Aisee Eya basi inaupiga mwingi. Baada ya hapo itakuwa inaelekea wapi?
 
Hongera mama SSH. Arusha tulizoea maafisa wa Jeshi la wananchi wakipewa Kamisheni yao hukuhuku Arusha. Hapa kati ghafla tulianza kushuhudia Kamisheni ikitolewa katika 'nchi ya ugenini' Magogoni DSM. Nini kilisababisha hali ile? Ilikuwa Kwa maslahi ya nani? Hongera kurudisha utaratibu unaokubalika Jeshini. Tusiichezee Jeshi la nchi hata kidogo.

Hayo madogo, umesahau kuna siku kamisheni ya jeshi ilifanyikia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha wakapokelewa wanaccm waliohama upinzani kwenda kuunga juhudi!
 
Hayo madogo, umesahau kuna siku kamisheni ya jeshi ilifanyikia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha wakapokelewa wanaccm waliohama upinzani kwenda kuunga juhudi!
Nakumbuka, siku hiyo nilikuwa pale Picnic. Tulishangaa na kusikitika sana. Nchi ilinajisiwa sana, halafu wajinga akina YEHODAYA Wakudadavuwa na manyang'au mengine yakililia legacy. Shenzi. Nchi hii imechezewa sana. Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Si kwa kuzurura huku...imagine miaka 10 kwa rate hii ya kuzurura...akitoka hapo anachukua pipa. Ni kama vile kuzurura kunamliwaza na mizigo yake mizito iliyomuelemea .
 
Nakumbuka, siku hiyo nilikuwa pale Picnic. Tulishangaa na kusikitika sana. Nchi ilinajisiwa sana, halafu wajinga akina YEHODAYA Wakudadavuwa na manyang'au mengine yakililia legacy. Shenzi. Nchi hii imechezewa sana. Au nasema uwongo ndugu zangu?

Acha tu, na ile ni kinyume kabisa na katiba kuchanganya jeshi na siasa. Halafu alikuwa anawaambia watu wafuate sheria.
 
Acha tu, na ile ni kinyume kabisa na katiba kuchanganya jeshi na siasa. Halafu alikuwa anawaambia watu wafuate sheria.
Ilikuwa ni kuhadaa wanyonge. Sheria ipi? Akitaka kupenyeza jambo lake kwenye kadamnsai utasikia "maendeleo hayana chamaaa". Daah. Tumetoka mbali lakini kama nchi.
 
Ndiyo majukumu yake ya kikatiba na yuko ndani ya nchi.Mbona Mwanza alikuja kwenye sherehe ya miaka 50 ya uhuru..Jua kwa sasa tunandege zetu za kisasa za airbus zanziba
 
Back
Top Bottom