Rais Samia, Unakotupeleka Utalaaniwa na Vizazi Vyote Vya Tanzania Na Dunia. Nchi Hii Haijawahi Kuwa na Ugomvi wa Kidini, Wewe Unauanzisha kwa Nguvu

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,096
Nchi hii, pamoja na mapungufu mengi, hatujawahi kuwa na ugomvi au uhasama wa kidini. Ndiyo maana kuna watu utasikia anaitwa Abel Abdalah, wengine utamsikia akiitwa Petro mume wake Khadija, au Abdallah mumewe Rozaria. Nilipoenda kumtembelea rafiki yangu bruda Peramiho, nilishuhudia shekhe amealikwa kwenye sherehe ya mahafali ya waseminari, naye baada ya kutoa salamu fupi, alianzisha sala ya Baba Yetu. Hivyo ndivyo tulivyoishi Watanzania kwa miaka mingi. Wapo baadhi ya wakristo ambao walitamani majina ya kiislam, unamsikia mktisto anaitwa Juma Joseph. Kulikuwa na Askofu Mkuu alikuwa akiitwa Mario Abdallah Mgulunde.

Katika nchi hii, wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, nani aliwahi kuwa maarufu kumzidi Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa? Nani anaweza kusimama na kusema Nyerere alikuwa na rafiki wa karibu zaidi kumzidi Kawawa? Rashid Kawawa alikuwa muislam, Nyerere mkristo, lakini walikuwa marafiki wakubwa. Kama nchi hii ingekuwa na udini, Nyerere si angemweka mkristo mwenzake kwenye nafasi ya karibu naye? Nyerere alipoamua kung'atuka, alimwachia nchi Ali Hassan Mwinyi, muislam. Yote ni kuonesha kuwa nchi hii ni yetu sote.

Nyerere aliwahi kumfukuza nchini padre mkatoliki kwa kutoa kauli aliyodai kuwa iliidhalilisha nchi, sikuwahi kusikia aliwahi kumfukuza shekhe.

TEC wamewahi kutoa nyaraka kukemea maovu yaliyotendwa na serikali nyakati mbalimbali, wakati wa utawala wa Mkapa, Kikwete, Magufuli, na sasa Samia. Mbona hizo nyakati zote nyingine hatukuwahi kusikia mashekhe wa BAKWATA wakilalamika, kwa nini iwe leo? Kwa nini kila kosa linalofanywa na vyombo vya Serikali, mashekhe wa BAKWATA wanaligeuza kuwa ni shambulio dhidi ya uislam? Kwani Samia au Serikali ndiyo uislam?

Lolote baya likitokea kwa nchi hii, lawama atazibeba Samia. Samia hakuwahi kuzuia utekaji na mauaji ya wanaomkosoa. Samia hakuwahi kukemea wala kuzuia mauaji ya maelfu ya vijana waliouawa kufuatia uchaguzi bandia. Samia hakuwahi kutengeneza mazingira ya uchaguzi huru na wa haki. Na sahizi, yupo kimya wakati kuna washenzi wanaotaka nchi iingie kwenye ugomvi wa kidini.

Huko nyuma, hawa washenzi wanaojiita mashekhe wa BAKWATA, waliwahi kuhamasisha washenzi wenzao, wakachoma makanisa, wakavunja bucha za kitimoto, wakamwua padre, wakavunja mabaa, LAKINI Rais Mwinyi, na Rais Kikwete, kila mmoja kwa wakati wake walikemea na kuchukua hatua dhidi ya washenzi hawa. Leo Samia yupo kimya wakati mashekhe washenzi wa BAKWATA wakitishia kuwakata vichwa watu wasiowataka.

Vyombo vya Ulinzi na Usalama, kuweni makini sana, kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kuiingiza nchi hii kwenye ugomvi wa kidini, hata kama Amiri Jeshi Mkuu atakuwa ameubatiki uovu huo.

Kwa upande mwingine, sisi wananchi na waumini wa dini mbalimbali, wakati tukiwaheshimu viongozi wetu wote wa dini, tuwatenge, tuwakatae kabisa, na ikiwezekana tuwaadhibu, hawa mashekhe uchwara wanaotaka kutugombanisha waislam na wakristo, kwa maslahi yao binafsi. Wao wanavyozidi kutengeneza chuki, sisi tuimarishe umoja na upendo miongoni mwetu bila ya kujali tofauti zetu za kiimani.

Kwa sasa adui yetu mkuu ni wadhulumaji wa haki, jitihada zetu za kuipambania haki, zituunganishe na kutuweka pamoja. Ndugu zetu kwa maelfu wameuawa, wauaji hawakuchagua dini, hawakuchagua kabila, wala jinsia, nasi tusimame hivyo hivyo kulazimisha uwajibikaji kwa watawala.
 
Tatizo ndiyo uwezo wake ulipoishia
Kama ndio uwezo wake ulipofikia kwanini Chama chake na vyombo vingine vya dola hawaoni kwamba sasa hivi ndio wakati mzuri wa kuweka sirikali ya mpito, na kubadili Katiba ili shida kama hizi
 
Mimi mnioneshe tamko moja tu la BAKWATA wakikemea maovu wanayotendewa Waislamu achilia mbali Watanzania.
 
Kama ndio uwezo wake ulipofikia kwanini Chama chake na vyombo vingine vya dola hawaoni kwamba sasa hivi ndio wakati mzuri wa kuweka sirikali ya mpito, na kubadili Katiba ili shida kama hizi
Chama chake na Hivyo vyombo vyote vipo chini yake yaani wote ni wateule wake.hawana ubavu wa kumwambia ukweli lazima wampe ushauri unaoelekea na yeye anavyopenda.Njia iliyobaki ya kupata katiba Bora Tz ni Maandamano yasiyo na kikomo kuwalazimisha watawala kutii Kwa lazima matakwa ya wananchi na siyo kubembelezana.
 
Kama ndio uwezo wake ulipofikia kwanini Chama chake na vyombo vingine vya dola hawaoni kwamba sasa hivi ndio wakati mzuri wa kuweka sirikali ya mpito, na kubadili Katiba ili shida kama hizi
Wanaogopa kuadhibiwa watakula wapi mkuu, si umeona tulia alivyoporomoshwa kutoka usipika hadi back bencher kukaa na baba levo!.
Samuya ana chuki sana kwa wenye mtazamo tofauti na wake, mbaya zaidi akili hana!.
 
Samia ni Rais wa nchi gani? Amechaguliwa kwa uchaguzi upi? Huyo ni kiongozi wa genge la KIGAIDI ambalo linatawala Tanzania kwa MABAVU. Muda wao unahesabika
 
Nadhani kama kulaaniwa,hii itakuwa ni mara yake ya 70 kulaaniwa
 
Nakubaliana nawe nawe, hana uhalali wa kuitwa rais
Samia ni Rais wa nchi gani? Amechaguliwa kwa uchaguzi upi? Huyo ni kiongozi wa genge la KIGAIDI ambalo linatawala Tanzania kwa MABAVU. Muda wao unahesabika
. Huyu ni mwovu kuliko jambazi anayetumia silaha kutisha ili ukimbie halafu apate nafasi ya kuiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…