Rais Samia: Tuache migongano, kusengenyana, uvivu na uzembe ili tufanye kazi za watu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha, leo tarehe 04 Machi, 2023

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Yapo mataifa ambayo yana watu wachache na ardhi yao ni ndogo lakini kwa kuwa uongozi wao ni bora yameendelea na furaha ndani ya Nchi ni kubwa, naamini sisi viongozi katika nafasi zetu tukibadilisha mitazamo yetu na kuacha mazoea tunaweza kuleta mafanikio makubwa.

Mitazamo yetu ikibadilika ni wazi migongano na mapambano sehemu ya kazi havitakuwepo, ubadhirifu utaisha, utendaji wa kazi utaimarika.

Niwasihi baada ya mafunzo haya twende tukaache migongano, kusengenyana, tukaaminiane, tuache uvivu, uzembe ili tukafanye kazi za watu kubwa zaidi tukaache dharau.

Tunawahudumia Wananchi wenye nchi, wala tusidharauliane wenyewe kwa wenyewe.

MAWASILIANO NDANI YA SERIKALI
Twende ngazi kwa ngazi, kosa kubwa tunalofanya ndani ya Serikali ni kudhani mawasiliano yamefanyika, tunasahau taarifa na mawasiliano.

Taarifa ni pale unapolisema jambo lakini haina maana itafika kule unapokusudia, ili ifike lazima kuwe na mawasiliano, pia hakikisha jambo lako limefika usidhani.

JIAMINI
Kama ukijiamini utafanikiwa, usipojiamini unajiwekea vikwazo mwenyewe, ukijiamini utapata mbinu, nendeni mkafanye kazi kwa kujiamini, aminini uwezo wenu, mnapofanya maamuzi sema haya ni maamuzi yangu.

Sema nimeamua haya kutoka na hali hii au hii, tusielekee kusema ‘haya ni maelekezo kutoka juu’, hiyo utakuwa haujiamini, fanya mamuzi kwa kujiamini na uwe tayari kutetea maamuzi yako
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha, leo tarehe 04 Machi, 2023

.....tusirude kure kwa zamani, ni amri kutoka juu".. ..
 
Mh Rais Samia amewaasa watumishi wa serikali kuhakikisha wanajiamini wanapotekeleza majukum yao.
Amesisitiza watende kwa kuzingatia sheria na wawe tayari kuwajibika kwa maamuzi hayo huku wakizingatia sheria zinasemaje.

Mh Samia amewaonya wasielekee kule tuliko toka kwa kudai ni amri kutoka juu. Hiyo ni dalili ya kutojiamini.
Ameyasema hayo akizungumza na mawaziri, manaibu waziri na makatibu wakuu na viongozi mbali mbali wa juu ktk serikali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha, leo tarehe 04 Machi, 2023

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Yapo mataifa ambayo yana watu wachache na ardhi yao ni ndogo lakini kwa kuwa uongozi wao ni bora yameendelea na furaha ndani ya Nchi ni kubwa, naamini sisi viongozi katika nafasi zetu tukibadilisha mitazamo yetu na kuacha mazoea tunaweza kuleta mafanikio makubwa.

Mitazamo yetu ikibadilika ni wazi migongano na mapambano sehemu ya kazi havitakuwepo, ubadhirifu utaisha, utendaji wa kazi utaimarika.

Niwasihi baada ya mafunzo haya twende tukaache migongano, kusengenyana, tukaaminiane, tuache uvivu, uzembe ili tukafanye kazi za watu kubwa zaidi tukaache dharau.

Tunawahudumia Wananchi wenye nchi, wala tusidharauliane wenyewe kwa wenyewe.

Kwa hiyo kila reshuffle ni semina. Mi naona ubadhirifu tu. Wangapi wamewekwa 'ngurdoto' hoteli na kulipwa, wangapi wameitwa eti kufundisha? Kwa nini usiteue watu tayari wana ujuzi wa uongozi? Unateua kina mwanafa vyeti feki unategemea nini? Hapo ni upigaji tu. Mwenyewe ulikua na maana gani kuwaambia wale kwa urefu wa kamba zao? Kama hukua na maana ya ulaji kila mtu anajua kwa nini hujasema kitu?
Viongozi unateua sio malaika na mwenyewe umesema hutaki ukali unategemea nini?
Cha kwanza kwenye teuzi ni uadilifu na uwezo. Hii inafuatiwa na usimamizi imara wa walio chini yako.
Eti '..sitaki nidhamu ya woga' wakati nidhamu ya woga kwa wezi na fisadi ina faida kubwa.
 
Mama anajielewa Sana tofauti na mazuzu wengi wa kijani,akiendelea hivi atakuja kua icon vizazi vingi mbele watamsoma Kama mama mageuzi maana hii inji Ina majitu ya kiume maoga Sana hayajui kujisimamia na kusimamia misamamo yao
#maendereohayanachamainjiwe
voices!
 
Ni kweli

Maana awamu ya 5 kila kitu walisingizia ni amri kutoka Juu kumbe urongo mtupu

Mfano uwepo wa akina Halima Mdee walisingizia ni amri kutoka kwa Shujaa, lakini mbona bado wanadunda bungeni hadi Kesho!!
Kwani awamu ya 5 Samia hakuwa miongoni mwa wale waliokuwa juu?

Najua utasema ooh yule jamaa alikuwa mbabe hamsikilizi mtu, ok, iweje sasa kina Mdee waendelee kuwepo bungeni mpaka leo, ikiwa uwepo wao haukuwa makubaliano yaliyomuhusisha Samia?
 
nitashangaa sana kuona mambo ya ajabu baada ya seminar hii!!!

nitashangaa kuwaona wanakuwa sehemu ya kulalamika badala ya kutatua kero za wananchi!!!

nitashangaa kuona hakuna ufanisi ktk utendaji wao!!!

nitashangaa kutokuona ubunifu!!!

nitawashangaa kuona hawajabadilika baada ya seminar hii!!!!

nitashangaa kuwaona wanashangaa badala ya kuchukua hatua!!!
 
Kwani awamu ya 5 Samia hakuwa miongoni mwa wale waliokuwa juu?

Najua utasema ooh yule jamaa alikuwa mbabe hamsikilizi mtu, ok, iweje sasa kina Mdee waendelee kuwepo bungeni mpaka leo, ikiwa uwepo wao haukuwa makubaliano yaliyomuhusisha Samia?
Alikuwa sana tu kwa sheria za Tanzania raisi ndio kila kitu
 
Utendaji safi kabisa naomba kujazia taasisi za serekali zijenge tabia ya kuaminiana, katika ripoti za kiuchunguzi au kiupelelezi miongoni mwa taasisi na taasisi, kunapotokea kuhofiana Inaleta mtafaruku mkubwa maana vyote vinakuwa ni vyombo halali vya umma kwa mujibu wa Bunge letu.
 
Back
Top Bottom