😁😁😁Bila mafuriko asingerudi? Mkutano umeisha siku nyingi
Anabiashara gani huko Dubai?
😁😁😁Bila mafuriko asingerudi? Mkutano umeisha siku nyingi
Anabiashara gani huko Dubai?
Kwani mkutano mmemaliza lini,tuanzie hapo kwaza!Rais wetu ni kiongozi mwenye upendo mkubwa sana kwa watanzania,ni kiongozi mwenye huruma na anayeguswa na matatizo ya watu.ni mfariji wa Taifa letu .Mungu ambariki sana Rais wetu mpendwa.
Tafuta namna nzuri ya uandishi. Narudia kukuambia kuwa huenda hata Mhe Mama yetu asifurahishwe na huo uandishi wako kwasababu hauna lengo la kuhabarisha bali UCHAWA ULIOPITILIZA.Sijaandika kikampeni wala kinafiki bali nimeandika na kuwasilisha taarifa kama ilivyo.
Akifika parapanda ikalia wewe ndo utakuwa shetwani kwa kuuficha ukweliAcha ushetani ndugu yangu.
Nani kakwambia kuwa nafanya uchawa hapa.mimi nawaleteeni ukweliTafuta namna nzuri ya uandishi. Narudia kukuambia kuwa huenda hata Mhe Mama yetu asifurahishwe na huo uandishi wako kwasababu hauna lengo la kuhabarisha bali UCHAWA ULIOPITILIZA.
Unajua ndio maana hata hupigiwi simu japo umeiweka namba yako
Mkutano haujaisha bali unaendelea mpaka tarehe 12 mwezi huuKwani mkutano mmemaliza lini,tuanzie hapo kwaza!
Itakuwa kapitia Makunduchi kwenda kuhesabu mawe kwanzaVipi bado hajafika tu Tz, inakuwaje safari ya kutoka Dubai-Tz iwe zaidi ya masaa 24?
Huyu mama toka amefiwa na mumewe mwezi wa 7 kichwa hakipo sawa tenaUandishi wa Kichawa hasa, Low minded people ni janga sana nchi huu, unamsufu mtu moja unahisi kinyaa, unamsifu mtu ambaye hata akikusikiliza anakiona haunazo, unatoa sifa kwa mtu zaidi ya kuonyesha masikitiko ya janga lililowapata wananchi
Pesa za bara zimekuwa zakufanyia mazoeziWaokoe pesa za walipa kodi masikini....PM yupo anatosha yeye acha azurule na wa zbar wengi maana wanajidanganya eti zamu yao......list of shame tumeiona ...aibù na dhambi kubwa wanatafuna hela masikiniii.....hata akirudi atafanya nini ?? Hana impact
Unamjua huyo? Uliereply comment yake?Nani kakwambia kuwa nafanya uchawa hapa.mimi nawaleteeni ukweli
Wewe unamfahamu?Unamjua huyo? Uliereply comment yake?
Anakuja kwa jambo moja tu ambalo ni hilo lililotokea mkoani manyara.Anakuja kwa jambo jingine, wee unasema mafuriko Lol.
Ila luca bhana, khaaaa.
Kijana Lucas kuwa makini..Wewe unamfahamu?
Haswaaaaa na hakuna mwenye uchungu na bara ......hakunaaaPesa za bara zimekuwa zakufanyia mazoezi
Wabara hatuna akili hata kidogo, mbona wazanzibar hawakubali za kwao zichezewe na mtu kutoka bara? hakuna hata diwani kutoka bara.Haswaaaaa na hakuna mwenye uchungu na bara ......hakunaaa
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia suluhu Hasssan ameamua kukatisha shughuli za mkutano unaoendelea Dubai ili kurejea kwa dharura nchini ,kwa ajili ya kushughulikia maafa yaliyotokea mkoani manyara eneo la kateshi yaliyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jumapili ambapo mpaka sasa watu takribani 20 wamepoteza maisha.
Ambapo Rais wetu mpendwa kwa maumivu makubwa ,uchungu mkubwa na hisia kali sana ametoa pole sanaa kwa watanzania wenzetu na familia zilizopatwa na kupoteza wapendwa wao,lakini pia mh Rais ametoa pole kwa majeruhi wote.
Pia mh Rais wetu mpendwa ametoa maagizo mazito sana ,ambapo ameagiza wizara ya afya kufika haraka sana eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia majeruhi wote.lakini pia mh Rais wetu ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufika kwa uharaka eneo la tukio ili kusaidia na kufanya shughuli za uokoaji,pia mh Rais wetu mpendwa ametoa maagizo kwa wizara ya madini kufika mlimani ambako ndiko athari ilikoanzia ili kufanya uchunguzi.
Lakini pia ameagiza waziri anayeshughulikia maafa pia naye afike haraka sanaa eneo la tukio na serikali yetu ielekeze nguvu zake zote huko wakati yeye akiwa njiani kurejea nchini kwa ajili ya kuja kuungana na kushiriki katika suala hilo zito lililochukua maisha ya watanzania wenzetu na kufanya uharibufu mkubwa sana.
Hii ndio maana ya kuitwa kiongozi ,.hii ndio maana ya Rais samia kupendwa na kukubalika sana na watanzania,kwa sababu ni kiongozi aliyekaribu sana na watanzania na anayeguswa na maisha ya watanzania.ni kiongozi mwenye huruma na anayethamini sana maisha ya kila mtanzania. Kwa upendo wake mkubwa kwa watanzania ndio maana tunamuona Rais wetu akikatisha mkutano wako na kurejea nchini, kwasababu anatambua kuwa yupo hapo alipo kwa ajili ya watanzania na ndio maana anarejea kwa ajili ya kuokoa na kushughulika na maisha ya watanzania.
Tumuombee Rais wetu mpendwa arejee salama na kufika salama hapa nchini. Mungu amlinde na kumtetea Rais wetu wakati wote wa safari yake katika kurejea nchini.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.