Rais Samia wewe ndio chanzo cha matatizo ya umeme nchini

Rais Samia wewe ndio chanzo cha matatizo ya umeme nchini

Ni sawa lakini na watendaji tanesco wanapaswa kubeba lawama kwa kutoweka mbele professionalism na badala yake wanahofia kufukuzwa kazi tu basi.
Ni wao haohao waliambiwa msikate umeme hawakukata na wao haohao wameambiwa kata umeme wanakata, inamaana wanasiasa ndio wataalamu wa uzalishaji na ugawaji umeme na sio wataalamu wetu wa tanesco?!

Kwanini asitokee jasiri mmoja akamwambia waziri, bwana mkubwa; situation ya sasa hairuhusu kukata umeme kwa sababu upo wa kutosha hivyo HATUKATI, kisha akafukuzwa kazi kwa kulinda profession yake akaenda kuomba kazi hata nchi za nje na hiyo cv yake ambayo inakuwa imepanda abrutly?
Kwani TANESCO Ni Limited Company?
 
Kama wewe siyo ccm na unawalaumu watendaji wa TANESCO yani unaamini wao ndiyo tatizo basi una mtindio wa akili haiko sawa
Umeme kuwa na utulivu wakati wa Magufuli ule ulikuwa msimamo wa Magufuli na wala siyo waziri
Umeme kukosa utulivu sasa ni msimamo wa samia
Pia alituambia mgawo utakuwa kwa miezi 6
 
Nina jamaa yngu ni kipofu lakini kutwa analalamika suala hili la mgao wa umeme,,


Imefika mahali hata kipofu amegunduwa inchi ipo gizani?
Hii ni hatari sana..

Watawala muwe na huruma na wanainchi,,

msiweke personal interest zenu kwenye masuala ya msingi kwenye maisha ya watu.
 
Kadanganye wapumbavu wenzako.

Kama umeme haukukatika.hizi.kauli alikuwa anamtishia nani?
View attachment 2851686View attachment 2851687
Kwani hawa watanzania wanao lalamika sasa hawakuwa wamezaliwa kipindi hiki? Hili kumtetea Samia kwenye hili unahitaji kunena zaidi ya lugha 200!
Watanzania wanajua fika hakukuwa na hakuwai kuwa na mgao wala katika katika ya sasa ndio maana kisingizio kimekuwa mitambo iliendeshwa bila kukarabatiwa muda wote na tukaambiwa kuna mgao kwa sababu mitambo haikukarabitiwa miaka 5 ! Hahaha yani kwenye hili la Umemebora unyamaze kila mwenye macho anaona mwenyewe na ana majibu kabisa …toka hapo nje kwako kawaulize halafu uwape huo utetezi wako….
Hahaha mkuu hata unene kwa lugha hili jambo hakuna wakukuelewa
 
Siku moja.kabla ya Kutangaza kifo cha Magufuli akiwa Tanga alisema umeme kukatika mwisho lakini yeye ndiye ameongoza kuongoza nchi ikiwa gizani, akapumzike hawezi kuongoza.
 
Kwani hawa watanzania wanao lalamika sasa hawakuwa wamezaliwa kipindi hiki? Hili kumtetea Samia kwenye hili unahitaji kunena zaidi ya lugha 200!
Watanzania wanajua fika hakukuwa na hakuwai kuwa na mgao wala katika katika ya sasa ndio maana kisingizio kimekuwa mitambo iliendeshwa bila kukarabatiwa muda wote na tukaambiwa kuna mgao kwa sababu mitambo haikukarabitiwa miaka 5 ! Hahaha yani kwenye hili la Umemebora unyamaze kila mwenye macho anaona mwenyewe na ana majibu kabisa …toka hapo nje kwako kawaulize halafu uwape huo utetezi wako….
Hahaha mkuu hata unene kwa lugha hili jambo hakuna wakukuelewa
Watanzania wa wapi hao?
 
Kwanza Rais alirusha kijembe wanao kejeli na kisha akasema hayo lakini maswali ya wengi kwanini Tatizo limekuwa kubwa zaidi tena maradufu kipindi ambacho mnasema mnakarabati mitambo wakati kipindi mnasema hakufanyiwa ukarabati au mantainance hakukuwa na hii shida? Hivi mtandanganya hadi lini? Kwenye hili la Umeme hakuna mtanzania mtamdanganya labda aliyezaliwa 2023
Cha ajabu watu walisha sahau hicho kisingizio cha ukarabati zinatolewa sababu zengine ila yeye Samia akaturudisha tena kwenye ukarabati et mitambo haikuwa ikifanyiwa service.
 
Kwamba february ndio wanamaliza wanamaliza kufanya service ya mitambo?
Uchakavu wa mitambo hausababishi mgao Bali unasababisha katika katika ya umeme.

Mgao upo Kwa sababu umeme uko kidogo kuliko unaohitajika.
 
Uchakavu wa mitambo hausababishi mgao Bali unasababisha katika katika ya umeme.

Mgao upo Kwa sababu umeme uko kidogo kuliko unaohitajika.
Ndio maana nilisema hili halieleweki, kwahiyo mwezi february shida ya umeme mdogo inakuwa imepatiwa ufumbuzi ndio maana unasema mgao unaisha huo mwezi wa pili?
 
Rais wangu bila kupepesa macho wala kuona haya wewe ndo chanzo cha matatizo ya umeme nchini yote haya yana baraka zako na chanzo ni wewe

Mama aliingia akakuta shirika la TANESCO na umeme ulikua umetengamaa kwa kiasi kikubwa.

Akaanza kubadilisha watu wa TANESCO na kuweka watu aliyowaona yeye....Hapa anaulaumiwa yeye.

Akaja kumtumbua Kalemani, kosa la kumtoa Kalemani hakulitoa, lakini za chini chini zinadai ni personal issues, kuogopa legacy ya mwendazake, na mambo ya ukabila, akamuweka Makamba, Makamba kaingia matatizo yakaanza....Hapa Rais ni wa kulaumiwa hadi Akhera

Hakuishia hapo tu, umeme ulipoanza kuharibiwa na Makamba hakukemea wala kuhoji au kumgombeza Makamba alitulia kama "halimuhusu vile"....,Samia unastahili lawama.

Gesi ikapanda, wakati huo huo waziri anazunguka kugawa mitungi ya Taifa gesi na Mihan kwa kutumia pesa za umma huku hiyo kampuni waziri ana hisa humo....Rais hakuongea chochote zaidi ya kuacha yaendelee.

TANESCO wakakodi app kutoka India kwa bilioni 69 Rais kimyaaa

Makamba akaanza kuivuruga TANESCO yeye na Maharage wakaja na matengenezo yasiyokwisha pesa zikiwa hazijulikani zinapokwenda Rais kimyaaa

Maharage akaingiza kitengo cha kampuni yake ya huduma kwa Wateja rais kimyaa

Nchi ikarudi Gizani Rais kimyaaa

Halafu mnasema Rais asilaumiwe kwenye hili la umeme kwani yakiwa yanatokea si yalikua na baraka zake? Au mnataka kusema wakati yote yakijiri yeye alikua usingizini?

Tunazunguka sana kuwalaumu wengine huku tukisahau mtu anayestahili kulaumiwa na kunyooshewa kidole ni "SAMIA SULUHU HASSAN" huyu ndo chanzo cha matatizo yote na yeye ndo aliyewapa "greenlight" kina Makamba wafanye wanavyotaka.

Mnawalaumu TANESCO wakati wao wanafata tu wanachoambiwa?Au mmesahau TANESCO ni watu wa "ndio mzee" wanafata maagizo ya wakubwa? Kipindi cha Magufuli waliambiwa hamna kukata umeme au migao na wakatii sasa tuwalaumu TANESCO wakati wao wanafuata maagizo ya "Samia na Makamba?"

Ingekua nchi nyingine huyu Samia angejiuzulu tu na kuwajibishwa pamoja na Makamba na Maharage lakini bahati tunatawaliwa na mfumo na bunge ambalo ni la chama kimoja tu.

Kuhusu umeme wakulaumiwa na Rais Samia kwa 100%
Mama sada anaupiga mwing

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Chawa lingine hili. Wao matatizo ya
Lawama za kipumbavu sana hizi. Moderator futa hii. Wewe mleta uzi elewa umeme wa Tanzania hautoshi na pia tayari kuanzia awamu ya 3 TANESCO imehujumiwa mno.... imekuwa ikilipa fedha nyingi kwa kuingia mikataba mibovu iliyosababishwa na watanzania wenzetu. Hata angekuwepo Magufuli bado tatizo lingeendelea. Tusubiri bwawa likamilike tujiondoe kwenye hili tatizo.
inci hayawahusu, wako after posho za uchawa
 
Back
Top Bottom