Rais Samia tusaidie tusiporwe ardhi yetu na serikali yako

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
237
239
Ni mgogoro wa muda mrefu toka 1974 wa kipande cha ardhi cha hekari 67 uliotatuliwa na Kumalizwa na Mheshimiwa Lukuvi aliyekuwa Waziri wa ardhi. Taasisi ya kilimo Uyole ilishindwa kuwalipa fidia wananchi wa Sae jijini Mbeya zaidi ya 300 katika ardhi waliyokuwa wakiitumia tokea mababu kwa kilimo, matambiko na makazi.

Kwa kuona kilio cha muda mrefu cha wananchi mwaka 2020 waziri Lukuvi aliwarudishia eneo lao ambapo wananchi wamejenga nyumba za makazi. Sasa ajabu ni kwamba eneo hilo limevamiwa na kikosi cha jeshi (JKT) wakiharibu mazao ya vyakula na kuchimba mtaro ili kujenga uzio wa eneo hilo kwa madai kwamba wametumwa na Kilimo Uyole.

Wananchi nikiwa mmoja wao hatujaridhika na maelekezo ya Mkuu wa Wilaya kwamba tutalipwa fidia kwa sababu mgogoro ulishaisha na wananchi wamefanya maendelezo makubwa na wanachi walichangishwa zaidi ya shilingi milion 30 ili kupimiwa na kupewa hati za viwanja vyao katika eneo hilo. Tunajua siku zote fidia ya serikali haiwezi kusaidia kupata ardhi YENYE THAMANI sawa na ile wanayoichukuwa.

Tunaomba mheshimiwa Rais tusaidie. Tunajua mbunge wetuTulia analijua sana hili waziri Bashe analijua sana hili na kwenye maadhimisho ya nanenane alikuomba uwapatie eneo hilo. wananchi wa hapo tumeumizwa sana na uamuzi huo wa kutusaidia na kutuhurumia ni wewe. Tusaidie kuokoa ardhi yetu isiporwe na serikali yako.
 
Serikali hii ipo bize sana na matajiri. Kiufupi msaada ni kama tajiri kuingia Mbinguni
 
Halafu asaidie Mbopo Madale Mpigi magohe Msumi na maeneo ya jirani....DDC inadai ni maeneo yake
 
Back
Top Bottom