Mnaosema wakenya wabinafs , sijui wanakuja kuchukua madini haya tuoneshen taifa ambalo halina hizo sifa
 
Tatizo lenu mna janja janja nyingi sana.

Unakumbuka kipindi cha nyuma Kenya ilikuwa inaongoza kwa kuuza tanzanite, vipi mna machimbo ya hayo madini huko kwenu?

Tunataka kufanya biashara na nyie ila kwa umakini wa hali ya juu...sio kwa ulegevu aliouonyesha mama.
Sasa kama hatuna migodi ya Tanzanite na tunaongoza kuuza hiyo bidhaa, hujiulizi wewe, imefika vipi KE, imetoka kwa nani(source) huko Tz na faida au hasara inagawanywa vipi?
Hapo ndipo utajua uhuni uko wapi, sio kusingizia ati tu KE wanjanja ilhali hamjachunguza huko kwenyu. Hakuna pahali pasipokuwa na wajanja.
 
Naona watu tunaendelea kulalamika na kubishana. Tumeunda timu mbili: Moja ni watetezi wa legacy na wapinzani wa mabadiliko na nyingine ni supporters wa utawala mpya ambao walikuwa hawakubaliani na style ya mtangulizi.

Wakati kila upande unahangaika kuandika uzi mpya, werevu wanaangalia fursa zinazojitokeza. Akili za woga na kuendekeza 'fear of unknown' vitatufanya tuendelee kuwa watu wa kulalamika na kujiona wanyonge kila siku.

Maisha lazima yaendelee. Ni lazima kuchukua risk ili kupata returns. Ukikataa risk jua kuwa umekataa na returns zake. Kama tulifanikiwa kuandika historia ya kwamba jana tulidhulumiwa, basi bila shaka tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa hatudhulumiwi tena na leo. Focus yetu isiwe kuzuia risk bali njia za kufanya ili kui-manage.

Kila Mtanzania ajiulize, ni kwa namna gani yeye binafsi atatumia fursa zinazojitokeza kutokana na kuhuishwa kwa uhusiano baina ya Tanzania na Kenya...

Tumetumwa kupeleleza nchi ya ahadi, tuwe na akili kama za Joshua na Kalebu - tusiwe na mawazo ya kutokujiamini na kujiona mapanzi kama wale wengine 10
 
tumeruka mkojo tumekanyaga mavi.
Leo kademka yeye,,,,,Uhuru kamdemsha tumeexchange Mahindi kwa makampuni
Very sad Mkuu... ...how comes mahindi Vs ardhi,madini,utalii....how much will earn from such kind of investment compared to the approaches tulizochukua miaka 5 iliyopita?kuna baadhi ya mambo asiyaguse kabisaa....
1.sheria za madini zilizopo
2.utalii
3.vibali vya kufanya kazi nchini
4._______
Naona ataaribu kabisaa.......
 
Nachelea kusema waliofanya maamuzi JPM apelekwe Nairobi wafuatiliwe japo haijawa officially stated ila naiona point ya kuanzia ivi kweli Kenyata at National Level anaongelea mambo ya mahindi?? Hii move sioni kama ina win win situation sisi tumewakaribisha wafanye invest kwenye madini ila wao wameruhusu tuuze mahindi hahahaha
 
Nimeandika Uzi humu ndani watu wakatoka mapovu.

Yaani Matatizo waliyotaka wenyewe waje kusaidiwa huku, nilishangaa Rais aliposema Tanzania ina Ardhi anawakaribisha Wakenya, Akanichosha aliposema Tanzania ina madini wakenya waje, utadhani watu hatuijui Kenya.

Hivi Wakenya wangapi watakuja Tanzania kuwekeza Madini Tanzania tusiwaite wachimbaji wadogowadogo,
Ninacho fahamu ni samia ni rais anaye penda kuzingatia taratibu kwa hivyo mnao dhani wakenya wamealikwa tanzania kama wamealikwa nyumbani kwa samia basi tafakarini vizuri

Nadhani mnakumbuka hata kipindi cha kikwete walialikwa pia lakini walipo taka kuvuka mipaka ya mualiko wao walikipata walicho kipata

Sasa hapo mlitaka asemaje labda maana mnalalami kasana.

Msimfanye SAMIA hajui chochote na nyie ndio mnao jua zaid yake
 
Iko hivi kwa taarifa yako Wasukuma ndio wanaogoza kuwekeza kwenye migodi ya Kenya au unafikiri Kenya hakuna migodi?

Kuanzia Migori hapo kwenda mpaka kisumu kuna migodi kibao na wakazi wa huko ni wasukuma na wajaluo.

Sasa wewe sijui unataka wawekezaji kutoka wapi ndio waje wawekeze na mchanga wabebe

Hii nchi watu tunashindwa kujua kitu tunachokitaka..

Kwenye swala la uwekezaji na kukuza uchumi niko na mama.

Ila tutagombana kwenye democracy na ufisadi na katiba mpya.
Tunachotaka ni win-win agreement kwenye hizo investments.....sio tu kufurahia kila uwekezaji.......

Ukijibu nitag.....
 
Kwenye ubinafsi ndio hapo napohofia tu maana sie watanzania ni social beings ila hawa wenzetu watakuja kutumia ile generous calibre yetu kutuumiza! It has nothing to do na uoga ila curiosity tu maana tulishaliona hili hata kwenye professionalism.

That is what selfish guys do na ndio maana wazee Jakaya na Magu waliamua kuwakazia at some point. Ngoja tuone tukiwakaribisha mpaka sebuleni hali itakuwaje maana kuna kundi linataka kuonja sumu kwa kuilamba ila nachowaza kwa ukabaji wao mpaka kwenye box la penati wakiingia kila sector watakao survive watakuwa akina Rostam, Dewji, Bhakresa and the like!
Wao huwa wanaweza hata kufanya "usanii" na "kamari" kwenye biashara kwa kutumia mkono wa serikali.

Tunakumbuka sekeseke la Indopower Solutions ambapo CEO wake Brian Mutembei alishikwa mkono na Balozi wa Kenya na akasaini provisional contract kununua 100,000 tonnes za korosho.

1620283517388.png



Baada ya hapo akawa na ujasiri kuanza kujinadi duniani kuwa ana korosho toka Mtwara; imagine mtu anaweza kupewa gov back-up kujaribu biashara akiwa hana mtaji wa kununua. Kama auction ile ingefanikiwa, jamaa angekuja na hela akanunua baada ya mkataba kuwa signed.

Jambo la gov back-up sisi kwetu tunalo?

Ndiyo tupate picha namna gani wenzetu wako aggressive hata kwa kujaribu na gov backing ipo. Wanajua biashara zote, safi na chafu (kama utoroshaji wa madini ya Tanzanite) na serikali yao inakaa kimya, maadam wallet za watu wao zinasoma.
 
Nimeandika Uzi humu ndani watu wakatoka mapovu.

Yaani Matatizo waliyotaka wenyewe waje kusaidiwa huku, nilishangaa Rais aliposema Tanzania ina Ardhi anawakaribisha Wakenya, Akanichosha aliposema Tanzania ina madini wakenya waje, utadhani watu hatuijui Kenya.

Hivi Wakenya wangapi watakuja Tanzania kuwekeza Madini Tanzania tusiwaite wachimbaji wadogowadogo,
Magufuli angemwita mwendawazimu. Hawa wakenya wametuibia tanzanite rubies na madini za vito zote kwa kununua magendo miaka toka 1960s. Nakumbuka walijaa pia kama wachimbaji wadogo hadi ikafanyika kusudi kuwatimua. Ndio leo uwaite kuwekeza? Si watabeba tena kupeleka kwao kimagendo kisha kuuza wao nje? Lets be serious..tumejenga ukuta mererani ila bado tanzanite inakwenda kenya kimagendo. Yaani huwezi kutrade na kenya bila wao kukuibia au kukulalia. Kuibiwa kwa maana ya kupunjwa na ukwepaji kodi kwa nchi yetu. Chini ya magufuli tumeona nguvu ya kodi yetu na mipango mizuri ikifanya mambo ya tija kwa mstakabali wa taifa letu.
Wakenya ni jirani na ndugu zetu ila tuishi nao kwa akili. Tukumbuke ule usemi wa kiswahili 'ukicheza na nyani utakula mabua'
 
Nina mashaka na Uwezo wa kuamua wa Rais wangu, au kuna kundi linalonunulika linamshauri, yaani kikubwa ambacho Kenya itaifanyia Tanzania ni kuruhusu Mahindi, alafu sisi tutaruhusu Masuala ya Anga, Utalii.

Wao Wanazuia Shirika letu la ndege kufanya Kazi,ila lao wanataka tulihusu, Eti Mtalii afike Kenya ndio aje Tanzania, Kwa nini asianze Tanzania

Mama alipaswa amuache Kabudi kwenye wizara ya mambo ya nje aisee,
Kama hayo waliyikubaliana yataruhusu haya.....itakuwa ni pigo kubwa sans
 
Jirani akusaidie kuzuia mwizi kwako, mwizi anayeshirikiana na wanao Huyo jirani anaanzaje? Tanzanite haiwezi kuibiwa bila wa TZ wenyewe kubariki mkenya wacha afaidi mpaka tutakapo amka kweli. Tumelala sana bana nasi.
Mkuu, hata ukiwa macho, kuna mpunga wa Escrow au EPA ulipigwa kwa ushirikiano na wakubwa; utazuiaje na wenye mamlaka washafanya maamuzi?

Kenya wanajua biashara safi na chafu; kitu kama bangi wao ni haramu isiyo haramu maana inakwenda Somalia, hata wahamiaji haramu toka Ethiopia, wao hawana noma, maadam wamepata chao, wanawapa access kuvuka kuingia kwetu.

Tuna jirani ambae yeye hela ikija mkononi lazima akamate. Anyway, tumpe mkuu wa nchi the benefit of the doubt, huenda this time sisi ndani tutaacha kupiga deal na wao "majirani na ndugu" nao huenda wataacha.
 
Marekani yenyewe unayoisema ndio inaongoza kuwa na wafanyakazi wa kigeni kuliko nchi zote duniani

Ndio nchi inayoongoza kununua bidhaa toka China kuliko nchi zote za America.

We jamaa vipi wewe uwekezaji gani unautaka?
So what...marekani anafanya hivyo kwa faida yake....

Tunataka win-win investments na si kingine.....na hapa si kwa mkenya tu hata kwa nchi nyingine...si mchina,mUSA,mUk,,Mfrance

Sa hivi atutaki business as usual....si politics wala economics....Tunachotaka ni win-win agreements in every investments....
 
Nina mashaka na Uwezo wa kuamua wa Rais wangu, au kuna kundi linalonunulika linamshauri, yaani kikubwa ambacho Kenya itaifanyia Tanzania ni kuruhusu Mahindi, alafu sisi tutaruhusu Masuala ya Anga, Utalii.

Wao Wanazuia Shirika letu la ndege kufanya Kazi,ila lao wanataka tulihusu, Eti Mtalii afike Kenya ndio aje Tanzania, Kwa nini asianze Tanzania

Mama alipaswa amuache Kabudi kwenye wizara ya mambo ya nje aisee,
na hayo mahindi kuanzia mwakani wakenya ndo wazalishaji wakuu wataanza kulima tanzania vijana wakitanzania waendelee kudemka mjini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom