Rais Samia, tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi

Mahali nilipo mfuko wa
cement ni tsh.23,000/-
Nondo mm 12 =21,000/-
Bati futi 8 gauge 32 = 18,000/-
futi 6 -//-. 17,000/-
Misumari kilo 1 = 8,000/-
Baadhi tu ya vifaa
Mkuu ni sawa na maeneo ya mkoa wa Kagera, yaani huko vifaa vya ujenzi ni anasa
 
Mahali nilipo mfuko wa
cement ni tsh.23,000/-
Nondo mm 12 =21,000/-
Bati futi 8 gauge 32 = 18,000/-
futi 6 -//-. 17,000/-
Misumari kilo 1 = 8,000/-
Baadhi tu ya vifaa

Duh! Tutajenga kweli jamani 😱 Mh Raisi alitazame hili, vifaa viko juu mno.
 
Mkuu unadhani kwa hizi bei wauzaji wanapata faida na kufaidika ?

Wenye viwanda wapunguze, ili wafanyabiashara nao wauze kwa faida.


Viwandani wakiuza kwa bei ya 8000, wafanya biashara wakatuuzia kwa 12000 mbona wanapata faida nzuri tu, ukitoa transport bado faida wanapata nzuri.
 
Hii tabia ya wanasiasa, KWA MASLAHI YAO BINAFSI, kutoa monopoly kwa kampuni au muuzaji mmoja inatunyonya raia.
By 2010, cement toka Pakistan iliuzwa nafuu kuliko ya Twiga (Wazohill)
Mamlaka zimeweka mifumo ya kinyonyaji kuliko hata wakoloni wenyewe wangelikuwepo.
Teknolojia inakuwa zaidi, ila ndio ukandamizwaji unaongezeka.
 
Mama yangu mama samia usiingilie hizi biashara kwa ushauri wangu.

Hawa wanaopandisha hivi vitu ni watanzania pia wanapata tonge lao hapo.

Haiwezekani tushare hasara au matatizo.

Yani kwa kuwa life gumu kwa mteja ati na mimi nilazimishwe kushusha bei hapana.

Huyu anaepandisha bei ni mtanzania pia hivyo anafaidika.

Kwa kuwa maduka yapo menngi yanayouza bidhaa kama hizo uwanja ni kwao wafannya biashara waangalie fursa zilizopo kama mtu ataweza kushusha bei auze kwa pesa ndefu zaidi na sio kusema bei ishuke.
Bei unayouzia si ihali yako bali nawe unalazimishwa kutokana na nguvu ya soko, ukizunguka mtaa au mji mzima bei ya siment, sukari, chunvi, nondo, misumari, mabati wote wana bei sawa, unadhani walikaa kikao kupanga bei?
 
Haya mambo ya protectionism ndo yanaumiza raia, unazuia soko huru la bidhaa kulinda viwanda vya watu wachache......unafaidisha watu wasiozidi laki tatu ili kuumiza mamilioni. Chukulia mfano sementi na nondo kuvisafirisha kutoka Dar kwenda Musoma ni ghali zaidi kama bidhaa hizo zingepatikana kutoka kenya au uganda. Bila kuruhusu soko huru la bidhaa tutaumiza sana wananchi kwa kufikiri tunawasaidia kwa kulinda viwanda vya wachache......
 
Mahali nilipo mfuko wa
cement ni tsh.23,000/-
Nondo mm 12 =21,000/-
Bati futi 8 gauge 32 = 18,000/-
futi 6 -//-. 17,000/-
Misumari kilo 1 = 8,000/-
Baadhi tu ya vifaa
Daah...ni cement gani hii inauzwa 23000
 
Vijana mkumbuke mambo ya msingi mnapopata fursa ya kuongea na viongozi.
Nyie bodaboda, mama ntilie na machinga mjue wengi wenu mmepanga nyumba za watu, kwa bei hizi za vifaa vya ujenzi, je mmnatarajia kurudi vijijini kujenga nyumba za miti na nyasi?
 
Haya mambo ya protectionism ndo yanaumiza raia, unazuia soko huru la bidhaa kulinda viwanda vya watu wachache......unafaidisha watu wasiozidi laki tatu ili kuumiza mamilioni. Chukulia mfano sementi na nondo kuvisafirisha kutoka Dar kwenda Musoma ni ghali zaidi kama bidhaa hizo zingepatikana kutoka kenya au uganda. Bila kuruhusu soko huru la bidhaa tutaumiza sana wananchi kwa kufikiri tunawasaidia kwa kulinda viwanda vya wachache......
Ukimuliza mtunga sera, je ni viwanda gani, vyenye uwezo gani anavyovilinda kwa nguvu hivyo hawezi kukupa jibu la maana.
Tuna sera za protectiosm kana kwamba viwanda vimetapakaa kila kichochoro.
Watunga sera watuambie pia, je hivi viwanda wanavyovilinda miaka na miaka havina mpango wa kuuza bidhaa nje? Wapi? Na kodi za malighafi ni stahiki?
Miaka na miaka CEO hawawazi kuboresha teknolojia kwa kuwa wanakingiwa kifua na serikali huku wananchi wakiangamia.
 
Kwakweli
Nondo mm12 = tshs 19,500
Cement =tshs 19000/ 19,500
Tofali moja 1200

Toeni na bei elekezi ya kokoto kwa cm3 / m3
Mchanga
Mawe
Wananchi tunahangaika..
Waruhusu Cement ya Uganda na Kenya kwa mikoa ya kanda ya ziwa na kaskazini..

Kwanini mnampa Tanga cement monopoly ya soko?
Ruhusa ipewe Dangote azalishe kwa wingi ili kuondoa hii shida
Mbona nondo bora yenu. Huku nondo 12mm ni 22,000
 
Kweli kabisa hili liangaliwe kwa umakini, gharama za vifaa vya ujenzi zimekuwa juu sana
 
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo.

Kama bati futi 10 la gauge 32 ni limefikia Tsh. 20,000/- tutaweza kujenga kweli. Tafadhali washauri wa Rais tunaomba mlifikishe hili, ni hatari huku vijijini.

Karibu watalaamu tushauriane ujumbe umfikie Mh. Rais. Ahsante sana.
Cement kaskazini 16000
Wacha tuuu mkulima ataendelea kupambana na hali yake mpaka akome
 
Bei unayouzia si ihali yako bali nawe unalazimishwa kutokana na nguvu ya soko, ukizunguka mtaa au mji mzima bei ya siment, sukari, chunvi, nondo, misumari, mabati wote wana bei sawa, unadhani walikaa kikao kupanga bei?
Hawajakaa kikao.

Na kama hawajakaa kikao kila mtu ana uhuru wa kuweka bei atakayo.

Hiyo ni fursa kwa wengine.

Usilazimishe watu kuuza kwa bei unayotaka wewe mkuu
 
Wenye viwanda wapunguze, ili wafanyabiashara nao wauze kwa faida.


Viwandani wakiuza kwa bei ya 8000, wafanya biashara wakatuuzia kwa 12000 mbona wanapata faida nzuri tu, ukitoa transport bado faida wanapata nzuri.
Kwa nini uwasemee kuwa wanapata faida nzuri ?

Mbona bei ya simu inatofautiana baina ya duka na duka kwa nini iqe kwenye cement ?

K/koo utaambiwa simu laki mbili,ukienda sehemu ingine utaambiwa laki mbili na nusu.

Mtu anauza kwa anavyojisikia na anavyoona inamlipa,hii ndio biashara.

Kwa nini munamkadiria mtu kwamba kwa bei fulani anapata faida nzuri wakati yeye ndo muuzaji anayejua vipi auze apate kulisha family na kuendeleza biashara ?

kama akishusha bei akauza 12000 kuna mambo kibao yanamkabili ambayo hayajashuka bei.

Wanaaouza bei kubwa vifaa hivyo sio kwamba hiyo pesa kazi yao kununua na kuuza,kumbuka wanafanyia mambo mengine ambayo wanapaswa watoe pesa hizi hizi unazonunua vifaa kwao.

Hiyo pesa yako ndio inamfanya aishi,ukisema apunguze bei maana yake unataka kutuambia kuwa na sehemu zingine bei vitu vishuke ili hii faida chache ya sasa hivi itoshe kukidhi mahitaji hayo.

Hii unaona imekaaje mkuu ?
 
Back
Top Bottom