Rais Samia, waeleze Watanzania Deusdedith Soka yupo wapi?

Rais Samia, waeleze Watanzania Deusdedith Soka yupo wapi?

..wakati unamuuliza Rais, kwamba Soka yuko wapi, Edson Mwakabela(Sativa) alitekwa kwa lengo la kuuawa, Mungu ni mwema akamnusuru..Sativa ameeleza hatua kwa hatua alivyotekwa..watu waliotakiwa kushikiliwa na kuhojiwa ni wale madalali waliomtafutia nyumba Sativa na hatimaye kutumiwa na watekaji kumlaghai ili wamkamate, wapo na amewataja majina yao, pili Sativa ametaja maofisa wa Polisi kwa majina..utekaji wa Soka unafanana na ule wa Sativa, sasa km Rais ameshindwa kuagiza waliotajwa kumteka Sativa wakamatwe na kuhojiwa..hili la Soka atalipa uzito? Hawezi kuchukua hatua kwa watu waliotajwa na wanajulikana, ije hao wa Soka wamwambie walipompeleka? Sidhani..!
Sativa aliahidi kumalizana nao mwenyewe kama hawatachukuliwa hatua. Tunasubiria matokeo ya kazi yake.
 
Ndugu rais.
Nakusabahi, hata hivyo nina swali kwako. Ni zaidi ya miezi sita sasa, kijana, mtanzania amepotea.

Umma wa Watanzania umepiga kelele kuhusu kupotea kwa kijana huyu lakini siyo ofisi yako wala wewe uliyeamua kulizungumzia suala hili.

Ndugu rais, ulipoapa kuwa rais uliapa kuwa amiri jeshi mkuu ikimaanisha kuwa ni mlinzi wa nchi, raia, mali zao n.k ndiyo maana vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yako.

Ndugu Rais Soka yuko wapi?

Kipindi Soka amepotea, aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Mbowe aliitisha mkutano wa vyombo vya habari na kueleza wanaotuhumiwa kumteka Soka, kwamba ni Polisi huko Temeke. Je ndugu rais umefanya nini ili kuwabana watuhumiwa wamrudishe Soka akiwa salama salmini?.

Ndugu Rais, Kupotea kwa Soka hakuna tofauti na kupotea kwa Ben Saanane. Ninachelea kuwa Legacy yako sababu ya Soka itakija kuchafuka kama vile Legacy ya JPM ilivyochafuka sababu ya Ben Saanane.

Umma wa Watanzania unatunza hizi kumbukumbu ndugu rais. Huko mbeleni vitabu vitaandikwa juu ya haya mambo. Je unataka Kumbukumbu zako za urais zitawaliwe na mambo ya watu kutekwa, kupotezwa na wengine kuuawa?.

Ndugu Rais.
Je huyu mtoto Deusdedith Soka yuko wapi?

Pia soma > Hivi Deusdedith Soka ndio amezimwa kama alivyozimwa Ben Saanane?

Yale Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 2023 yaliyotoa ruhusa ya kuua Watu kwa Maafisa wa Polisi na TISS sasa matunda yake ndio yanaonekana Wazi wazi kabisa kwa Watu kutekwa, kuteswa, kupotezwa na kuuawa.

Aidha, Mabadiliko yale ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 2023 yamewapa ruhusa Watu hao wa Tiss na Polisi kufanya Mauaji ya Watu kadiri watakavyo, na hakuna kitu chochote kile wanaweza wakafanywa. Wameruhusiwa kuua Watu bila ya wao Wauaji kuweza kushitakiwa.
 
Muda utafika, hizo roho zote zitakua accounted tu including za mamia ya vijana waliochinjwa mkiru na kulishwa mamba mto rufiji, damu zao zinalia nyikani!
 
Mtu ambaye alikuwa hatusikilizi...nasisi tutampuuza...hatutamsikiliza hii miezi miwili anayotaka kujitembeza linafki🤔
 
Back
Top Bottom