Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,390
- 5,310
Rais wa Tanzania Samia Suluhu leo akiwa anahutubia kwenye baraza la Eid amewatoa hofu mashehe na watanzania kwa ujumla kuwa Tanzania siyo uwanja wa majaribio na haitakubali kupokea chanjo ya Corona kabla ya kufanya utafiti wa faida na madhara ya chanjo hiyo kwa watanzania.
My take.
Chanjo ya corona aliyochanjwa Mbowe akiwa Dubai na akarudi mbio mbio kuhamasisha watanzania tuchanjwe haraka alijiridhisha madhara yake lini?
=====
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ugonjwa wa Covid-19 umeathiri dunia nzima, ili kukabiliana nao lazima kushirikiana na mataifa mengine lakini Serikali itaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo matumizi ya chanjo ya ugonjwa huo.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 14, 2021 katika baraza la Idd lililofanyika leo jioni katika viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.
Alizungumzia suala hilo baada ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) katika risala yao kutaka chanjo ya corona kutolewa kwa hiari huku Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi akiwataka Waislamu kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya nchini kuhusu kujikinga na ugonjwa huo.
“Nataka kuhakikishia kwamba tahadhari mlizitoa hapa juu ya chanjo na mengine zitafuatwa kikamilifu na Serikali yenu, hata hivyo hii haina maana kwamba tutapokea kila kitu tunacholetewa au kuambiwa la hasha lazima na sisi tujiridhishe kwa hiyo.”
“Hata suala la chanjo nalo tutajiridhisha kabla ya kuamua kutumia au kuacha kutumia, hivyo nawasihi Watanzania kutokuwa na hofu yoyote Serikali ipo makini sana katika kushughulikia suala hilo,” amesema Rais Samia
RAIS SAMIA AHUTUBIA BARAZA LA EID ELFITR VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
My take.
Chanjo ya corona aliyochanjwa Mbowe akiwa Dubai na akarudi mbio mbio kuhamasisha watanzania tuchanjwe haraka alijiridhisha madhara yake lini?
=====
Samia: Tutajiridhisha kabla ya kukubali chanjo ya corona
- Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ugonjwa wa Covid-19 umeathiri dunia nzima, ili kukabiliana nao lazima kushirikiana na mataifa mengine lakini Serikali itaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo matumizi ya chanjo ya ugonjwa huo.