Rais Samia, wakulima wa Miwa wanatishia kukibomoa Kiwanda cha Sukari cha Mbigiri

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,107
1,782
Salaam kwa jina la jamhuri ya muungano Mama Samia Suluhu Hassan!

INGILIA KATI KWENYE HILI WAKULIMA WANATAKA KUKIBOMOA KIWANDA CHA SUKARI MBIGIRI.

1623735375465.png

Kiwanda cha sukari Mbigiri ambacho haijulikani ni lini kitaanza kazi kuokoa mamilioni ya pesa yatayopotea kwa kuaribika kwa miwa iliyofikia kuvunwa.​

Baada ya serikali kuamua kuanzisha kiwanda cha miwa cha Mkulazi chini ya NSSF na PPF tarehe 6 Septemba, iliwashawishi wakulima wa nje (outgrowers) kwa kufuata sera ya kilimo ya mwaka 2013 kuanzisha vikundi vyao kupitia vyama vyao vya msingi vya ushirika ili walime mashamba ya miwa.

Wakulima walikuwa na hofu ya kilimo cha miwa kwani walikuwa wamezoea kilimo cha mpunga na mahindi. Serikali iliwatumia wataalam wa kilimo cha miwa kuwaelimisha wakulima kuwa kilimo cha miwa kina faida kubwa na kuwaaminisha kuwa ni zao litakalowaondolea umasikini walionao kama anavyofanya waziri mkuu kwenye zao la alizeti kwa sasa.

Kwa kupitia mifano hai waliyoitoa kwa wakulima kutoka kwa wakulima wa Mtibwa na Kilombero jinsi wanavyonufaika na kilimo cha miwa , wakulima wa mbigiri walishawishika na kutenga mashamba yao waliyokuwa wanalima mpunga na kuyaandaa kwa ajili ya kulima miwa.

Kulikuwa na matangazo mbalimbali kwenye radio ya taifaTBC kuamasisha wakulima kuchangamkia fulsa ya kulima miwa kwa vile mkombozi wao kiwanda cha miwa kimekuja kuwaondolea umasikini na kuwakomboa kimaisha.

Wakulima wengi walishawishika japo walikuwepo wachache walishindwa kuamini, walisema mara nyingi serikali hii si ya kweli na haina nia njema na watu wa maisha ya chini.

Mkataba ulisainiwa kati ya Kampuni ya Mkulazi, Benki ya Azania na Chama cha ushirika cha kati cha Magole mwaka 2018 kwa lengo la kutoa mkopo kwa wakulima wa nje(outgrowers)

Benki ya Azania iliridhia kutoa jumla ya Tshs bilioni 4.9628 kwa awamu kwa ajili ya kugharamia gharama za kilimo ambacho ni gharama za kuandaa mashamba, mbolea, dawa za wadudu, mbegu na kuchimba visima.

Kilimo kilianza vizuri kwa awamu na kuleta matumaini makubwa maeneo ya Mbigiri, Msowero na Magole. Mwaka 2017/18 lengo lilkuwa ni kulima ekari 3200 za miwa, lakini zililimwa na kupandwa ekari 1044 za miwa pekee.

Kwa mwaka wa fedha 2019/20 lengo lilikuwa kupanda ekari 2500 lakini walifanikiwa kulima na kupanda ekari 1035 tu.

1623735509342.png

WAKULIMA WAKAAMINISHWA KUWA PUNDE MIWA YAO ITAKAPOFIKIA KUVUNWA, KIWANDA KITAKUWA KIMEKAMILIKA
Kwa baati mbaya kwa wale wakulima walianza kulima kwenye awamu ya awali, miwa yao ilifikia hatua ya kuvunmwa lakini kiwanda kikawa bado kukamilika. Hali hii iliwalazimu wakulima wasafirishe miwa yao na kwenda kuiuza kiwanda cha Mtibwa kwa bei ya hasara sana.

Mpaka kufikia leo hii ya tarehe 15-06-2021 kiwanda bado akijakamilika na miwa mingi imefikia hatua ya kuaribika na hakuna sehemu ya kwenda kuiuza.
1623735554705.png

BENKI YA AZANIA YASITISHA MKOPO KWA WAKULIMA
Baada ya kuona kiwanda kinasuasua kukamilika, Benki ya Azania imeamua kukataa kutoa mkopo wa Tshs bilioni 1.797 kwa wakulima ambao mashamba yao bado yanaendelea kuandaliwa.

Kitendo cha kusitisha mkopo huo, wakulima leo hii wanadaiwa na wakandarasi waliowasambazia pembejeo na wamewafungulia kesi kwa kushindwa kuwalipa pesa za gharama za madawa, kuandaa mashamba, mbolea na mbegu walizowasambazia.

BENKI YA AZANIA YAWAONGEZEA WAKULIMA RIBA YA ASILIMIA SITA(6%) KAMA ADHABU YA KUCHELEWA KULIPA MADENI WANAYODAIWA
Kwa vile kiwanda bado hakijakamilik a na mkulima anashindwa kuuza miwa yake na wengine kushindwa kumalizia mashamba yao kwa vile benki imekataa kuwapa mikopo ya kumalizia, mkulima ameongezewa mzigo mwingine wa asilimia sita (6%) kama adhabu na Benki ya Azania kwa kuchelewa kulipa wakati.

WAKANDARASI WA PEMBEJEO, BIASHARA ZAO ZIMEYUMBA NA WENGINE WAMEFIRISIKA
Baadhi ya wakandarasi waliotumika kuwasambazia pembejeo wakulima wamefunga kampuni zao na kubaki na madeni makubwa benki walipokopa pesa.

Azania Benki wamekataa kulipa pesa na wakulima hawana pesa za kuwalipa wakandarasi licha ya kushitakiwa na wakandarasi. Kwa kweli wakulima hawana hamu tena na kilimo cha miwa.

WIZARA YA VIWANDA NA KILIMO WOTE WANAFAHAMU SHIDA WANAYOIPATA WAKULIMA HAWA
Wizara hizi mbili zinafaham malalamiko na mateso wanayoyapata wakulima hawa wa Mbigiri. Miaka inapita wanashindwa kulipatia ufumbuzi jambo hili. Wakulima wanapata shaka” huenda wanapata masirai yao binafsi” Wanashindwaje kuiamuru Azania ilipe pesa walizoaidi kuzilipa?

Wanashindwaje kumalizia hatua ya kiwanda iliyobaki ili kianze kazi na kuokoa mamilioni ya pesa?

KIFUPI NI KWAMBA;
Hali ya wakulima wa miwa Mbigiri imekuwa ni mbaya sana. Kilimo cha miwa kimewaletea umasikini mkubwa sana. Kibaya zaidi hawana wa kuwasemea, mbunge wao Kabudi yupo kimya juu ya jambo hili japo anafahamu nini wapiga kura wake wanavyoangamia.

Baadhi ya wakulima wameanza kuchimbua miwa na kujiandaa na kilimo cha mpunga walichokizoea.

Wakulima wameongezewa adhabu ya asilimia sita na Benki ya Azania kwa kosa la serikali la kutokamilisha kiwanda kwa wakati.

Wakulima wameshitakiwa na wakandarasi wakidaiwa pesa ambazo kimsingi Azania ndiyo wanapaswa kulipa.

WAKULIMA WATISHIA KUKIBOMOA KIWANDA

Kwa hasara waliyoipata na madeni wanayodaiwa na wakandarasi, pamoja na umasikini uliosababishwa na serikali na waliowashawishi kujiingiza kwenye kilimo cha miwa, wakulima wanaona kuwa yote haya yasingewapata kama kusingekuwa na kiwanda hiki cha sukari.

Wanatishia kwenda kukibomoa kiwanda maana ndiyo chanzo cha maisha yao kuwa duni. Wanafikiri ni bora serikali ingewaacha waendelee na kilimo chao cha mpunga kuliko kuwarubuni na kushindwa kumaliza kiwanda.

MAMA SAMIA SULUHU HASSAN, kwa vile serikali unayoiongoza inajipambanua kuwa haitaki dhulma, tunaomba usaidie mambo yafuatayo;

  • Watake Azania benki walipe deni ambalo wakulima wanadaiwa na wakandarasi ili wakulima waweze kuwa huru.
  • Mtake waziri wa viwanda kumaliza kiwanda hiki cha sukari Mbigiri haraka ili wakulima wapeleke miwa yao iliyofikia kuvunwa kwenye kiwanda hicho.
  • Watake Azania Benki wasitishe kuwatoza adhabu wakulima ya asilimia sita kwani sio kosa lao kuchelewesha kulipa madeni wanayodaiwa.
  • Mtake waziri wa kilimo akawaombe radhi wakulima wa miwa wa Mbigiri kwa kuwalaghai na kuwasababishia umasikini mkubwa.
  • Ufanyie kazi ushauri wa CAG aliyoutoa kwenye ripoti yake ya 2020/21 juu ya kuwasaidia wakulima hawa wa miwa ili kuokoa mamilioni ya shilingi yanayokwenda kupotea kwa kuaribika kwa miwa ya wakulima.
MAMA TUSAIDIE KUIKOA MIWA HII INAKWENDA KUARIBIKA
 
Ahsante kwa mada nzuri iliyojaa FACTS ,hili sio suala la President Samia kuamua,kwani hapo hakuna mamlaka nyingine including RC?na ndio maana nchi inahitaji TAASISI imara na huru maana hii issue ungeweza kuifungulia kesi serikali kwenye mahakama ili mahakama iiamuru serikali kukifungua kiwanda hiki,pls tufuate ngazi za utawala bora,President Samia hawezi kuwa ndio mwamuzi wa kila kitu.
 
Ahsante kwa mada nzuri iliyojaa FACTS ,hili sio suala la President Samia kuamua,kwani hapo hakuna mamlaka nyingine including RC?na ndio maana nchi inahitaji TAASISI imara na huru maana hii issue ungeweza kuifungulia kesi serikali kwenye mahakama ili mahakama iiamuru serikali kukifungua kiwanda hiki,pls tufuate ngazi za utawala bora,President Samia hawezi kuwa ndio mwamuzi wa kila kitu.
Kama kiwanda kilianzishwa kwa tamko la Ikulu na Rais ana wasaidizi ambao wanaonekana hawana msaada kwanini asiingilie ?

Hio ndio gharama ya kuwa Supreme Leader.
 
Ahsante kwa mada nzuri iliyojaa FACTS ,hili sio suala la President Samia kuamua,kwani hapo hakuna mamlaka nyingine including RC?na ndio maana nchi inahitaji TAASISI imara na huru maana hii issue ungeweza kuifungulia kesi serikali kwenye mahakama ili mahakama iiamuru serikali kukifungua kiwanda hiki,pls tufuate ngazi za utawala bora,President Samia hawezi kuwa ndio mwamuzi wa kila kitu.
Kiwanda kilianzishwa kwa matamko ya Rais mwendazake, thats why tunaiambia Ikulu ichukue maamuzi.
 
Huwezi lazimisha benki kutoa mkopo, we ulisikia wapi? Benki inafanya analysis na assessment yenyewe. Kwanza ningekuwa nahusika kwenye hiyo benki tangu mwanzo sitoi mkopo kwa kauli za kisiasa.
 
Huwezi lazimisha benki kutoa mkopo, we ulisikia wapi? Benki inafanya analysis na assessment yenyewe. Kwanza ningekuwa nahusika kwenye hiyo benki tangu mwanzo sitoi mkopo kwa kauli za kisiasa.
Toka awali walisaini mkataba wa kukopesha hao wakulima. Hakuna asiyefahamu kuwa mambo mengi yalifanywa kwa shinikizo la kisiasa.
Sasa nani alaumiwe, mwanasiasa au mtaalamu anayemsujudia mwanasiasa?
 
MAMA TUSAIDIE KUIKOA MIWA HII INAKWENDA KUARIBIKA
Bandiko zuri lililoshiba vithibitisho vyote, Prof. Palamagamba Kabudi mbunge ambaye pia ni waziri, aishauri serikali iwajibike kununua miwa hii kama alivyohangaika na suala la soko la korosho kule kusini mpaka zikanunuliwa kwa operesheni kubwa iliyoongozwa na mwendazake hayati (the revered late) Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli.
 
Kuna kitu huaga sikielewi kabisa, labda na mimi ningekua serikalini huenda ningebweteka hivo. Azania bank inamilikiwa kwa sehemu kubwa na mashirika ya hfadhi ya jamii, NSSF na PPF.

Kiwanda cha sukari (bila kujali kwamba yalikua matamko ya kisiasa au laa) kinamilikiwa na NSSF na PPF, zile ni pesa za NSSF na PPF na hao hao ndio wenye Azania bank, so wanaacha tu kiwanda kife and hence pesa zao zipotee hivi hivi tu kwasababu mwanzilishi wa wazo la kiwanda hicho kafariki?

Msukuma akiwadharau Wasomi anakua kakosea wapi? Anyway, kama match ya Yanga na Simba iliahirishwa kwasababu za matajiri, matajiri hao hao hawawezi kushindwa kuzuia sukari isitengenezwe Tanzania. RIP Magufuli
 
Back
Top Bottom