Rais Samia, tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi

RUSHAMBYA

Member
Dec 2, 2015
40
32
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo.

Kama bati futi 10 la gauge 32 ni limefikia Tsh. 20,000/- tutaweza kujenga kweli. Tafadhali washauri wa Rais tunaomba mlifikishe hili, ni hatari huku vijijini.

Karibu watalaamu tushauriane ujumbe umfikie Mh. Rais. Ahsante sana.
 
Kwakweli
Nondo mm12 = tshs 19,500
Cement =tshs 19000/ 19,500
Tofali moja 1200

Toeni na bei elekezi ya kokoto kwa cm3 / m3
Mchanga
Mawe
Wananchi tunahangaika..
Waruhusu Cement ya Uganda na Kenya kwa mikoa ya kanda ya ziwa na kaskazini..

Kwanini mnampa Tanga cement monopoly ya soko?
Ruhusa ipewe Dangote azalishe kwa wingi ili kuondoa hii shida
 
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo.

Kama bati futi 10 la gauge 32 ni limefikia Tsh. 20,000/- tutaweza kujenga kweli. Tafadhali washauri wa Rais tunaomba mlifikishe hili, ni hatari huku vijijini.

Karibu watalaamu tushauriane ujumbe umfikie Mh. Rais. Ahsante sana.
Vijana walipoenda Nyamagana stadium wakaishia kutoa ng'ombe tu
 
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo...
Mama yangu mama samia usiingilie hizi biashara kwa ushauri wangu.

Hawa wanaopandisha hivi vitu ni watanzania pia wanapata tonge lao hapo.

Haiwezekani tushare hasara au matatizo.

Yani kwa kuwa life gumu kwa mteja ati na mimi nilazimishwe kushusha bei hapana.

Huyu anaepandisha bei ni mtanzania pia hivyo anafaidika.

Kwa kuwa maduka yapo menngi yanayouza bidhaa kama hizo uwanja ni kwao wafannya biashara waangalie fursa zilizopo kama mtu ataweza kushusha bei auze kwa pesa ndefu zaidi na sio kusema bei ishuke.
 
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo...
Halafu lile zumbukuku kwenye bajeti halikuondoa tozo na kupunguza kodi kwenye vifaa vya ujenzi.
 
Mama yangu mama samia usiingilie hizi biashara kwa ushauri wangu.

Hawa wanaopandisha hivi vitu ni watanzania pia wanapata tonge lao hapo...
Haimanishi kwamba wafanyabiashara ndio washushe bei za vifaa bila serikali kushusha kodi za vifaa hivyo. Serikali ikipunguza kodi ya vifaa vya ujenzi vinaingia kutoka nje na vinavyotengenezwa hapa nchini bila shaka hata wafanya biashara watakuwa na unafuu kwenye kodi hivyo nao kupunguza bei kwenye biashara zao.
 
Yaan hata hujui nini kinasababisha bei kupanda ama kushuka umecoment ilimradi umecoment
Mkuu mimi nimetoa maoni.

Kama nakosea unaona kuna haja ya kunielimisha unanielimisha ndio lengo la JF hatushindani tunaelimishana.

Mwaga nondo tuelimike
 
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo...
Mimi naona tatizo kwenye habari nzima ya kumtaka rais aangalie kila kitu kama nchi haina mifumo.

Wananchi wanatakiwa kujipanga zaidi kimfumo, sio kila kitu kulalamika kwa rais.

Kwa mfano, kuna vikundi vya wanunuzi wa bidhaa za ujenzi vinavyofanya uchunguzi kuhakikisha bei hizi hazipatikani kwa ulanguzi? Kuna mbunge aliyepewa kazi ya kufuatilia chanzo cha tatizo na kuweka ufumbuzi wa kisheria kupitia bunge?

Rais ana sehemu yake kwenye utatuzi wa haya matatizo, kwa mfano, ameongea na Dangote kuhusu kuendeleza uwekezaji wa Dangote nchini. Lakini je, wananchi wamejipanga vipi zaidi ya kulalamika rais aingilie?

Rais hawezi kuwapo kila sehemu. Rais hawezi kusikia kila lalamiko. Na hata akisikia kila lalamiko, rais hana majibu ya maswali yote.Kuna maelfu na maelfu ya watu wanalia rais aingilie hili na lile. Hawezi kujigawa asikilize wote.

Inabidi tujipange kimfumo zaidi.
 
Mkuu, naomba uorodheshe vifaa vyote. Mfano, cement iko juu sana, nondo pia iko juu n.k
Mahali nilipo mfuko wa
cement ni tsh.23,000/-
Nondo mm 12 =21,000/-
Bati futi 8 gauge 32 = 18,000/-
futi 6 -//-. 17,000/-
Misumari kilo 1 = 8,000/-
Baadhi tu ya vifaa
 
Unataka Rais afanye nini?
Orodhesha mambo matatu unayofikiri Rais anaweza kufanya kushusha hizo gharama.
Mh. Rais mama Samia Suluhu Hassan tunaomba uliangalie upya suala la vifaa vya ujenzi kwani gharama zake ziko juu sana kiasi mtu wa kipato cha kawaida hasa wa kijijini hawezi kumudu gharama hizo hata kidogo.

Kama bati futi 10 la gauge 32 ni limefikia Tsh. 20,000/- tutaweza kujenga kweli. Tafadhali washauri wa Rais tunaomba mlifikishe hili, ni hatari huku vijijini.

Karibu watalaamu tushauriane ujumbe umfikie Mh. Rais. Ahsante sana.
 
Ungependa mfuko wa cement uuzwe shilingi ngapi ?
Mahali nilipo mfuko wa
cement ni tsh.23,000/-
Nondo mm 12 =21,000/-
Bati futi 8 gauge 32 = 18,000/-
futi 6 -//-. 17,000/-
Misumari kilo 1 = 8,000/-
Baadhi tu ya vifaa
 
Mimi naona tatizo kwenye habari nzima ya kumtaka rais aangalie kila kitu kama nchi haina mifumo.

Wananchi wanatakiwa kujipanga zaidi kimfumo, sio kila kitu kulalamika kwa rais.

Kwa mfano, kuna vikundi vya wanunuzi wa bidhaa za ujenzi vinavyofanya uchunguzi kuhakikisha bei hizi hazipatikani kwa ulanguzi? Kuna mbunge aliyepewa kazi ya kufuatilia chanzo cha tatizo na kuweka ufumbuzi wa kisheria kupitia bunge?

Rais ana sehemu yake kwenye utatuzi wa haya matatizo, kwa mfano, ameongea na Dangote kuhusu kuendeleza uwekezaji wa Dangote nchini. Lakini je, wananchi wamejipanga vipi zaidi ya kulalamika rais aingilie?

Rais hawezi kuwapo kila sehemu. Rais hawezi kusikia kila lalamiko. Na hata akisikia kila lalamiko, rais hana majibu ya maswali yote.Kuna maelfu na maelfu ya watu wanalia rais aingilie hili na lile. Hawezi kujigawa asikilize wote.

Inabidi tujipange kimfumo zaidi.
Sahihi kabisa.

Tatizo inaonekana kama waliopewa dhamana hawawezi kufanya maamuzi yoyote mpaka wapate maagizo kutoka kwa mtoa dhamana.

Inaonekana kama wanaogopa kufanya maamuzi ambayo yataenda kinyume na aliyeteuwa hivyo wanahofia kupoteza nafasi.

Inaonekana kama wapewa dhamana hawajiamini kwa nafasi zao wizopewa wazitumikie.

Watanzania wameuona huo mchezo ndio maana wanaamua kila kitu kulia na raisi.

Lakini inatakiwa wapewa dhamana warudishe moyo kwa wananchi kwa wao kufanya kazi wakijiamini,wakiwa wanatoa maamuzi kwa kuangia zaidi maslahi ya Nchi na sio mtazamo wa mteuaji.
 
Haimanishi kwamba wafanyabiashara ndio washushe bei za vifaa bila serikali kushusha kodi za vifaa hivyo. Serikali ikipunguza kodi ya vifaa vya ujenzi vinaingia kutoka nje na vinavyotengenezwa hapa nchini bila shaka hata wafanya biashara watakuwa na unafuu kwenye kodi hivyo nao kupunguza bei kwenye biashara zao.
Hata kama wakipunguza kodi serikali bado sio sahihi kumpangia bei muuzaji.

Hoja yangu ni kuwa maadamu wauzaji ni wengi waachwe kila mtu ajipangie bei yake anayoona itamlipa.

Watu wanaochukua mzigo wa simu nje wakileta hapa tanzania wanalipa kodi lakinii utashangaa tecno hiyo hiyo ukinunua k/koo laki mbili,ukienda sehemu nyingine laki tatu ama nne.

Ikipunguza kodi serikali ni jambo zuri,lakini kupunguzwa kwa kodi isiwe sababu ya kuwalazimisha watu washushe bei wakuu.

Hawa nao watanzania wanaouza,sio wahamiaji,wanataka kufaidika kama wanavyofaidika wengine.
 
Back
Top Bottom