Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,147
- 56,248
Ndugu rais.
Nakusabahi, hata hivyo nina swali kwako. Ni zaidi ya miezi sita sasa, kijana, mtanzania amepotea.
Umma wa Watanzania umepiga kelele kuhusu kupotea kwa kijana huyu lakini siyo ofisi yako wala wewe uliyeamua kulizungumzia suala hili.
Ndugu rais, ulipoapa kuwa rais uliapa kuwa amiri jeshi mkuu ikimaanisha kuwa ni mlinzi wa nchi, raia, mali zao n.k ndiyo maana vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yako.
Ndugu Rais Soka yuko wapi?
Kipindi Soka amepotea, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Mbowe aliitisha mkutano wa vyombo vya habari na kueleza wanaotuhumiwa kumteka Soka, kwamba ni Polisi huko Temeke. Je ndugu rais umefanya nini ili kuwabana watuhumiwa wamrudishe Soka akiwa salama salmini?.
Ndugu Rais, Kupotea kwa Soka hakuna tofauti na kupotea kwa Ben Saanane. Ninachelea kuwa Legacy yako sababu ya Soka itakija kuchafuka kama vile Legacy ya JPM ilivyochafuka sababu ya Ben Saanane.
Umma wa Watanzania unatunza hizi kumbukumbu ndugu rais. Huko mbeleni vitabu vitaandikwa juu ya haya mambo. Je unataka Kumbukumbu zako za urais zitawaliwe na mambo ya watu kutekwa, kupotezwa na wengine kuuawa?.
Ndugu Rais.
Je huyu mtoto Deusdedith Soka yuko wapi?
Pia soma > Hivi Deusdedith Soka ndio amezimwa kama alivyozimwa Ben Saanane?