Rais Samia: Tutaanza kutoa Tsh 10,000/= kwa siku kwenye pesa za kujikimu (Boom) kwa wanachuo

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Fuatilia matangazo ya mbashara (moja kwa moja) kutoka Ikulu Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anazungumza na wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (TAHLIFE) leo tarehe 11 Februari 2023.



********* *******

Rais Samia ameanza kwa kumshukuru Waziri wa Elimu, Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara hiyo kwa kutekeleza wajibu wao kikamilifu.

Zamani tulisema vijana ni taifa la kesho, lakini siku hizi tunasema vijana ni taifa la leo maana wanachangia sana kwenye uchumi wa nchi.

Katika kuthibitisha hilo, katika teuzi, Ni vijana ambao wanajenga taifa leo ndio wanachaguliwa. Vijana wahakikishe wanajipanga kulitumikia taifa.

A1C12700-AC4A-4B46-8560-293FCD6B7760.jpeg

Amewataka vijana kuifahamu vizuri historia ya nchi yetu ili wawe na uelewa mpana wa masuala anuai yanayohusu nchi. Hapo watakuwa ni vijana wazuri wa taifa hasa kwenye kulinda tunu za taifa.

Suala lingine ni kuhusu mwelekeo wa nchi yetu na aina ya taifa tunalotaka kujenga, ambapo kujitegemea ndio uhuru wa kweli. Ukijitegemea mwenyewe, una kitu chako mwenyewe, unaweza kufanya jambo lolote unalotaka. Kujitegemea huku huanza na mtu mmoja mmoja hivyo hii ianzie kwa wasomi wetu.

Vijana wengi hatukuwatayarisha kujiajiri baada ya kumaliza chuo kikuu. Wizara iandae mitaala mipya itakayowajengea vijana uwezo wa kujitegemea baada ya masomo. Mchakato umefikia pazuri. Vyuo vizalishe vijana wenye uwezo wa kutatua changamoto, siyo kuongeza changamoto za ajira ndio maana tumeanza upande wa TEHAMA.

Tumshukuru Marehemu (Hayati Magufuli), wakati wa Korona alisema kila mtu atoke kujitafutia, maradhi haya yalishusha kasi ya ukuaji wa uchumi kutoka 7 hadi 4. Hatukuanza pabaya. Matatizo mengine ni kutokuwa na usalama wa chakula, mabadiliko ya tabianchi pamoja na vita ya Urusi na Ukraine.

Pamoja na matatizo haya, hakuna mwananchi atakufa kwa njaa, tunayo akiba ya kutosha kwenye maghala. Hakuna uhaba, Serikali tumefungua maghala, tumetoa chakula. Tunapozungumza sasa, tanzania tunajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100.

Kwa upande wa sekta ya Elimu, yote yaliyosemwa ni ya kweli, naongeza moja la vijana kuwa na sifa ya kwenda chuo lakini wazazi hawana uwezo. Tumezungumza na mabenki, na NMB wametoa bilioni 200 kwa wazazi ambao mishahara inapitia hapo watatoa mkopo kwa riba nafuu. Tumezungumza pia na mataifa mbalimbali kurudisha scholarships mbalimbali ili vijana wa kitanzania wanufaike.

Tumetoa kipaumbele cha kwanza kwenye kilimo, tuna kila kitu, tutazalisha kwa uwezo wa Mungu. Tumefungua nchi na kualika wawekezaji waje Tanzania. Upande wa utalii, tumefanya jitihada na sasa idadi ya wageni wanaokuja Tanzania ni kubwa mno.

Kuhusu nishati, serikali tumejipanga kuhakikisha umeme unatulia. Tuna mradi wa bwawa la Nyerere ambapo tayari tumefungulia maji yaingie, pengine katikati ya mwaka huu au mwezi wa 9 tunaweza kuwasha mashine kwa majaribio. Tunaenda kuongeza umeme wa kutosha, tunajipanga Tanzania iwe power pool iweze kuuza kwenye nchi zingine.

Upande wa maji, ikifika 2025 tutakuwa tumepeleka asilimia 95 mjini na zaidi ya asilimia 80 vijijini.

Suala la boom, tutaanza na 10,000/= kwa siku. Pia, tunafikiria na kuweka kwenye mipango yetu kuwa mikopo itolewe kuanzia ngazi ya cheti hapo baadae.

Kasi ya kuzaa inakuza mahitaji kwenye elimu, maji, afya, kilimo, chakula n.k. Mnaofaidika na mikopo mlipe baada ya kupaka kazi ili mdogo wako apate pia mkopo. Mkijikausha hamtakuwa wazalendo, wanangu mkitoka hapa rudisheni hizo pesa. Serikali hatuchapishi pesa kila mwaka, bali tunakusanya kwenye kodi. Na tulkiweka tozo mnaanza kelele, oooo bibi Tozo huyooo.. kwa hiyo, rushisheni ili wenzenu pia waje kupata

Nawaasa, jiepusheni na tabia mbaya, uasherati, madawa ya kulevya, jiheshimuni. Madawa ya kulevya hatayawafikisha pazuri. Angalieni vizuri.

Pia, acheni kuiga ya nje, ishini kwa kufuata mila na desturi zetu. Niwaombe sana wanangu, muwe mabalozi wa wenzenu, walindeni wenzenu. Hii haki inayosema ya kibinadamu (ushoga) tusiige na kuona ni mambo ya kawaida. Tuna haki nyingi sana, hizi hazi zingine tafadharini lindeni wadogo zenu, ninyi Mungu amewaepusha, vinginevyo tutakuja kuwa taifa la ajabu. Tushini kwa mila na desturi zetu.

Mwenyezi Mungu awashushie wote baraka, mambo ya nitakufa juu yako yatawaharibia maisha. Kasomeni, Mungu awape baraka, someni kwa bidii.

******** ******

Taarifa kutoka Ikulu
FB_IMG_1676118682582.jpg
 
Rais R kubwa na r ndogo naoa kama kichekesho...Kwanini asiadress moja kwa moja Mh Rais Dr Samia au Rais wa tahiliso?
 
Rais Dkt. Samia anajitahidi sana kukutana na makundi mbalimbali ktk jamii, nashauri aendelee na mwendo huo huo wa kukutana na kuzungumza na makundi hayo, najua bado mengi ila afanye utaratibu wa kukutana na idara mbalimbali za serikali na kufanya mazungumzo nao.
 
Changamoto ya udangaanyifu kwenye elimu yetu inahitaji mikakati madhubuti.

Udanganyifu unao fanywa na wanafunzi vyuo vikuu na hata shule za sekondari ni sumu na bomo kubwa kwa Taifa letu, hatuna budi kuja na mikakati madhubuti.
Suala la udanganyifu ni pana, vidole vinyoshwe kwa wote wanaohusika bila ubaguzi.
 
Rais Dkt. Samia anajitahidi sana kukutana na makundi mbalimbali ktk jamii, nashauri aendelee na mwendo huo huo wa kukutana na kuzungumza na makundi hayo, najua bado mengi ila afanye utaratibu wa kukutana na idara mbalimbali za serikali na kufanya mazungumzo nao.
Hatua kwa hatua, taifa linajengwa.

Tusonge Mbele Kwa Pamoja.
 
Rais Dkt. Samia anajitahidi sana kukutana na makundi mbalimbali ktk jamii, nashauri aendelee na mwendo huo huo wa kukutana na kuzungumza na makundi hayo, najua bado mengi ila afanye utaratibu wa kukutana na idara mbalimbali za serikali na kufanya mazungumzo nao.
Tanzania makundi mengi ni YA MCHONGO.

Ndio maana MATATIZO ya KIJINGA JINGA nchi hii HAYATAISHA.
 
Kwakweli Serikali ya DR. SSH Inagusa nyoyo za ss wananchi Ina focus fulani hivi tamu balaa na utekelezaji wake Ni faster faster, kila kinacho ongelewa tayari kinakuwa kimesha andaliwa modality yake ya utekelezaji. Mm na ndugu zangu tunasema hivii Kura yetu DR. SSH 2025 Unayo na kwaheshima yako kuanzia 2024 Kura Ni kijani mwanzo mwsho.
Kazi iendelee
 
Elfu 10 itaongeza idadi ya wanywa gongo, wanaobet, wanaodanga na wanaocheza pool.
 
Back
Top Bottom