Hivi karibuni kulifanyika mkutano kati ya wadau mbalimbali ili kutatua hili tatizo. Walikuwepo wenye kumbi za starehe,wakazi wa sehemu hizo wanaolalamika,kamati ya mazingira ikiongozwa na madiwani na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mtanda.
Walikubaliana kwamba wenye kumbi wachukue hatua za kupunguza kelele katika sehemu hizo ili wakazi waweze kulala bila kubughudhiwa na kelele za muziki baada ya saa sita usiku.
Mojawapo ya maazimio ni kuweka sound proof system na pia kuomba leseni ya Night Club ambayo ina vigezo vyake.
Kila moja akitimiza wajibu wake hili sio tatizo kubwa.Tatizo ni pale wenye kumbi wanapokataa kwa makusudi au kutojali kufuata makubaliano.
Mkuu wa Wilaya ni mchapa kazi hivyo majungu hayawezi kusaidia kwenye hili.
Kuwa wa mjini born town haina maana ya kutofuata sheria na kanuni tulizojiwekea.